Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,191
- 674
Picha inasema mengi kuliko yale tuwezayo kuyaeleza kwa ufasaha.
Hapa kuna unsanii.
Si kweli kwamba MH JK Kikwete amelala kwa sababu moja kuu.
Ukiangalia mkono wake wa kushoto, mkono wenye pete,unaonekana ukiwa out of Focus. Camera imeshindwa kuFocus mkono wa kushoto kama ilivyo weza Focus mkono wa kulia au mikono yote ya waheshimiwa pembeni mwa rais.
Camera kushindwa Kufocus mkono wa president kuna maana moja tu, mkono huo ulikuwa katika movement wakati picha inapigwa.
Haiwezekani mtu auchape usingingizi huku mkono wake mmoja ukiwa katika movement kiasi cha Camera kushindwa kuFocus.
Pia mguu wake wa kushoto unaonekana uko kwenye movement katika hali ya kukaa vizuri kwenye kigoda. Kwa ujumla president yuko live na katika movement na haonyeshi dalili yeyote kwamba alikuwa amelala.
Kwa hiyo maelezo kwamba President alikuwa amelala ni ya Usanii na sikubaliani nayo hata kidogo.
Mwenye utetezi mwingine aulete hapa.
hapa walitaka kuspinkiaina, ahsante mkuu kwa uchambuzi ulioenda shule