Live kutoka NMC-ARUSHA

Live kutoka NMC-ARUSHA

Jasho la Damu

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2011
Posts
956
Reaction score
120
Mkandarasi yupo site anapiga kazi balaa, vibarua wake wanajitaid kuweka uzio wa senyenge uwanja mzima, greda na makatapila yanatamba uwanjani. Vifusi vya mchanga na moram vinaingizwa na malori zaidi ya kumi. Hapa leo serikal imechukua pointi 3 dhidi ya Cdm.
 
Ila kwa plan za Kawaida lazima Mji uwe na official area for gathering!! Sasa wametenga wapi pengine? Au wameona Hawana Umuhimu wa Kufanya Mikusanyiko kama aliyofanya Pinda Mwanza Juzi? Duh Hii kali!!
 
Mkandarasi yupo site anapiga kazi balaa, vibarua wake wanajitaid kuweka uzio wa senyenge uwanja mzima, greda na makatapila yanatamba uwanjani. Vifusi vya mchanga na moram vinaingizwa na malori zaidi ya kumi. Hapa leo serikal imechukua pointi 3 dhidi ya Cdm.

nini kimekufurahisha!
 
M4C haizuiliki kamwe..tutafanya mkutano sehemu yeyote ile...chadema ipo ndani ya mioyo ya watu mkuu haipo viwanjani...:nono:
 
Vijana wako kwa pembeni na nyuso za huzuni. Serikal ingekuwa active siku zote kama leo hakika hata washington wasingetupata kwa maendeleo.
 
Ubabe usio na msingi... Ngoja tuone Meya wa Arusha kama amekubaliana na hili...
 
Nmc kashapewa bakhressa zamaaaani, viwanja navyo mnaambiwa "uzieni bidhaa za bakhressa"

ukifuatilia hata hiyo tenda mkandarasi kapewa kinyume na taratibu za ppra.
Kalaga baho!
 
Mkandarasi yupo site anapiga kazi balaa, vibarua wake wanajitaid kuweka uzio wa senyenge uwanja mzima, greda na makatapila yanatamba uwanjani. Vifusi vya mchanga na moram vinaingizwa na malori zaidi ya kumi. Hapa leo serikal imechukua pointi 3 dhidi ya Cdm.

Arusha ipo kazi. Hivi Uwanja wa NMC ni wa CCM kama ulivyo wa Sheikh Amri Abeid?
 
Ngoja nichape mwendo maana naona mkandaras na askari m1 wananiangalia kila saa wasije akanimwangosi bure
 
nashauri mkutano ufanyikie mianzini.barabara ikijifunga ndio waonyeshe pa kufanyia mkutano.
 
Uwanja wa Sahara mwanza ambapo Pinda alizomewa zamu yake lini? Zoezi hilo lina maswali mengi.
Wapi uwanja wa mikutano ya umma kama kampeni mbali mbali na siyo ya siasa tu.
Pili, wapi uwanja wa michezo isiyo rasmi ambayo wakazi wa jiji wanaweza kutumia kwa uhuru wakati wo wote kwa michezo au mazoezi ya mbali mbali.
 
Viwanja ni vingi sana Arusha...Kujenga eneo la NMC hbakutazuia kitu...Hata Kwa Mrombo sokoni tutaenda!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom