Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 57,103
- 128,722
Wanabodi
Niko hapa King Jada Hotel Morocco DSM: Kikao Kazi Kati ya Shirika la Nyumba la Taifa, NHC na Jukwaa la Wahariri, TEF.
Tuanze na wasilisho
Yaliyomo
Utangulizi q Matokeo ya Utendaji
Utekelezaji miradi
Vipaumbele
Hitimisho
1.0. UTANGULIZI
Ndugu zangu Wanahabari, awali ya yote nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu ambaye ametuwezesha kukutana nanyi siku hii ya leo tukiwa na afya njema.
Aidha, nitaeleza mwelekeo wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Shirika tangu tulivyoachana mara ya mwisho na mipango ya baadae tuliyo nayo.
Shirika la Nyumba la Taifa lilianzishwa mwaka 1962 kwa Sheria ya Bunge Na. 45 kwa lengo la kuwapatia wananchi makazi bora. Lilikuwa ni Shirika la kwanza kuanzishwa na Mwalimu Nyerere mwaka mmoja tu baada ya uhuru wa nchi yetu. Ili kutimiza lengo hilo, Shirika lilipatiwa ruzuku na Serikali (47%), mikopo kutoka iliyokuwa Benki ya Nyumba na Serikali ya Shirikisho ya Jamhuri ya Ujerumani Magharibi (40%) na lilichangia lenyewe 13% kutoka kodi za nyumba.
• Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) liliundwa upya kupitia Sheria ya Bunge Na. 2 ya mwaka 1990 kwa kuunganishwa na iliyokuwa Msajili wa Majumba lililoanzishwa mwaka 1971 kwa sheria Na. 13.
• Kupitia Sheria ya mwaka 1990, Shirika la Nyumba la Taifa lilikabidhiwa mali zote za Msajili wa Majumba. Baadaye sheria hii, ilirekebishwa kupitia Sheria ya Marekebisho (Miscellaneous Amendments Law) Na. 2 ya mwaka 2005 ambayo imerekebishwa tena mwaka 2025.
• Marekebisho hayo yaliyohusu marekebisho ya Sheria ya Ardhi Na. 4 ya mwaka 1999 na kufuta Sheria ya Udhibiti wa Kodi za Pango la Nyumba (Rent Restriction Act) Na. 17 ya mwaka 1984.
• Marekebisho ya sasa(2025) yamelenga kuliwezesha Shirika kutekeleza majukumu yake kiufanisi zaidi kwenye mazingira ya ushindani wa kibiashara katika soko la miliki.
2.0 MAJUKUMU YA SHIRIKA
• Kujenga nyumba za makazi na majengo mengine kwa ajili ya kuuza na kupangisha
• Kujenga majengo kulingana na mipango (schemes) iliyoidhinishwa na serikali
• Kuzalisha na kuwezesha uzalishaji wa vifaa vya ujenzi.
• Kusimamia miliki za majengo yake na ya wamiliki wengine ikiwa ni pamoja na kuyafanyia matengenezo na kukusanya kodi za pango
• Kuendesha shughuli za ushauri, upangaji na ukaandarasi wa ujenzi wa nyumba na majengo.
3.0 MUUNDO WA SHIRIKA
Mchanganuo wa Kurugenzi na Vitengo katika muundo wa sasa ni kama ifuatavyo:-
(a)Kurugenzi ya Ujenzi (b)Kurugenzi ya Usimamizi wa Miliki (c)Kurugenzi ya Uendelezaji Biashara na Masoko (d)Kurugenzi ya Ubunifu na Ushauri (e)Kurugenzi ya Fedha (f)Kurugenzi ya Mipango, Vihatarishi,Utafiti na Maendeleo
Mchanganuo wa Kurugenzi na Vitengo katika muundo mpya: (g)Kurugenzi ya Rasilimaliwatu na Utawala (h)Kurugenzi ya Usimamizi wa Ununuzi (i)Kurugenzi ya Huduma za Sheria
(j)Kurugenzi ya Ukaguzi wa ndani (k)Kitengo cha Habari na Uhusiano (l)Kitengo cha TEHAMA na (m)Ofisi za Mikoa- 24
4.0 MATOKEO YA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA SHIRIKA
Majukumu ya Shirika la Nyumba la Taifa yanatekelezwa kwa kuzingatia Mpango Mkakati wa Shirika wa Miaka 10 (2015/16 – 2024/25) ambao unalenga kuwezesha ujenzi wa nyumba na kusimamia rasilimali nyumba za Shirika.
Matokeo ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Shirika ni pamoja na:-
4.1. MAPATO
Katika miaka mitano(2019/20-2023/24) mapato ya Shirika yamekua kutoka TZS Bilioni 125 kwa mwaka hadi TZS 189 Bilioni sawa na asilimia 34.
Mapato ya mwaka 2023/24 ambayo yamekaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali yamefikia TZS 189 Bilioni.
DASHIBODI FEDHA (MIAKA MITANO)
MCHANGANUO WA MAPATO
4.2. FAIDA
Katika kipindi cha miaka mitano(2019/20 – 2023/24) Shirika lilipata faida ya TZS. 235.4 Bilioni. Ukuaji wa faida kwa miaka mitano ni asilimia 33.1.
Aidha, katika kipindi cha Julai 2023 hadi Juni 2024, Shirika limepata faida kabla ya kodi ya TZS 36.8 Bilioni sawa na asilimia 112.5 ya lengo hilo, kwa hesabu zilizokaguliwa na CAG.
4.3 THAMANI YA MALI ZA SHIRIKA Mtaji wa Shirika hadi kufikia Juni 2024 ilikuwa TZS. 5.5 Trilioni ikilinganishwa na mwaka uliopita TZS 5.08 Trillion.
4.4 KODI/GAWIO ZILIZOLIPWA SERIKALINI Katika kipindi cha miaka mitano(2019/20-2023/24) Shirika liliweza kulipa kodi mbalimbali serikalini zinazofikia TZS. 134.4 Bilioni.
