Chishango
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 875
- 363
Wakuu kama nilivyowaeleza jana kuwa kutakuwa na mkutano mkubwa hapa Mbamba Bay watu wanaendelea kumiminika uwanja wa Polisi hapa Mbamba Bay wakimsubiri Dk. Slaa.
Mch. msigwa ameshawasili hapa pamoja na viongozi wengine, katibu wa chama wilaya anamkaribisha mch. Msigwa naye anawasalimia wananchi na moja kwa moja anawaambia kuwa Rais wetu ni mtalii nchi ina rasilimali nyingi lakini inafilisiwa na wezi yaani CCM.
Bado dk. Slaa hajawasili.
UPDATE:
Dk slaa kawasili kwa helikopta analakiwa kwa vifijo na nderemo na vigelegele akina mama wanalala chini hali inayomzuia kuendelea kuelekea jukwaani ...hatimaye anapanda jukwaani anakaribishwa mara moja ili kwenda na wakati....anaanza kwa salaamu ya chama then anaomba radhi kwa kuchelewa anawaambia wanyasa kuhusu maendeleo chini ya serikali hii ya CCM wasahau kwani hawana jipya wamechoka hawana visheni....anagusia kuhusu safari za rais anawaambia wanyasa safari ya juzi ya JK ni ya 358 tangu aingie madarakani hana muda na watanzania na watz waliomchagua .......anaendelea.... CCM wana mpango a kuhujumu mchakato wa katiba mpya hawataki kuona katiba ya watanzania wote inapatikana....anawaambia wananchi kuwa zaidi ya 72% ya mapendekezo ya rasimu ya katiba mpya ni ya Chadema....anawaambia vijana wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu anamaliza na kuondoka kuendelea na ratiba maeneo mengine.

Leo Dr. Slaa akizungumza na wa Mbamba bay amesema safari ya mwisho ya JK ilikuwa ni ya 358.
Kama safari za JK zimefikia 358, yaani jumla yake ni karibu sawa na siku za mwaka mmoja; na kama tukisema kuwa katika kila safari alitumia siku 2 tu huko nje, basi ni sawa na kusema kuwa ha.tu.ku.wa na raisi kwa miaka miwili katika miaka minane ya JK ikulu. Kwa lugha nyingine: based on my assumption that JK spent only 2 days in each trip, basi ni sawa na kusema kuwa, asilimia 25% ya muda aliokaa JK ikulu ameutumia angani (nje ya nchi).