CHADEMA fahamuni kwamba Katiba mpya haina uwezo wa kuwapelekeni Ikulu

Trump2

JF-Expert Member
May 28, 2017
1,553
2,000
Hivi tunahitaji katiba mpya au tunahitaji kiongozi mwenye utashi wa kisiasa? Mpaka sasa Magufuli anatumia katiba ile ile aliyoikuta ila mambo yananyooka vizuri mno.Tuachane na hayo hebu tuangalie wanasiasa hasa wapinzani kwa nini wanapiga kelele kuhusu mchakato wa katiba mpya.

Kila mpinzani ukimuuliza kwa nini walishindwa uchaguzi wa 2015 watataja mambo makuu yafuatayo:-

1. Wanadai kuwa Tume ya Uchaguzi sio huru.

2. Katiba ya zamani ndio iliywashindisha CCM hivyo katiba mpya itawashindisha upinzani.

3. CCM waliiba Kura.

Muulize yeyote awe Lowassa aliyegombea uraisi na kushindwa, awe mbowe aliyebadili Gia angani au awe mfuasi aliyekuwa anatengeneza mafuriko wote majibu yao ni hayo. Hili la CCM kuiba kura sintolijadili kwa kuwa halina ushahidi na iweje muibiwe kura wakati kila kituo kulikuwepo na wakala wenu??

Na hitimisho lao wanasema mchakato wa katiba mpya ukikamilika basi watashinda uchaguzi mkuu ujao. Kila chama cha upinzani kinadai katiba mpya ya warioba ili kiweza kuingia Ikulu. Kwao hawana sera za kushawishi wananchi bali wanataka kukanyaga ganda la ndizi (Katiba) waende Ikulu. Hata Lowassa naye anaimba kuhusu katiba mpya.

Tuachane nalo twende tuingalie rasimu ambayo itapigiwa kura na ikipitishwa itakuwa katiba mpya ambayo upinzani wanadai kuwa kupitia hiyo watashinda.

HOJA YAO WAPINZANI

Upinzani unasema kuwa upatikanaji wa Tume ya taifa ya uchaguzi hauifanyi tume hiyo kuwa huru. Ni hoja ya ukweli kabisa kwani katiba ya zamani ibara ya 74 pamoja na ibara zake ndogo zinampa mamlaka makubwa sana ya raisi aliyepo madarakani kumteua mwenyekiti na makamu mwenyekiti. Nainukuu ibara hiyo:-

Ibara ya 74.

Ibara ndogo ya (1),
Kutakuwa na Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano ambayo itakuwa na wajumbe wafuatao watakaoteuliwa na Rais:-

(a) Jaji wa Mahakama Kuu au Jaji wa Mahakama ya Rufani, ambaye atakuwa mwenyekiti;

(b) Makamu Mwenyekiti ambaye atakuwa mtu anayeshika, aliyewahi kushika au anayestahili kuteuliwa kushika madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu au Jaji wa Mahakama ya Rufani;

(c) wajumbe wengine watakaotajwa na sheria iliyotungwa na Bunge.

Ibara ndogo ya (2),
Rais atamteua Makamu wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi kwa kufuata kanuni kwamba endapo Mwenyekiti ni mtu anayetoka sehemu moja ya Muungano, Makamu wake atakuwa ni mtu anayetoka sehemu ya pili ya Muungano.

Kosa kubwa hapa ambalo wapinzani wanalilalamikia ni Raisi kupewa mamlaka ya kuteua wajumbe hao......

KATIBA PENDEKEZWA INASEMAJE KUHUSU KUPATA TUME YA UCHAGUZI?

Sijui kama wapinzani au wanaoililia katiba mpya kama wameisoma katiba hiyo pendekezwa. Kama wameisoma vizuri wasingelipiga kelele hizi.

Kwenye hoja ya kwanza ya tume ya uchaguzi kutokuwa huru katiba pendekezwa inasemaje kuhusu tume huru ya uchaguzi?? nanukuu toka katiba pendekezwa.