Aidha, katika kipindi hicho cha miaka mitano(2019/20- 2023/24), Shirika lililipa Gawio kwa Serikali TZS. 9.85 Bilioni. Mwaka huu pekee 2025 Shirika limelipa gawio la TZS 5.5 Bilioni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akikabidhi tuzo kwa NHC baada ya Shirika kuongeza gawio lake kutoka Shilingi Bilioni 1 mwaka uliopita hadi kufikia Shilingi Bilioni 5.5 kwa mwaka huu wa fedha.
KODI NA GAWIO SERIKALINI
5.0 UTEKELEZAJI WA MIRADI
5.1 AINA YA MIRADI INAYOTEKELEZWA
1. Uboreshaji wa miji kwa kuvunja majengo ya zamani na kujenga mapya (Redevelopment)
2. 3. ─ Makazi ─ Biashara (majengo ya maofisi, maduka, hoteli na matumizi ya viwanda)
Vitovu vya miji (Satellite Cities) ─ Maendelezo ya miliki ─ Miradi ya Ubia ─ Uendelezaji miliki i.e. Makazi & Biashara
Miradi ya Nyumba za gharama nafuu au za kipato cha chini ─ Mpango wa muda mrefu ni kuwa kila Wilaya nchini zijengwe nyumba kulingana na mahitaji.
4. Miradi ya Ukandarasi
v Katika kipindi cha Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita, Shirika limejenga nyumba 5,399 zenye thamani ya shilingi bilioni 659.48 kwa ajili ya kuuza na kupangisha ambapo nyumba 3,217 ujenzi wake umekamilika na nyumba 2,182 ziko katika hatua mbalimbali za ujenzi na zinatarajiwa kukamilika ifikapo Juni, 2026
MIRADI INAYOTEKELEZWA.......
5.2. MIRADI YA UKANDARASI Katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita, Shirika limetekeleza miradi 67 ya ukandarasi yenye thamani ya bilioni 458.2 ambapo ujenzi wa miradi 57 umekamilika na miradi 10 ujenzi wake upo katika hatua mbalimbali za ujenzi.
Miradi iliyokamilika kwa asilimia kubwa ni pamoja na:_
Ujenzi wa Majengo ya Ofisi za Wizara nane (8) za Serikali eneo la Mtumba – asilimia 95
Soko la Kimataifa la Madini ya Tanzanite Mirerani- asilimia 96; v Kitengo cha Moyo cha Jakaya Kikwete (JKCI) asilimia 100; v Ghala la chakula Masasi Vijijini asilimia 100
Miundombinu kwa ajili ya tanuru (incinerator) la Mamlaka ya Dawa na
Vifaa Tiba (TMDA) eneo la Nala Jijini Dodoma –asilimia 100.
MIRADI YA UKANDARASI .............
Ujenzi wa majengo mengine unaendelea yakiwemo Shule ya Uchumi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 90;
Ofisi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Temeke Dar es Salaam ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 65;
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Jijini Dodoma umefikia asilimia 46 na Zanzibar umefikia asilimia
5.3 UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAZI/BIASHARA
Shirika linaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya nyumba za makazi kama ifuatavyo:-
i) Mpango wa ujenzi wa nyumba 5,000 za gharama ya kati chini kupitia mradi wa Samia Housing Scheme (SHS) ambao utekelezaji wake unaendelea. Mradi huu wa nyumba za kuuza na kupangisha unakusudia kuenzi kazi nzuri anazofanya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwemo kuwezesha upatikanaji wa mikopo ya ujenzi wa nyumba bora nchini.
- Asilimia 50 ya nyumba hizi zitajengwa katika Mkoa wa Dar es Salaam, asilimia 20 katika mkoa wa Dodoma na asilimia 30 zitajengwa katika mikoa mingine.
UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAZI/BIASHARA.....
Nyumba 560 zimejengwa katika eneo la Kawe Jijini Dar es Salaam na kuuzwa na sasa Shirika lipo katika hatua ya kuanza kukabidhi nyumba hizo kwa wanunuzi-asilimia 91 na gharama 48 Bilioni
Aidha mradi huu wa nyumba 5,000 unaotekelezwa kwa awamu, utagharimu takriban TZS. bilioni 466 sawa na dola za Kimarekani milioni 200.
Awamu ya pili ya utekelezaji wa mradi huu imeanza eneo la Medeli, Jijini Dodoma; na Kawe na Kijichi Jijini Dar es Salaam ambapo nyumba 908 zinajengwa.
Ujenzi wa nyumba 68 Iyumbu zimekamilika kwa asilimia 100
Mwonekano wa mchoro wa Samia Housing Scheme (SHS) II Kawe.
Shirika limekamilisha ujenzi wa nyumba 68 eneo la Iyumbu Jijini Dodoma
NYUMBA 68– IYUMBU ZIMEKAMILIKA
UJENZI WA NYUMBA ZA BIASHARA ..............
Jengo la Biashara Masasi (Mtwara) ujenzi umefikia asilimia 75 v Jengo la Biashara, Morogoro(2H) umefikia asilimia 80. v Jengo la biashara Mtanda limefikia asilimia 54
Miradi ya kimkakati iliyopo Mount Meru (Arusha); Tabora Commercial Complex (Tabora); Singida Shops (Singida); Kashozi
Complex (Kagera); Mkwakwani Plaza(Tanga), Uluguru Plaza(Morogoro), Iringa Commercial Complex(Iringa), Maghala ya biashara(Mtwara) na maduka ya biashara Ilala(Dar es Salaam) ujenzi wake umeshaanza.
