Live Updates: Mdahalo wa katiba ITV leo

Live Updates: Mdahalo wa katiba ITV leo

Huwezi kuua hatua mojawapo Kati ya hizo NNE ukasema unaunda katiba
 
IL: aliyeua mchakato wa katiba mpaka sasa anajulikana.... na kilichofanya mpaka sisi tutoke nje ni kwa sababu wenzentu walibandilisha moyo wa rasimu ya katiba.
TL: sheria ya rasimu ya katiba ina hatua nne:
i) kuunda tume kwa lengo la kukusanya maoni.
ii) tume kuandaa rasimu ya katiba mpya na kuipeleka kwa wadau ili waijadili.
iii) bunge maalumu kujadili na kupitisha rasimu ya katiba mpya
iv) wananchi kuipigia kura rasimu ya katiba mpya ili iwe sheria kamili na kuunda katiba mpya.
 
Hoja ni kwamba katika hatua NNE sio haki kwa BMK kuua kauli ya wananchi na kuunda jambo jipya
 
Lisu: anasisitiza kuwa hatua zote 4 zinategemeana... anatoa historia ya mabunge maalumu ya katiba, anafafanua kuwa ktk hizo hatua 4 ... Bunge Maalum haliwezi kubadilisha ama kukanusha kauli za wananchi na kutoka na kitu kipya ... Nafasi kwa wassira sasa...
 
Lipumba:Muundo wa muungano ndio moyo wa rasimu
 
Sasa ni zamu ya Wassira....anasema amekuja kwenye mdahalo....hivyo watu wa social media waandike kuwa amekuja
 
wasira anasema watu wa social media walisema sitakuja but nmekuja
 
JF oyeeee!! Wassira alisoma hapa kapigwa madongo mpaka ikabidi aje, mwenyewe kakubali
 
Katiba ina sura mbili....sura ya sheria na pili maridhiano
 
Tundu Lissu anaongea kuna hatua nne ktk mchakato wa katiba. Utaratibu wa sasa hivi ni tofauti kabisa na taratibu nyingine tulizowahi kuwa nazo. Ugomvi je BMK lina uwezo wa kubadili maoni yasiyotokana na wananchi
 
Lipumba:Wenzetu walikuja kwenye bunge maalumu na mkakati wa kuuwa moyo wa rasimu ya katiba
 
Ndugu wanabodi,

Msisahau kufuatilia mdahalo wa Katiba utakaorushwa live na ITV. Watoa mada ni Prof Ibrahim Lipumba, Tundu Lissu, Ally Awadhi, na Humprey Polepole.

Pia alialikwa Steven Wassira lakini inasemekana ameingia mtini, hatakuwepo.

Naomba tufuatilie mdahalo huu kwani itatoa mwelekeo mzuri wa mwenendo wa Rasimu ya katiba ambayo sasa ipo njiapanda. Tuachane na propaganda za CCM ambao hawana nia nzuri na upatikanaji wa Katiba.

KARIBUNI

comrade wasira ndani ya nyumba...
 
Wassira: wale watu wa social media walisema kuwa hatahudhuria sasa waandike kuwa amehudhuria. Wasira: katiba inasura mbili, tume imefanyakazi ya kukusanya maoni, anasema kuwa Sisi wanasiasa tunauwezo mkubwa sana wa kusingizia wananchi! Lisu alishiriki sana ktk kutengeneza sharia!
 
Back
Top Bottom