TUME HURU YA UCHAGUZI

(a) Tume Huru ya Uchaguzi.

211.-(1) Kutakuwa na Tume Huru ya U chaguzi ya Jamhuri ya Muungano itakayoitwa “Tume Huru ya Uchaguzi”.

(2) Tume Huru ya Uchaguzi itakuwa na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wengine saba watakaoteuliwa na Rais baada ya kupendekezwa na Kamati ya Uteuzi.

(3) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi watashika madaraka mara baada ya kuapishwa na Rais.

(4) Uteuzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya
Uchaguzi utafanywa kwa misingi kwamba, endapo Mwenyekiti atateuliwa kutoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano, basi Makamu Mwenyekiti atateuliwa kutoka upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano.

(5) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi
watakuwa na sifa zifuatazo:-

(a) awe ni raia wa kuzaliwa, na angalau mmoja kati ya wazazi wake ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano;

(b) awe ni mtu aliyewahi kushika nafasi ya madaraka ya Jaji wa
Mahakama ya Juu, Mahakama ya Rufani au Mahakama Kuu na
ameshika nafasi ya madaraka hayo kwa kipindi kisichopungua miaka mitano;

(c) awe ni mwaminifu, mwadilifu na mwenye mwenendo usiotiliwa
shaka na jamii; sifa nyingine zinaendelea.................ila tuishie kwa sifa hizi.

Goli walilofungwa wapinzani kwenye katiba ya 1977 wanafungwa tena goli kama hilo kwenye katiba pendekezwa kama ikipita. Baada ya tume ya uteuzi kupitisha majina bado raisi anakuwa mtu wa mwisho kuwateua na kuwaapisha. Hii ina maana lazma wajumbe hao kwa namna yoyote wawe na vinasaba na raisi kisiasa. Sijui kama mnajua nini maana ya tume ya uteuzi.

IPO HIVI.

Sheria yetu ya mabadiliko ya katiba inasema baada ya maoni ya wananchi kutumika kutengenezea Rasimu, Rasimu hiyo itapelekwa kwenye bunge maalumu la katiba kuijadili kifungu kwa kifungu. Jukumu mojawapo la Bunge hili ni kuboresha maoni yale na mwisho iandikwe katiba pendekezwa kwa nia ya kurudishwa kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura.

Kulikuwa hakuna maana yoyote ya kuunda bunge la katiba kama maoni yale yasingepata marekebisho ya bunge la katiba. Ninasema hivi kwa kuna vijana wengi wamekuwa wakidai kuwa wabunge walichakachua rasimu ya warioba. Si kweli kwa kuwa walitimiza takwa la kisheria katika hatua iliyowahusu ya kujadili na kuboresha walipoona panafaa.

Ipo hivi ukusanyaji wa maoni na kuyachambua na kutengeneza Rasimu haina tofauti sana na utafiti (research) Lengo la kuweka hatua ya bunge kujadili na kuboresha vipengele vya katiba ni katika kuondokana na bias za watafiti wenyewe (Tume).

Muafaka upo kwenye hatua ya Mwisho ya upigaji kura.Kwa wale waliosoma vizuri research watanielewa hiki ninachoongea hapa ni nini. Hapa nitazungumzia validity ya data za tume ya mzee warioba walizokusanya na kutuletea kama rasimu ya katiba mpya.

Kipengele cha validation ni muhimu sana kwenye tafiti ya aina yoyote ambapo mtafiti ataangalia vitu vingi sana kabla haja generalize data zake kwa watanzania wote.

Mfano katika maoni yale hakuna mahali popote wazanzibar walisema wanataka serikali 3 katika asilimia za watu wote waliohojiwa toka zanzibar walisema wanataka serikali mbili na wengine wakadai kuwa wanataka serikali ya mkataba. Ila katika rasimu kuna option ya serikali mbili. Hata kwa upande wa Tanzania bara asilimia ndogo sana wanadai kuwa walikuwa wanataka serikali mbili.

Ni makosa kusema kuwa bunge la katiba lilichakachua rasimu ya katiba. Sema kwa nafasi yao walirekebisha maoni ya rasimu ya katiba kwa kadri walivyoona inafaa.

Kwa mujibu wa sheria ile hatua iliyobakia ni moja tu kupigia kura katiba pendekezwa. Hakuna uwezekano wa kurudi nyuma tena....

CCM ITAKWENDA KINYUME NA ILANI YAKE?

Ilani ya CCM inadai kuwa mchakato wa katiba mpya utaendelezwa pale ulipoishia ambapo ni kwenye hatua ya kuipigia kura.

Someni ilan ya CCM mtaona kuwa hakuna uwezekano wa kurudi nyuma.

Kama mnakumbuka Magufuli alivyochukua form ya uraisi yeye alisema hana cha kuahidi sana ila ataitekeleza ilani ya CCM kwa asilimia Zote. Sasa tuangalie ilani ya CCM inasema nini kuhusu katiba mpya:-

Kipengele cha "Utawala Bora, Demokrasia na Uwajibikaji" Ukurasa wa 163 katika ilani ya CCM Kipengele (e) kinasema nanukuu

"Mchakato wa kutungwa kwa Katiba mpya umeendeshwa na umefikia hatua ya Katiba Inayopendekezwa iliyopitishwa na Bunge Maalumu la Katiba ambayo itapigiwa Kura ya Maoni na wananchi"

Ukurasa wa 164 kipenge (g) Kinasema nanukuu "Kukamilisha mchakato wa kutunga Katiba mpya na kuanza kuitekeleza kwa
mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba"

Kwa kuwa ilani ya uchaguzi ndio dira ya uongozi ulioingia madarakani, kwa kuwa mchakato wa katiba mpya ulifuata sheria yake ya uchaguzi na kwa kuwa kilichosababisha mchakto huu kusimama ni siku kutokutosha kwa wananchi kujiandikisha na kuipigia kura sioni mahali au hoja itakayoletwa na Ukawa mchakato huu kuanza upya. Kwa vipengele hivi vya ilani ya ccm na kwa msimamo wa Magufuli kutekeleza ilani ya CCM basi mjadala huu umefungwa. Hapa ndipo CCM iliposhinda kabla ya kuingia vitani.

Katiba hii inamtaka raisi kufanya maamuzi ya Mwisho nani awe Mwenyekiti wa Tume baada ya kamati ya uteuzi kumfikishia majina ya walioomba kuwa mwenyekiti wa Tume na Makamu mwenyekiti. Kwa kipengele hiki tayari naona madhara ya UKAWA KUTOKA bungeni wakati wa kujadili rasimu hii. Haya tuambieni mtashindia wapi??

Anayepaswa kuwa mwenyekiti na makamu mwenyekiti lazma wawe na na sifa ya kuwa hapo awali walishakuwa majaji either mahakama kuu au mahakama ya rufaa, Nafikiri mnajua uteuzi wa majaji katika mahakama kuu au mahakama ya rufaa kwa hiyo moja kwa moja watu hawa watakuwa ni watu ambao walishawahi kuonja incentives za Ofisi ya Raisi. Nafikiri tunaelewana hapa kwa pamoja hawa walishawahi kuteuliwa na Raisi kuwa majaji sasa wanakuja kuwa wasimamizi wa Tume...... haya niambieni mnashindia wapi??

Hoja hii inajibu na hoja ya pili ya nyie kudai Katiba mpya ..... labda mniambie katiba mpya inalazmisha watu wote Tanzania kuwachagueni.

Lakini katiba mpya inaruhusu matokeo ya Uraisi kupingwa mahakamani. Ila nileteeni kesi ya namna hii iliyowahi kushinda hapa Africa.Tutaendelea kuijadili Rasimu hii kuelekea kura ya maoni.

Katiba mpya si suluhu ya UKAWA kwenda Ikulu.