MRADI WA JENGO LA BIASHARA MTANDA
5.4. UKAMILISHAJI WA MIRADI MIKUBWA ILIYOKUWA IMESIMAMA
Kazi ya ukamilishaji wa miradi iliyosimama tangu 2018 inaendelea kama ifuatavyo:-
i) MOROCCO SQUARE
v Mradi wa Morocco Square, mmoja kati ya miradi mitatu mikubwa ya makazi iliyokwama kuanzia mwaka 2018, sasa umekamilika na nyumba zake 100 zimeuzwa kikamilifu, maeneo ya biashara na ofisi yamepangishwa kwa umma.
v Ufanisi huu umewezekana baada ya Serikali ya Awamu ya Sita kutoa kibali cha kukopa shilingi bilioni 174 mwaka 2023 na
kuukwamua mradi huo wenye thamani ya TZS Bilioni 153. 51
(ii) KAWE 711
v Ujenzi wa Mradi wa Kawe 711 wenye thamani ya shilingi bilioni 169 umefikia asilimia 60 na unatarajiwa kukamilika Aprili 2026.
q Natoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha Shirika la Nyumba la Taifa kupata kibali cha kukopa shilingi bilioni 174 mwaka 2023. Fedha hizi zimesaidia kukamilisha Mradi wa Morocco Square uliokuwa umesimama kwa miaka mitano na kuanza ujenzi wa KAWE 711
(iii) GOLDEN PREMIER RESIDENCE
v Mradi wa Golden Premier Residence(GPR) wenye thamani ya shilingi Bilioni 127 uliopo Kawe, mazungumzo kati ya mkandarasi na Shirika yamekamilika na ujenzi unaendelea na utakamilika Septemba 2027.
(IV) PLOT.300 REGENT ESTATE
Mradi huu ulikuwa umesimama kwa muda na sasa tumeutangaza ili kupata mkandarasi wa kuendelea na ujenzi
Hatua hii inalenga kurejesha utekelezaji wa mradi huu uliokuwa umesimama tangu 2018, ili kuchochea maendeleo ya eneo la Regent Estate na Jiji kwa ujumla.
5.5. USANIFU NA USIMAMIZI WA MIRADI YA UJENZI
a) Usimamizi wa ujenzi soko la Kariakoo wenye thamani ya TZS. bilioni 28 umekamilika kwa asilimia 100. Mradi huu umeshakabidhiwa kwa Shirika la Masoko Kariakoo.
b) Usanifu na Usimamizi wa jengo la Ofisi ya Wizara ya Fedha na Mipango eneo la Mtumba umekamilika na ujenzi umefikia asilimia 92 na Mjenzi ni Kampuni ya Estim Construction;
Muonekano wa sasa wa jengo la Wizara ya Fedha .
USANIFU NA USIMAMIZI WA MIRADI YA UJENZI........ c) Usimamizi wa ujenzi wa jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais
(Mazingira) - ujenzi umefikia asilimia 90 na Mjenzi ni Suma JKT;
d) Usanifu na ujenzi wa jengo la soko la madini (Tanzanite) eneo la Mirerani Manyara – Usanifu umekamilika na ujenzi umefikia asilimia 96.
5.6 UTEKELEZAJI WA SERA YA UBIA
Kutokana na azma ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kufungua uchumi wa nchi na kushirikisha sekta binafsi ambayo ni injini ya maendeleo endelevu, Shirika lilifanya marekebisho ya Sera ya Ubia ambayo ilizinduliwa rasmi Novemba 16, 2022 Jijini Dar es Salaam.
Sera hii imechochea ushiriki wa sekta binafsi katika ujenzi wa majengo ya matumizi mbalimbali, ambapo jumla ya miradi 21 yenye thamani ya shilingi billioni 351 inaendelea kutekelezwa katika mikoa ya Dar es Salaam (17), Mwanza (3) na Iringa (1).
Shirika limeidhinisha miradi mingine 64 yenye thamani ya shilingi bilioni 607 na uchambuzi wa uwezo wa wawekezaji hao unaendelea kabla ya kupewa mikataba.
Utekelezaji wa miradi hii una manufaa makubwa ikiwemo kuongeza upatikanaji wa nyumba bora za makazi na biashara, kuongezeka kwa ajira kwa watanzania na kupendezesha mandhari ya miji yetu na wigo wa kodi na mapato ya Serikali.
5.6.1 USHIRIKISHWAJI WA WAPANGAJI KWENYE UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UBIA
NHC imeendelea kufanya vikao kadhaa na wapangaji wa eneo la Kariakoo na wapangaji wamepisha wabia kufanya uendelezaji unaokusudiwa.
Wapangaji waliokuwa wanalipa kodi vizuri wamehakikishiwa kurejeshewa upangaji wao pindi ujenzi wa majengo mapya utakapokamilika.
6.0. UKUSANYAJI WA KODI YA PANGO NA MADENI MENGINEYO
Shirika limepunguza madeni yake kutoka shilingi bilioni 27 hadi 22 baada ya kukusanya bilioni 5. Jitihada hizi zimewezekana kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha, Msajili wa Hazina na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kukusanya madeni ya serikali
Ili kukabiliana na changamoto za madeni, kampeni ya kukusanya kodi na malimbikizo kutoka kwa wadaiwa sugu, imeendelea kwa kutumia mikakati ifuatavyo:-
Kuchukua hatua kwa wadaiwa wasiozingatia masharti ya mikataba, ambapo wapangaji 150 wamevunjiwa mikataba yao.
Vilevile, Shirika linashirikiana na NIDA, Credit Information Reference Bureau na BRELA ili kuwapata wadaiwa wengine binafsi na kampuni zilizohama kwenye nyumba za Shirika.
Shirika limewapa notisi wadaiwa 100 ya kuhakikisha wanalipa madeni yao kabla ya kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
Wapangaji wote wa sasa na wa zamani wamelipa amana ya pango(security deposits) – Tuna amana zinazofikia TZS Bilioni 27.
7.0 UENDELEZAJI WA VITOVU VYA MIJI
Tunaendeleza Miji midogo ndani ya Mji Mkubwa (Satellite Towns) ya Luguruni (Ubungo), Salama Creek (Kigamboni), Kawe (Kinondoni), Safari city (Arusha Jiji) na eneo la Usa River (Meru).
8.0 MPANGO WA MATENGENEZO YA NYUMBA
Hadi tarehe 15 Mei, 2025, Shirika limekarabati na kuboresha nyumba 3,004 zilizopo kwenye majengo 205. Aidha, ukarabati wa nyumba 1,546 zilizopo kwenye majengo 45 unaendelea katika mikoa mbalimbali nchini.
