Live Updates: Bayern Munich vs Real Madrid

Live Updates: Bayern Munich vs Real Madrid

10154012_10152018722026333_3490482611395641469_n.jpg
 
Ule mpambano wa mechi ya marudiano kati ya Bayern Munich na Real Madrd ndio unakaribia kuanza

First Leg: Real Madrid 1 - Bayern Munich 0

LINE UPS:

Bayern Munich team: Neuer, Lahm, Boateng, Dante, Alaba, Robben, Schweinsteiger, Kroos, Muller, Ribery, Mandzukic.

Subs: Raeder, Van Buyten, Martinez, Rafinha, Pizarro, Gotze, Hojbjerg.

Real Madrid team: Casillas, Carvajal, Ramos, Pepe, Coentrao, Alonso, Modric, Di Maria, Ronaldo, Bale, Benzema.

Subs: Lopez, Varane, Marcelo, Casemiro, Isco, Illarramendi, Morata.

Half Time

Bayern 0 - Madrid 3 { Ramos 16", 20" : Ronaldo 34" }
hasante sana mkubwa kwa taarifa, hawa star times naona hawarushi game
 
rubaman

Baada ya mechi ya kwanza ya Madrid vs Bayern nilisoma sehemu Rais wa Bayern Franz Beckenbauer alilalamika style ya Bayern waliyotumia [pasi nyingi ambazo hazina mafanikio]

Sasa na leo wanavyotolewa hivi tena kwa kucheza kiwango cha chini sijui itakuwaje

Pundits baada ya mechi ya kwanza walishaanza kusema Bayern ya yule kocha {Mzee] kablaya ya Pep ilikuwa ni tishio kuliko hii ya sasa
 
Last edited by a moderator:
Kuna ukweli wadau wanataka kiisahau...iko hivi':
Buyern alibidi atolewe na Arsenal tangia kipindi kile, refa akaharibu mpira. Buyern kufika hapa now semi ni alinacha sana au ndondo kwa lugha rahisi.
 
Dakika ya 64

Madrid wanakosa goli

Huu mpira ni rahisi Madrid kufunga kuliko Bayern
 
Mpira huu siyo ule wa Kijerumani , acha wafungwe labda watatia akili! Wanakoswakoswa la 4 hapa, shenzi kabisa hawa!
 
Pamoja na kudominate Bundesliga Pep kaiharibu Bayern Munich. Timu iliyokuwa inatisha Europa misimu 2 iliyopita imebadilika kuwa kama tmu fulani ya mid-table Premier League.

Kroos, Bastian, muller.. always ni watu wa kujaribu mashuti mbali kila wanapopata nafas ya kushoot..lakin cha kushangaza mpaka kwenye 18 ya adui wamekuwa wanakaribu kupenetrate kwa pass fupifupi..

Inakera sana..hii siyo Bayern munich tulyoizoea!!!
 
yaani leo wamelala tayari tena kwao na watu wote hao
 
DonDonald, ile Bayern ya kile kibabu ilikuwa kali ingebeba UCL back to back sema Chelsea walipata bahati ya mtende . Miaka yote aliyokuwa Barca Pep ameonyesha anajua kufundisha staili moja tu sasa timu zimeshajulia staili yake. Anyway inawezekana hana vipaji alivyokuwa navyo Barca lakini hii Bayern haiingii ndani ya Bayern iliyopita.
 
Ball Possession

Bayern 68 Madrid 32

Live score Bayern 0 Madrid 0

Hapa kuna tatizo sehemu, sasa faida ya kuwa unamiliki mpira ni nini?

Ohh mechi ya kwanza ugenini ball possession ilikuwa Madrid 30 Bayern 70 ila Madrid akashinda
 
Back
Top Bottom