Ole Mushi.
0712 702602
 
mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
53,442
2,000
Rudisheni mchakato wa kudai Katiba mpya alafu maraa paap imepatikana....
Muone kama mtasalia madarakani

Ova
 
SODIUM CYANIDE

JF-Expert Member
Jun 5, 2013
676
1,000
Katiba mpya ni kwa manufaa ya jamii nzima ya kitanzania. Hata kama chadema wasipoingia madarakani lakini jamii nzima itanufaika kwayo.
Hivyo ni muhimu mchakato wa katiba mpya urudishwe mezani haraka iwezekanavyo.
 
kauga JR

JF-Expert Member
Mar 4, 2015
3,512
2,000
Wao wenyewe wabadilike, waache kufanya chama kama SACCOS, na waakisi kiuhalisia neno DEMOCRACY, mwenyekiti awe anapigiwq kura na sio awe AMEKIONA chama na wanachama.
 
zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
12,900

Mbowe mbona kapigiwa kura 2004....2009 na 2013 au ulitaka apate kura 0 ndio uone kuna demokrasia??
 
Maxmizer

JF-Expert Member
Aug 14, 2016
4,819
2,000
huyu sijui wa wapi anachojua katiba mpya ina manufaa kwa chadema akili gani hizi
 
zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
12,900
2,000
Mtoa mada acha kupotosha CHADEMA hawakudai katiba mpya kwa ajili ya tume huru tu kuna mambo mengi wanayapinga hasa kuhusu mchakato Mzima wa bajeti.... Uendeshaji wa bunge.... Upatikanaji wa mawaziri.... Kupunguza gharama serikalini kwa kupunguza vyeo visivyokuwa na tija kma wakuu wa wilaya.... Kupunguza majimbo na wabunge kuweza kuwajibishwa na wananchi n.k sasa hayo yote huoni kma rasimu ya warioba ingenufaisha hata CCM

Mfano tume huru ikija alafu CCM mkashinda kihalali kabisa hamuoni mtakuwa mmejisafisha juu ya kelele za upinzani kuwa mnaiba kura??

Kingine wewe kama unaona katiba mpya haitowaingiza wapinzani ikulu si uwape benefit of doubt alafu baada ya hapo wakishindwa wasipate pa kujifichia au unaonaje??

Mfano mtoto analilia kwamba ukimpeleka english medium atafaulu kuliko ST kayumba sasa ww mzazi kwanini ukomae na kusema English medium haitokufanya ufaulu...... Kwanini usimpeleke alafu akifeli utakua umejivua lawama milele ndio hivyo hivyo CCM wekeni tume huru ikiwezekana hata UN isimamie chaguzi zetu alafu CHADEMA ikianguka basi mtakuwa mmefuta kelele za kuibiwa kura rejea tsvangirai 2013 kelele za kuibiwa zilikufa rasmi
 
zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
12,900
2,000
Sababu ya Zitto kuindoka CDM unaikumbuka au ulikuwa unanyonya maziwa.?
Eeeeh aliandika waraka wa kutaka kuweka mapandikizi ngazi za wilaya hadi taifa ili apite kwa kishindo.... Intelijentsia ikamgundua ikamchomoa leo hii wamekimbilia CCM mengine yote blah blah tu ila bila waraka asingetumbuliwa
 
bigmind

JF-Expert Member
Oct 28, 2015
12,326
2,000
Hivi tunahitaji katiba mpya au tunahitaji kiongozi mwenye utashi wa kisiasa? Mpaka sasa Magufuli anatumia katiba ile ile aliyoikuta ila mambo yananyooka vizuri mno.Tuachane na hayo hebu tuangalie wanasiasa hasa wapinzani kwa nini wanapiga kelele kuhusu mchakato wa katiba mpya.

Kila mpinzani ukimuuliza kwa nini walishindwa uchaguzi wa 2015 watataja mambo makuu yafuatayo:-

1. Wanadai kuwa Tume ya Uchaguzi sio huru.

2. Katiba ya zamani ndio iliywashindisha CCM hivyo katiba mpya itawashindisha upinzani.

3. CCM waliiba Kura.

Muulize yeyote awe Lowassa aliyegombea uraisi na kushindwa, awe mbowe aliyebadili Gia angani au awe mfuasi aliyekuwa anatengeneza mafuriko wote majibu yao ni hayo. Hili la CCM kuiba kura sintolijadili kwa kuwa halina ushahidi na iweje muibiwe kura wakati kila kituo kulikuwepo na wakala wenu??

