LIVE UPDATES: Mkutano wa CCM Morogoro

LIVE UPDATES: Mkutano wa CCM Morogoro

Ninyi Magambaz waelezeni watanzania jinsi mlivyotekekeza ilani yenu ya maisha bora kwa kila mTZ, siyo mnabwabwaja tu majukwaani na kuponda chama pendwa CDM! Au ilani imekuwa CDM?
Shame on you Nepi and Jangili
 
Jamani hata mavazi ya chadema yanawatisha?
 
Naona chadema inawachanganya sana Ccm, kinana analia na chadema tu hana jingine, nimemshusha sana sikumtegemea namna hii, naanza kuhisi tabia za mwigulu, lusinde na nape nadhani ni yeye anaprogram
 
Mimi huwa ninajiuliza, hivi CCM wanapoitisha mikutano kama hiyo wanawaambia nini wananchi? Maana tangu watuahidi maisha bora kwa kila mtanzania mwaka 2005, hali yetu ya maisha imekuwa mbaya kuliko ya awali, sasa wakija kwa wananchi wanasema nini?

Wanawapa sababu za maisha kuwa magumu zaidi, wanawaambia wavumilie hali inarekebishwa au wanawaambia CHADEMA wamekwamisha utekelezaji wa sera za CCM? Na wananchi tuna nini cha kutufanya tuwaamini hawa watu ambao ndiyo chanzo cha umaskini wetu?

Yani inaleta ukakasi,mkutano mkubwa kama huu..badala ya kuongelea utekelezaji wa sera za chama,matatizo na suluhu zake,yani wao kila sentensi ni chadema,chadema,chadema...
 
Hivi huu mkutano ni kuhusu Chadema? Aaargh nani kanambia niangalie leo TBCCM

Suzie, umeona eh yaani neno cdm limetajwa zaidi ya neno ccm,hii inaonesha ni kiasi gani cdm inaogopwa na ccm,Chadema tuko strong hatuyumbi,na mwisho wa ccm ndo huu.
 
Wananchi ninyi ni mahodari kwny kazi,serikali haitoi ajira kwa kila mtu,tuwarahisishie watu fursa..wana morogoro mnamshikamano,mna umoja na nawahakikishia ccm ni chama madhubuti na kina viongozi mahiri, tulichoahidi tutatimiza.
 
Kama unataka habari za mkutano wa chadema nenda kwenye thread yake. Ipo kule ina comments nane tu tangu mchana.
kwa maana hizi pg 12 kwenye uzi huu mnasifiwa sana eeh! kweli akili ndogo...................................
 
Lakini badala ya kususa na kutangaza live kuwa hawataki huduma yake wangeacha jamii ione kama wanaonewa na ihukumu yenyewe. Waliposusa wameharibu kwa sababu sehemu kubwa ya jamii ilikuwa haijaona kama chadema inaonewa.
Nafikiri kususa hakukutokana na mikutano ya live, bali kulitokana na kutangaza matukio kinyumenyume. Na issue ilikuwa ni kuuawa kwa Mwangosi ambapo TBC walishadadia kifo kile huku wakikielezea CHADEMA kama chama cha vurugu ilihali ushahidi ulikuwa wazi. Ndiyo tangu pale CHADEMA wakatangaza mgogoro na TBC. Lakini nakubaliana na wewe pia kwamba badala ya CHADEMA kutangaza mgogoro na kuwasusia ambako wamewapa advantage, wangechukua hatua dhidi ya chombo hiki cha umma. Kwa kuwasusia ni kwamba wamekubali kodi zao ziliwe na TBC kwa kazi ya kukibeba CCM.
 
Mi si mshabiki sana wa siasa, ila mkuu UNATISHA:
Umejiunga JF APRI 8 (SIKU 13 ZILIZOPITA) hadi leo una post 732( WASTANI WA POST 56 KILA SIKU) zaid hata ya watu waliojiunga mwaka mmoja uliopita. Mkuu nijibu mawali yangu mawili tu
1. HUNA KAZI YA KUFANYA HAPA MJINI ZAIDI YA KUSHINDA JF NA KUPOST SIKU NZIMA?
2. UNALIPWA KWA KILA POST UNATUPIA JAMVINI?
3.JF MODS WAMEKOSEA IDADI YA POST ZAKO?


KWA KWELI NIMESHANGAZWA SANA WANA JF
Swali la kitoto na kama siyo la kitoto basi bado unaishi katika dunia ya zama za mawe.

Watu wana investment zao, wanaishi kwa interest. Usilinganishe maisha yako naya wengine.

Wewe unafikiria jinsi ya kupata pesa wengine wanafikiria jinsi ya kutumia.

Wewe endelea na kazi za kuvuja jasho and mind your own life. dude.
 
1.+KINANA+NA+NAPE+WAKIINGIA+UWANJANI+MJINI+MOROGORO.jpg



Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakiingia kwenye Uwanja wa mkutano wa hadhara wa CCM mjini Morogoro.


Wananchi wakishangilia wakati wa mkutano huo

Maelfu wakiwa wamefurika kwenye mkutano wa CCM uliofanyika mkoani Morogoro jioni hii

Msanii Nasibu Abdul 'Diamond' akibebwa na wasanii wake kukoleza, alipotumbuiza kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika mjini Morogoro leo jioni

Diamond akitumbuiza kwenye mkutano wa CCM uliofanyika jioni hii mjini Morogoro

Msanii Lina akitumbuiza kwenye mkutano huo

Wasanii Chege na Temba kutoka TMK Family wakishambulia jukwaa wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika kwenye mjini Morogoro jioni hii









 
nimechoka kulipia show za wasanii bora mtembee tu nchi nzima na hao wasanii wenu
kumbuken kula na kura ni maneno tofaut
 
Yani inaleta ukakasi,mkutano mkubwa kama huu..badala ya kuongelea utekelezaji wa sera za chama,matatizo na suluhu zake,yani wao kila sentensi ni chadema,chadema,chadema...
Itakuwa ngumu sana kwao kuongelea ya CCM kwa kuwa hawana lililo positive. Mengi ya mambo waliyonayo yana mwonekano hasi mbele ya jamii, kwahiyo wanaamua kujikita kwenye kuwasakama wapinzani wao ili watu waone CCM ina unafuu kuliko wapinzani.
 
Mkuu tukiacha uongo watu ni wengi balaa ukipinga unatatizo
 
Diamond on the stage now...the can is about to get kicked down the road now.
And TBC goose offair.
 
Pro-CHADEMA bana,

Wanang'ang'ana na vi-comment vyao vya kitotot wakati mikutano unapatikana katika njia zote za mawasiliano kwa Tanzania.

CCM haitembezi uongo kama CHADEMA. I'm sorry, kama huna macho na masikio.

Hakuna propaganda hapa.
 
Ushuhuda wa mafuriko ya morogoro haya hapa!
 

Attachments

  • download_1_.jpg
    download_1_.jpg
    101.6 KB · Views: 69
Back
Top Bottom