Ukarabati huu ni endelevu na nyumba zote za Shirika zinatarajiwa kufanyiwa ukarabati mkubwa ifikapo 2026/27.
9.0 MIFUMO YA TEHAMA
Ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia duniani, mwanzoni mwa mwaka 2021, Shirika lilianza kutengeneza mfumo jumuishi “NHC Integrated System – NHC IS”.
Mfumo huu ulitengenezwa na wataalamu wa hapa nchini, wakisimamiwa kwa karibu na Kitengo cha TEHAMA cha Shirika.
NHC Integrated System – ERP
Mpaka sasa mfumo huu unawasiliana na mfumo wa malipo wa GePG na mfumo wa TRA kwa ajili ya taarifa za kodi ya ongezeko la thamani.
Inategemewa mfumo huu utaendelea kuunganishwa na mifumo mingine kadiri itakavyohitajika ili kurahisisha kazi za Shirika na kutoa huduma kikamilifu.
Aidha, Shirika linakamilisha mfumo wa NHC MOBILE APP utakaowezesha wateja kuwasilisha maoni na mambo mbalimbali ya kuboresha huduma za Shirika kwa kutumia simu za mkononi. Mfumo huu utakuwa tayari ifikapo Julai 2025
9.0 UDHIBITI WA MAPATO YA SHIRIKA:
Zimekuwepo juhudi mbalimbali za kudhibiti matumizi yasiyokuwa ya lazima na usimamizi madhubuti wa miradi ya ujenzi. Juhudi hizi zimeendelea kupunguza gharama za uendeshaji wa Shirika na kuliongezea Shirika mapato stahiki.
Ili kudhibiti matumizi katika miradi, Shirika limeweka kamera (CCTV) katika miradi yote mikubwa.
Aidha, tumefunga vifaa vya bayometriki (biometric fingerprint) ili kudhibiti malipo ya wafanyakazi katika miradi mikubwa ya Shirika. Hatua hizi zimeongeza tija na faida kwa Shirika.
10. TUZO TULIZOPATA v NHC Ilitunukiwa tuzo ya Mjenzi Bora wa Makazi ya Umma kwa Mwaka 2024 na Taasisi ya Global Construction.
NHC ilipewa tuzo na NBAA ya Uandaaji Bora wa Hesabu wa Mashirika ya Umma kwa kufuata Viwango vya Kimataifa vya Uandaaji wa Hesabu(IFRS).
NHC ilishinda Tuzo ya Mjenzi Bora wa Makazi ya Kuishi Afrika Mashariki kwa mwaka 2024(East Africa Construction Awards).
NHC imetunukiwa pia tuzo ya Mkandarasi Bora wa Makazi ya Kuishi – Tuzo za ZICA 2025 ka.ka Tuzo za Kimataifa za Ujenzi Zanzibar (Zanzibar Interna.onal Construc.on Awards – ZICA/
NHC imekabidhiwa che. cha kutambua udhamini wake ka.ka Mkutano wa 13 na 14 wa Wahariri Jijini Dodoma na Songea, kwa kuthamini mchango wa vyombo vya habari ka.ka kueneza mafanikio ya serikali.
NHC ilishika Nafasi ya Tatu ka.ka Uwasilishaji wa Taarifa za Kifedha – na kusifiwa kwa ubora uwasilishaji wa taarifa za kifedha miongoni mwa mashirika ya umma.
NHC wakipewa na Mheshimiwa Rais tuzo ya Shirika lililojibadilisha kiutendaji miongoni mwa Mashirika ya Umma Tanzania na kupata .ja kubwa
NHC ikikabidhiwa cheti cha kutambua udhamini wake ka.ka Mkutano wa 13 wa Wahariri jijini Dodoma, kwa kuthamini mchango wa vyombo vya habari kueneza mafanikio ya serikali.
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limepata tuzo ya heshima kwa kuwa mkandarasi bora wa nyumba za makazi ka.ka tuzo za Zanzibar International Construction Awards (ZICA) 2025!
11. UTEKELEZAJI WA SERA YA HUDUMA KWA JAMII
Shirika limeendeleza utekelezaji wa sera ya huduma kwa jamii (CSR) kwa kutoa michango katika sekta za elimu, afya, vijana, maendeleo ya jamii na michezo.
Katika kipindi cha miaka mitano(2020-2024) Shirika limetoa misaada kwa jamii ya TZS Bilion 1.42
Jedwali la Muhtasari wa Michango (Kwa TZS Mamilioni)
12. MWELEKEO WA SHIRIKA
Kuanzisha NYUMBANI BOND ambayo itawezesha Watanzania kununua hisa na hivyo kutunisha mapato ya Shirika ili liweze kujenga nyumba katika maeneo mbalimbali nchini.
Kujenga miradi ya kimkakati ili kukidhi mahitaji ya nyumba za biashara na Ofisi katika maeneo mbalimbali nchini
Kuendelea na ujenzi wa nyumba 5,000 za Samia Housing Scheme eneo la Medeli, Mtoni Kijichi, Kawe 711 na Iyumbu
13. HITIMISHO
Kwa kuzingatia umuhimu wa Sekta ya nyumba na uendelezaji milki, Shirika linaendelea kuchukua jitihada za dhati kuhakikisha kuwa sekta hii inastawi. Hatua zinazoendelea kuchukuliwa ni pamoja na:-
i) Kukamilisha miradi iliyokuwa imesimama hususan mradi wa Kawe 711 ili tija ya uwekezaji katika miradi hiyo ipatikane.
Kutafuta ardhi ya gharama nafuu pamoja na kutumia teknolojia inayopunguza gharama za ujenzi na vifaa vya ujenzi ili kuwezesha upatikanaji wa nyumba za gharama nafuu
Tunaendelea kuimarisha Kitengo chetu cha Utafiti ili kiweze kuleta matokeo chanya ya kusaidia ujenzi wa nyumba za gharama nafuu nchini.
Kuendelea kuboresha mawasiliano na vyombo vya habari kama mhimili muhimu wa kuwafikishia wananchi taarifa sahihi na kwa wakati. Hii itatuongezea mauzo ya bidhaa zetu na kuongeza mapato ya Shirika.
AHSANTENI KWA KUNISIKILIZA
Hamad Abdallah Hamad Mkurugenzi Mkuu Shirika la Nyumba la Taifa
Juni 16, 2025
Asante kwa kulisoma wasilisho hili.
Paskali
Niko hapa King Jada Hotel Morocco DSM: Kikao Kazi Kati ya Shirika la Nyumba la Taifa, NHC na Jukwaa la Wahariri, TEF.
Tuanze na wasilisho
WASILISHO KUHUSU UTENDAJI WA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA KWA WAHARIRI WA
VYOMBO VYA HABARI

| Viashiria fedha | Mwaka wa fedha | ||||
| 2019/2020 (Miezi 12) | 2020/2021 (Miezi 12) | 2021/2022 (Miezi 12 ) | 2022/2023 (Miezi 12) | 2023/2024 (Miezi 12) | |
| Kiasi kwashilingi Bilioni | |||||
| Mapato | 141.1 | 145.6 | 259.4 | 175.7 | 189.1 |
| Vyanzo vingine vya mapato pamoja na hisa ya faid | kwenye u0w.e9k | ezaji 1.0 | 1.5 | 0.5 | 1.3 |
| Matumizi taslimu ya uendeshaji | 101.7 | 112.8 | 196.3 | 133.3 | 136.6 |
| Faida taslimu ya uendeshaji | 40.4 | 33.8 | 64.6 | 42.9 | 53.7 |
| Faida ya uendeshaji (Ukitoa, kushuka kwa thamani, | futaji mad3e6n.i1, | asara ya ubad3i1lis.7h | ji fedha) 60.7 | 40.0 | 36.8 |
| Jumla ya rasilimali | 4,975.9 | 5,043.7 | 5,030.7 | 5,084.8 | 5,504.2 |
| Jumla ya Mtaji wa Hisa | 3,245.1 | 3,320.6 | 3,396.5 | 3,454.2 | 3,702.1 |
| Jumla ya Mikopo | 224.9 | 222.1 | 223.5 | 200.7 | 200.5 |
| Uwiano wa kukopa (benki) | 0.1 | 0.1 | 0.1 | 0.1 | 0.1 |
| Uwiano wa kukopa yakiwemo madeni yote | 0.1 | 0.1 | 0.1 | 0.1 | 0.1 |
| Gharama za nyumba za kupanga | 7.3 | 8.2 | 8.9 | 8.9 | 10.8 |
| Mchango katika Mfuko mkuu wa serikali | 1.2 | 1.2 | 0.8 | 1.2 | 1.2 |
MCHANGANUO WA MAPATO
| MAPATO | KIASI KWA SHILINGI MILIONI ZA KITANZANIA | ||||
| Mwaka Wa Fedha | 2019/2020 2020/2021 2021/2022 2022/2023 2023/2024 | ||||
| Kodi ya Pango | 89,520 | 89,230 | 91,204 | 90,205 | 95,035 |
| Mauzoyanyumba | 16,183 | 29,330 | 121,948 | 12,318 | 31,585 |
| MauzoyaUkandarasina | 33,579 | 25,601 | 43,984 | 56,309 | 52,820 |
| Mauzoyaviwanja | 578 | 264 | 773 | 10,740 | 7,220 |
| Mapatomengineyo | 1,269 | 1,183 | 1,508 | 6,173 | 2,410 |
| Jumla | 141,129 | 145,607 | 259,417 | 175,745 | 189,070 |
Katika kipindi cha miaka mitano(2019/20 – 2023/24) Shirika lilipata faida ya TZS. 235.4 Bilioni. Ukuaji wa faida kwa miaka mitano ni asilimia 33.1.
Aidha, katika kipindi cha Julai 2023 hadi Juni 2024, Shirika limepata faida kabla ya kodi ya TZS 36.8 Bilioni sawa na asilimia 112.5 ya lengo hilo, kwa hesabu zilizokaguliwa na CAG.
4.3 THAMANI YA MALI ZA SHIRIKA Mtaji wa Shirika hadi kufikia Juni 2024 ilikuwa TZS. 5.5 Trilioni ikilinganishwa na mwaka uliopita TZS 5.08 Trillion.
4.4 KODI/GAWIO ZILIZOLIPWA SERIKALINI Katika kipindi cha miaka mitano(2019/20-2023/24) Shirika liliweza kulipa kodi mbalimbali serikalini zinazofikia TZS. 134.4 Bilioni.
Aidha, katika kipindi hicho cha miaka mitano(2019/20- 2023/24), Shirika lililipa Gawio kwa Serikali TZS. 9.85 Bilioni. Mwaka huu pekee 2025 Shirika limelipa gawio la TZS 5.5 Bilioni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akikabidhi tuzo kwa NHC baada ya Shirika kuongeza gawio lake kutoka Shilingi Bilioni 1 mwaka uliopita hadi kufikia Shilingi Bilioni 5.5 kwa mwaka huu wa fedha.
KODI NA GAWIO SERIKALINI
| KODI MBALIMBALI NA GAWIO KWA SERIKALI | |||||
| AINA YA KODI/MCHANGO | 2019/2020 | 2020/2021 | 2021/2022 | 2022/2023 | 2023/2024 |
| Kodi ya Ongezeko la thamani (VAT) | 12,069,397,486 | 7,743,082,056 | 9,016,726,870 | 14,088,191,406 | 13,642,599,646 |
| Kodi ya mapato ya wafanyakazi (PAYE) | 3,755,275,940 | 3,336,351,471 | 3,789,957,516 | 3,756,300,587 | 4,029,952,812 |
| Kodi ya Zuio (WITHHOLDING TAX) | 920,881,957 | 1,177,929,294 | 1,246,100,162 | 1,010,821,110 | 1,422,467,356 |
| Kodi ya ufundi stadi (SKILLS AND DEVEL | OPME7N0T0,3L2E3V,Y8)97 | 595,762,458 | 679,471,896 | 701,590,663 | 651,096,401 |
| Kodi ya mapato ya Kampuni (CORPORA | E T6A, 7X7) 2 , 4 9 2 , 7 5 8 | 6,957,466,285 | 4,860,130,152 | 9,300,334,955 | 7,351,609,306 |
| Kodi ya Majengo (PROPERTYTAX) | 1,323,983,768 | 375,764,248 | 219,726,640 | 448,209,029 | 290,859,636 |
| Kodi ya Ardhi (LAND RENT) | 730,307,488 | 720,953,559 | 1,053,685,761 | 1,430,422,055 | 569,390,075 |
| Gawio (DIVIDEND) | 550,000,000 | 1,205,000,000 | 750,000,000 | 1,000,000,000 | 1,200,000,000 |
| Kodi ya biashara/leseni (IMPORT DUTY | AND B1U0S3I,N34E1S,S14L7I | ENCE2)24,650,621 | 2,400,000 | 2,900,000 | 58,809,000 |
| Ushuru wa manispaa/Majiji (CITYSERVI | CE LE3V9Y8) ,025,125 | 443,041,098 | 427,882,466 | 639,727,008 | 687,318,817 |
| JUMLA | 27,324,029,566 | 22,780,001,089 | 22,046,081,463 | 32,378,496,814 | 29,904,103,049 |
5.0 UTEKELEZAJI WA MIRADI
5.1 AINA YA MIRADI INAYOTEKELEZWA
1. Uboreshaji wa miji kwa kuvunja majengo ya zamani na kujenga mapya (Redevelopment)
2. 3. ─ Makazi ─ Biashara (majengo ya maofisi, maduka, hoteli na matumizi ya viwanda)
Vitovu vya miji (Satellite Cities) ─ Maendelezo ya miliki ─ Miradi ya Ubia ─ Uendelezaji miliki i.e. Makazi & Biashara
Miradi ya Nyumba za gharama nafuu au za kipato cha chini ─ Mpango wa muda mrefu ni kuwa kila Wilaya nchini zijengwe nyumba kulingana na mahitaji.
4. Miradi ya Ukandarasi
v Katika kipindi cha Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita, Shirika limejenga nyumba 5,399 zenye thamani ya shilingi bilioni 659.48 kwa ajili ya kuuza na kupangisha ambapo nyumba 3,217 ujenzi wake umekamilika na nyumba 2,182 ziko katika hatua mbalimbali za ujenzi na zinatarajiwa kukamilika ifikapo Juni, 2026
MIRADI INAYOTEKELEZWA.......
5.2. MIRADI YA UKANDARASI Katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita, Shirika limetekeleza miradi 67 ya ukandarasi yenye thamani ya bilioni 458.2 ambapo ujenzi wa miradi 57 umekamilika na miradi 10 ujenzi wake upo katika hatua mbalimbali za ujenzi.
Miradi iliyokamilika kwa asilimia kubwa ni pamoja na:_
Ujenzi wa Majengo ya Ofisi za Wizara nane (8) za Serikali eneo la Mtumba – asilimia 95
Soko la Kimataifa la Madini ya Tanzanite Mirerani- asilimia 96; v Kitengo cha Moyo cha Jakaya Kikwete (JKCI) asilimia 100; v Ghala la chakula Masasi Vijijini asilimia 100
Miundombinu kwa ajili ya tanuru (incinerator) la Mamlaka ya Dawa na
Vifaa Tiba (TMDA) eneo la Nala Jijini Dodoma –asilimia 100.
MIRADI YA UKANDARASI .............
Ujenzi wa majengo mengine unaendelea yakiwemo Shule ya Uchumi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 90;
Ofisi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Temeke Dar es Salaam ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 65;
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Jijini Dodoma umefikia asilimia 46 na Zanzibar umefikia asilimia
5.3 UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAZI/BIASHARA
Shirika linaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya nyumba za makazi kama ifuatavyo:-
i) Mpango wa ujenzi wa nyumba 5,000 za gharama ya kati chini kupitia mradi wa Samia Housing Scheme (SHS) ambao utekelezaji wake unaendelea. Mradi huu wa nyumba za kuuza na kupangisha unakusudia kuenzi kazi nzuri anazofanya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwemo kuwezesha upatikanaji wa mikopo ya ujenzi wa nyumba bora nchini.
- Asilimia 50 ya nyumba hizi zitajengwa katika Mkoa wa Dar es Salaam, asilimia 20 katika mkoa wa Dodoma na asilimia 30 zitajengwa katika mikoa mingine.
UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAZI/BIASHARA.....
Nyumba 560 zimejengwa katika eneo la Kawe Jijini Dar es Salaam na kuuzwa na sasa Shirika lipo katika hatua ya kuanza kukabidhi nyumba hizo kwa wanunuzi-asilimia 91 na gharama 48 Bilioni
Aidha mradi huu wa nyumba 5,000 unaotekelezwa kwa awamu, utagharimu takriban TZS. bilioni 466 sawa na dola za Kimarekani milioni 200.
Awamu ya pili ya utekelezaji wa mradi huu imeanza eneo la Medeli, Jijini Dodoma; na Kawe na Kijichi Jijini Dar es Salaam ambapo nyumba 908 zinajengwa.
Ujenzi wa nyumba 68 Iyumbu zimekamilika kwa asilimia 100
Mwonekano wa mchoro wa Samia Housing Scheme (SHS) II Kawe.
Shirika limekamilisha ujenzi wa nyumba 68 eneo la Iyumbu Jijini Dodoma
NYUMBA 68– IYUMBU ZIMEKAMILIKA
UJENZI WA NYUMBA ZA BIASHARA ..............
Jengo la Biashara Masasi (Mtwara) ujenzi umefikia asilimia 75 v Jengo la Biashara, Morogoro(2H) umefikia asilimia 80. v Jengo la biashara Mtanda limefikia asilimia 54
Miradi ya kimkakati iliyopo Mount Meru (Arusha); Tabora Commercial Complex (Tabora); Singida Shops (Singida); Kashozi
Complex (Kagera); Mkwakwani Plaza(Tanga), Uluguru Plaza(Morogoro), Iringa Commercial Complex(Iringa), Maghala ya biashara(Mtwara) na maduka ya biashara Ilala(Dar es Salaam) ujenzi wake umeshaanza.
MRADI WA JENGO LA BIASHARA MTANDA
5.4. UKAMILISHAJI WA MIRADI MIKUBWA ILIYOKUWA IMESIMAMA
Kazi ya ukamilishaji wa miradi iliyosimama tangu 2018 inaendelea kama ifuatavyo:-
i) MOROCCO SQUARE
v Mradi wa Morocco Square, mmoja kati ya miradi mitatu mikubwa ya makazi iliyokwama kuanzia mwaka 2018, sasa umekamilika na nyumba zake 100 zimeuzwa kikamilifu, maeneo ya biashara na ofisi yamepangishwa kwa umma.
v Ufanisi huu umewezekana baada ya Serikali ya Awamu ya Sita kutoa kibali cha kukopa shilingi bilioni 174 mwaka 2023 na
kuukwamua mradi huo wenye thamani ya TZS Bilioni 153. 51
(ii) KAWE 711
v Ujenzi wa Mradi wa Kawe 711 wenye thamani ya shilingi bilioni 169 umefikia asilimia 60 na unatarajiwa kukamilika Aprili 2026.
q Natoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha Shirika la Nyumba la Taifa kupata kibali cha kukopa shilingi bilioni 174 mwaka 2023. Fedha hizi zimesaidia kukamilisha Mradi wa Morocco Square uliokuwa umesimama kwa miaka mitano na kuanza ujenzi wa KAWE 711
(iii) GOLDEN PREMIER RESIDENCE
v Mradi wa Golden Premier Residence(GPR) wenye thamani ya shilingi Bilioni 127 uliopo Kawe, mazungumzo kati ya mkandarasi na Shirika yamekamilika na ujenzi unaendelea na utakamilika Septemba 2027.
(IV) PLOT.300 REGENT ESTATE
Mradi huu ulikuwa umesimama kwa muda na sasa tumeutangaza ili kupata mkandarasi wa kuendelea na ujenzi
Hatua hii inalenga kurejesha utekelezaji wa mradi huu uliokuwa umesimama tangu 2018, ili kuchochea maendeleo ya eneo la Regent Estate na Jiji kwa ujumla.
5.5. USANIFU NA USIMAMIZI WA MIRADI YA UJENZI
a) Usimamizi wa ujenzi soko la Kariakoo wenye thamani ya TZS. bilioni 28 umekamilika kwa asilimia 100. Mradi huu umeshakabidhiwa kwa Shirika la Masoko Kariakoo.
b) Usanifu na Usimamizi wa jengo la Ofisi ya Wizara ya Fedha na Mipango eneo la Mtumba umekamilika na ujenzi umefikia asilimia 92 na Mjenzi ni Kampuni ya Estim Construction;
Muonekano wa sasa wa jengo la Wizara ya Fedha .
USANIFU NA USIMAMIZI WA MIRADI YA UJENZI........ c) Usimamizi wa ujenzi wa jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais
(Mazingira) - ujenzi umefikia asilimia 90 na Mjenzi ni Suma JKT;
d) Usanifu na ujenzi wa jengo la soko la madini (Tanzanite) eneo la Mirerani Manyara – Usanifu umekamilika na ujenzi umefikia asilimia 96.
5.6 UTEKELEZAJI WA SERA YA UBIA
Kutokana na azma ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kufungua uchumi wa nchi na kushirikisha sekta binafsi ambayo ni injini ya maendeleo endelevu, Shirika lilifanya marekebisho ya Sera ya Ubia ambayo ilizinduliwa rasmi Novemba 16, 2022 Jijini Dar es Salaam.
Sera hii imechochea ushiriki wa sekta binafsi katika ujenzi wa majengo ya matumizi mbalimbali, ambapo jumla ya miradi 21 yenye thamani ya shilingi billioni 351 inaendelea kutekelezwa katika mikoa ya Dar es Salaam (17), Mwanza (3) na Iringa (1).
Shirika limeidhinisha miradi mingine 64 yenye thamani ya shilingi bilioni 607 na uchambuzi wa uwezo wa wawekezaji hao unaendelea kabla ya kupewa mikataba.
Utekelezaji wa miradi hii una manufaa makubwa ikiwemo kuongeza upatikanaji wa nyumba bora za makazi na biashara, kuongezeka kwa ajira kwa watanzania na kupendezesha mandhari ya miji yetu na wigo wa kodi na mapato ya Serikali.
5.6.1 USHIRIKISHWAJI WA WAPANGAJI KWENYE UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UBIA
NHC imeendelea kufanya vikao kadhaa na wapangaji wa eneo la Kariakoo na wapangaji wamepisha wabia kufanya uendelezaji unaokusudiwa.
Wapangaji waliokuwa wanalipa kodi vizuri wamehakikishiwa kurejeshewa upangaji wao pindi ujenzi wa majengo mapya utakapokamilika.
6.0. UKUSANYAJI WA KODI YA PANGO NA MADENI MENGINEYO
Shirika limepunguza madeni yake kutoka shilingi bilioni 27 hadi 22 baada ya kukusanya bilioni 5. Jitihada hizi zimewezekana kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha, Msajili wa Hazina na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kukusanya madeni ya serikali
Ili kukabiliana na changamoto za madeni, kampeni ya kukusanya kodi na malimbikizo kutoka kwa wadaiwa sugu, imeendelea kwa kutumia mikakati ifuatavyo:-
Kuchukua hatua kwa wadaiwa wasiozingatia masharti ya mikataba, ambapo wapangaji 150 wamevunjiwa mikataba yao.
Vilevile, Shirika linashirikiana na NIDA, Credit Information Reference Bureau na BRELA ili kuwapata wadaiwa wengine binafsi na kampuni zilizohama kwenye nyumba za Shirika.
Shirika limewapa notisi wadaiwa 100 ya kuhakikisha wanalipa madeni yao kabla ya kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
Wapangaji wote wa sasa na wa zamani wamelipa amana ya pango(security deposits) – Tuna amana zinazofikia TZS Bilioni 27.
7.0 UENDELEZAJI WA VITOVU VYA MIJI
Tunaendeleza Miji midogo ndani ya Mji Mkubwa (Satellite Towns) ya Luguruni (Ubungo), Salama Creek (Kigamboni), Kawe (Kinondoni), Safari city (Arusha Jiji) na eneo la Usa River (Meru).
8.0 MPANGO WA MATENGENEZO YA NYUMBA
Hadi tarehe 15 Mei, 2025, Shirika limekarabati na kuboresha nyumba 3,004 zilizopo kwenye majengo 205. Aidha, ukarabati wa nyumba 1,546 zilizopo kwenye majengo 45 unaendelea katika mikoa mbalimbali nchini.
Ukarabati huu ni endelevu na nyumba zote za Shirika zinatarajiwa kufanyiwa ukarabati mkubwa ifikapo 2026/27.
9.0 MIFUMO YA TEHAMA
Ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia duniani, mwanzoni mwa mwaka 2021, Shirika lilianza kutengeneza mfumo jumuishi “NHC Integrated System – NHC IS”.
Mfumo huu ulitengenezwa na wataalamu wa hapa nchini, wakisimamiwa kwa karibu na Kitengo cha TEHAMA cha Shirika.
NHC Integrated System – ERP
Mpaka sasa mfumo huu unawasiliana na mfumo wa malipo wa GePG na mfumo wa TRA kwa ajili ya taarifa za kodi ya ongezeko la thamani.
Inategemewa mfumo huu utaendelea kuunganishwa na mifumo mingine kadiri itakavyohitajika ili kurahisisha kazi za Shirika na kutoa huduma kikamilifu.
Aidha, Shirika linakamilisha mfumo wa NHC MOBILE APP utakaowezesha wateja kuwasilisha maoni na mambo mbalimbali ya kuboresha huduma za Shirika kwa kutumia simu za mkononi. Mfumo huu utakuwa tayari ifikapo Julai 2025
9.0 UDHIBITI WA MAPATO YA SHIRIKA:
Zimekuwepo juhudi mbalimbali za kudhibiti matumizi yasiyokuwa ya lazima na usimamizi madhubuti wa miradi ya ujenzi. Juhudi hizi zimeendelea kupunguza gharama za uendeshaji wa Shirika na kuliongezea Shirika mapato stahiki.
Ili kudhibiti matumizi katika miradi, Shirika limeweka kamera (CCTV) katika miradi yote mikubwa.
Aidha, tumefunga vifaa vya bayometriki (biometric fingerprint) ili kudhibiti malipo ya wafanyakazi katika miradi mikubwa ya Shirika. Hatua hizi zimeongeza tija na faida kwa Shirika.
10. TUZO TULIZOPATA v NHC Ilitunukiwa tuzo ya Mjenzi Bora wa Makazi ya Umma kwa Mwaka 2024 na Taasisi ya Global Construction.
NHC ilipewa tuzo na NBAA ya Uandaaji Bora wa Hesabu wa Mashirika ya Umma kwa kufuata Viwango vya Kimataifa vya Uandaaji wa Hesabu(IFRS).
NHC ilishinda Tuzo ya Mjenzi Bora wa Makazi ya Kuishi Afrika Mashariki kwa mwaka 2024(East Africa Construction Awards).
NHC imetunukiwa pia tuzo ya Mkandarasi Bora wa Makazi ya Kuishi – Tuzo za ZICA 2025 ka.ka Tuzo za Kimataifa za Ujenzi Zanzibar (Zanzibar Interna.onal Construc.on Awards – ZICA/
NHC imekabidhiwa che. cha kutambua udhamini wake ka.ka Mkutano wa 13 na 14 wa Wahariri Jijini Dodoma na Songea, kwa kuthamini mchango wa vyombo vya habari ka.ka kueneza mafanikio ya serikali.
NHC ilishika Nafasi ya Tatu ka.ka Uwasilishaji wa Taarifa za Kifedha – na kusifiwa kwa ubora uwasilishaji wa taarifa za kifedha miongoni mwa mashirika ya umma.
NHC wakipewa na Mheshimiwa Rais tuzo ya Shirika lililojibadilisha kiutendaji miongoni mwa Mashirika ya Umma Tanzania na kupata .ja kubwa
NHC ikikabidhiwa cheti cha kutambua udhamini wake ka.ka Mkutano wa 13 wa Wahariri jijini Dodoma, kwa kuthamini mchango wa vyombo vya habari kueneza mafanikio ya serikali.
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limepata tuzo ya heshima kwa kuwa mkandarasi bora wa nyumba za makazi ka.ka tuzo za Zanzibar International Construction Awards (ZICA) 2025!
11. UTEKELEZAJI WA SERA YA HUDUMA KWA JAMII
Shirika limeendeleza utekelezaji wa sera ya huduma kwa jamii (CSR) kwa kutoa michango katika sekta za elimu, afya, vijana, maendeleo ya jamii na michezo.
Katika kipindi cha miaka mitano(2020-2024) Shirika limetoa misaada kwa jamii ya TZS Bilion 1.42
Jedwali la Muhtasari wa Michango (Kwa TZS Mamilioni)
| Sekta | 2020 | 2021 | 2022 | 2023 | 2024 |
| Elimu | 50 | 125 | 245.6 | 52.5 | 67.9 |
| Afya | 11 | 14 | 31.5 | 48.7 | 46.1 |
| Vijana | 4 | 6 | 47.6 | 7 | 2.3 |
| Jamii | 75 | 21 | 90.5 | 303 | 124.47 |
| Michezo | – | – | – | 38 | 6.25 |
| Jumla | 140 | 166 | 415.2 | 449.2 | 246.02 |