Na hitimisho lao wanasema mchakato wa katiba mpya ukikamilika basi watashinda uchaguzi mkuu ujao. Kila chama cha upinzani kinadai katiba mpya ya warioba ili kiweza kuingia Ikulu. Kwao hawana sera za kushawishi wananchi bali wanataka kukanyaga ganda la ndizi (Katiba) waende Ikulu. Hata Lowassa naye anaimba kuhusu katiba mpya.

Tuachane nalo twende tuingalie rasimu ambayo itapigiwa kura na ikipitishwa itakuwa katiba mpya ambayo upinzani wanadai kuwa kupitia hiyo watashinda.

HOJA YAO WAPINZANI

Upinzani unasema kuwa upatikanaji wa Tume ya taifa ya uchaguzi hauifanyi tume hiyo kuwa huru. Ni hoja ya ukweli kabisa kwani katiba ya zamani ibara ya 74 pamoja na ibara zake ndogo zinampa mamlaka makubwa sana ya raisi aliyepo madarakani kumteua mwenyekiti na makamu mwenyekiti. Nainukuu ibara hiyo:-

Ibara ya 74.

Ibara ndogo ya (1),
Kutakuwa na Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano ambayo itakuwa na wajumbe wafuatao watakaoteuliwa na Rais:-

(a) Jaji wa Mahakama Kuu au Jaji wa Mahakama ya Rufani, ambaye atakuwa mwenyekiti;

(b) Makamu Mwenyekiti ambaye atakuwa mtu anayeshika, aliyewahi kushika au anayestahili kuteuliwa kushika madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu au Jaji wa Mahakama ya Rufani;

(c) wajumbe wengine watakaotajwa na sheria iliyotungwa na Bunge.

Ibara ndogo ya (2),
Rais atamteua Makamu wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi kwa kufuata kanuni kwamba endapo Mwenyekiti ni mtu anayetoka sehemu moja ya Muungano, Makamu wake atakuwa ni mtu anayetoka sehemu ya pili ya Muungano.

Kosa kubwa hapa ambalo wapinzani wanalilalamikia ni Raisi kupewa mamlaka ya kuteua wajumbe hao......

KATIBA PENDEKEZWA INASEMAJE KUHUSU KUPATA TUME YA UCHAGUZI?

Sijui kama wapinzani au wanaoililia katiba mpya kama wameisoma katiba hiyo pendekezwa. Kama wameisoma vizuri wasingelipiga kelele hizi.

Kwenye hoja ya kwanza ya tume ya uchaguzi kutokuwa huru katiba pendekezwa inasemaje kuhusu tume huru ya uchaguzi?? nanukuu toka katiba pendekezwa.

TUME HURU YA UCHAGUZI

(a) Tume Huru ya Uchaguzi.

211.-(1) Kutakuwa na Tume Huru ya U chaguzi ya Jamhuri ya Muungano itakayoitwa “Tume Huru ya Uchaguzi”.

(2) Tume Huru ya Uchaguzi itakuwa na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wengine saba watakaoteuliwa na Rais baada ya kupendekezwa na Kamati ya Uteuzi.

(3) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi watashika madaraka mara baada ya kuapishwa na Rais.

(4) Uteuzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya
Uchaguzi utafanywa kwa misingi kwamba, endapo Mwenyekiti atateuliwa kutoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano, basi Makamu Mwenyekiti atateuliwa kutoka upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano.

(5) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi
watakuwa na sifa zifuatazo:-

(a) awe ni raia wa kuzaliwa, na angalau mmoja kati ya wazazi wake ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano;

(b) awe ni mtu aliyewahi kushika nafasi ya madaraka ya Jaji wa
Mahakama ya Juu, Mahakama ya Rufani au Mahakama Kuu na
ameshika nafasi ya madaraka hayo kwa kipindi kisichopungua miaka mitano;

(c) awe ni mwaminifu, mwadilifu na mwenye mwenendo usiotiliwa
shaka na jamii; sifa nyingine zinaendelea.................ila tuishie kwa sifa hizi.

Goli walilofungwa wapinzani kwenye katiba ya 1977 wanafungwa tena goli kama hilo kwenye katiba pendekezwa kama ikipita. Baada ya tume ya uteuzi kupitisha majina bado raisi anakuwa mtu wa mwisho kuwateua na kuwaapisha. Hii ina maana lazma wajumbe hao kwa namna yoyote wawe na vinasaba na raisi kisiasa. Sijui kama mnajua nini maana ya tume ya uteuzi.

IPO HIVI.

Sheria yetu ya mabadiliko ya katiba inasema baada ya maoni ya wananchi kutumika kutengenezea Rasimu, Rasimu hiyo itapelekwa kwenye bunge maalumu la katiba kuijadili kifungu kwa kifungu. Jukumu mojawapo la Bunge hili ni kuboresha maoni yale na mwisho iandikwe katiba pendekezwa kwa nia ya kurudishwa kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura.

Kulikuwa hakuna maana yoyote ya kuunda bunge la katiba kama maoni yale yasingepata marekebisho ya bunge la katiba. Ninasema hivi kwa kuna vijana wengi wamekuwa wakidai kuwa wabunge walichakachua rasimu ya warioba. Si kweli kwa kuwa walitimiza takwa la kisheria katika hatua iliyowahusu ya kujadili na kuboresha walipoona panafaa.

Ipo hivi ukusanyaji wa maoni na kuyachambua na kutengeneza Rasimu haina tofauti sana na utafiti (research) Lengo la kuweka hatua ya bunge kujadili na kuboresha vipengele vya katiba ni katika kuondokana na bias za watafiti wenyewe (Tume).

Muafaka upo kwenye hatua ya Mwisho ya upigaji kura.Kwa wale waliosoma vizuri research watanielewa hiki ninachoongea hapa ni nini. Hapa nitazungumzia validity ya data za tume ya mzee warioba walizokusanya na kutuletea kama rasimu ya katiba mpya.

Kipengele cha validation ni muhimu sana kwenye tafiti ya aina yoyote ambapo mtafiti ataangalia vitu vingi sana kabla haja generalize data zake kwa watanzania wote.

Mfano katika maoni yale hakuna mahali popote wazanzibar walisema wanataka serikali 3 katika asilimia za watu wote waliohojiwa toka zanzibar walisema wanataka serikali mbili na wengine wakadai kuwa wanataka serikali ya mkataba. Ila katika rasimu kuna option ya serikali mbili. Hata kwa upande wa Tanzania bara asilimia ndogo sana wanadai kuwa walikuwa wanataka serikali mbili.

Ni makosa kusema kuwa bunge la katiba lilichakachua rasimu ya katiba. Sema kwa nafasi yao walirekebisha maoni ya rasimu ya katiba kwa kadri walivyoona inafaa.

Kwa mujibu wa sheria ile hatua iliyobakia ni moja tu kupigia kura katiba pendekezwa. Hakuna uwezekano wa kurudi nyuma tena....

CCM ITAKWENDA KINYUME NA ILANI YAKE?

Ilani ya CCM inadai kuwa mchakato wa katiba mpya utaendelezwa pale ulipoishia ambapo ni kwenye hatua ya kuipigia kura.

Someni ilan ya CCM mtaona kuwa hakuna uwezekano wa kurudi nyuma.

Kama mnakumbuka Magufuli alivyochukua form ya uraisi yeye alisema hana cha kuahidi sana ila ataitekeleza ilani ya CCM kwa asilimia Zote. Sasa tuangalie ilani ya CCM inasema nini kuhusu katiba mpya:-

Kipengele cha "Utawala Bora, Demokrasia na Uwajibikaji" Ukurasa wa 163 katika ilani ya CCM Kipengele (e) kinasema nanukuu

"Mchakato wa kutungwa kwa Katiba mpya umeendeshwa na umefikia hatua ya Katiba Inayopendekezwa iliyopitishwa na Bunge Maalumu la Katiba ambayo itapigiwa Kura ya Maoni na wananchi"

Ukurasa wa 164 kipenge (g) Kinasema nanukuu "Kukamilisha mchakato wa kutunga Katiba mpya na kuanza kuitekeleza kwa
mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba"

Kwa kuwa ilani ya uchaguzi ndio dira ya uongozi ulioingia madarakani, kwa kuwa mchakato wa katiba mpya ulifuata sheria yake ya uchaguzi na kwa kuwa kilichosababisha mchakto huu kusimama ni siku kutokutosha kwa wananchi kujiandikisha na kuipigia kura sioni mahali au hoja itakayoletwa na Ukawa mchakato huu kuanza upya. Kwa vipengele hivi vya ilani ya ccm na kwa msimamo wa Magufuli kutekeleza ilani ya CCM basi mjadala huu umefungwa. Hapa ndipo CCM iliposhinda kabla ya kuingia vitani.

Katiba hii inamtaka raisi kufanya maamuzi ya Mwisho nani awe Mwenyekiti wa Tume baada ya kamati ya uteuzi kumfikishia majina ya walioomba kuwa mwenyekiti wa Tume na Makamu mwenyekiti. Kwa kipengele hiki tayari naona madhara ya UKAWA KUTOKA bungeni wakati wa kujadili rasimu hii. Haya tuambieni mtashindia wapi??

Anayepaswa kuwa mwenyekiti na makamu mwenyekiti lazma wawe na na sifa ya kuwa hapo awali walishakuwa majaji either mahakama kuu au mahakama ya rufaa, Nafikiri mnajua uteuzi wa majaji katika mahakama kuu au mahakama ya rufaa kwa hiyo moja kwa moja watu hawa watakuwa ni watu ambao walishawahi kuonja incentives za Ofisi ya Raisi. Nafikiri tunaelewana hapa kwa pamoja hawa walishawahi kuteuliwa na Raisi kuwa majaji sasa wanakuja kuwa wasimamizi wa Tume...... haya niambieni mnashindia wapi??

Hoja hii inajibu na hoja ya pili ya nyie kudai Katiba mpya ..... labda mniambie katiba mpya inalazmisha watu wote Tanzania kuwachagueni.

Lakini katiba mpya inaruhusu matokeo ya Uraisi kupingwa mahakamani. Ila nileteeni kesi ya namna hii iliyowahi kushinda hapa Africa.Tutaendelea kuijadili Rasimu hii kuelekea kura ya maoni.

Katiba mpya si suluhu ya UKAWA kwenda Ikulu.

Ole Mushi.
0712 702602
Wewe ni msenge, tena narudia u msenge ata mie ni ssm ila umsenge wa kutupwa...! Elimu ndogo, akili ndogo, nadhani ata watoto wako wanakuzidi akili pusi wewe..!

Hivi katiba mpya na chadema wapi na wapi??? Agenda ya katiba why mnalazimisha iwe ya kiasa katiba mpya inakulinda ata wewe nyau unayedhania uko salama! Siku ukitofautiana na mtu anakuzidi mamlaka ndiyo utajua mbwa wewe..!
 
kauga JR

JF-Expert Member
Mar 4, 2015
3,512
2,000
Eeeeh aliandika waraka wa kutaka kuweka mapandikizi ngazi za wilaya hadi taifa ili apite kwa kishindo.... Intelijentsia ikamgundua ikamchomoa leo hii wamekimbilia CCM mengine yote blah blah tu ila bila waraka asingetumbuliwa
Tatizo CDM ni mbowe maan anatamaa mpak basi ameuza chama kwa EL mzee wa munduli anakichezea chama atakavyo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom