LIVE: Barca VS AC Milan...Barca akifudhu ntajing'ata mgongoni

LIVE: Barca VS AC Milan...Barca akifudhu ntajing'ata mgongoni

klabu yenye mafanikio na makombe meengi zaidi ya kimataifa hapa nalazimika kuitaja Klabu ya AC Milan yenye maskani yake katika Barabara ya Turati iliyopo Sansiro katika Wilaya ya Milan usiku wa leo inaingia katika uwanja wa Nou Camp kwenda kupambana na Barcelona ambao tayari wako nyuma kwa goli mbili kwa bila.

Numero uno Milan wakiwa kwenye kiwango kizuri wanatarajiwa kuhitimisha safari ya Barca hii leo, kwani kwa matokeo yaliopo sasa yanaonyesha wazi kuwa Barca ashabakwa na leo wanalazimika tu kwenda kukamilisha ratiba.

katika mechi ya mwanzo iliofanyika wiki kadhaa zilizopita Milan waliwasasambua Barca na kuwacharaza goli 2-0 huku Milan ikimkosa siku hiyo mshambuliaji wake mahiri waliemsajili mwezi Januari Super Mario Balotelli ambaye kafunga magoli 6 ktk mechi 6 lakini Barca nao walimkosa mshambuliaji wao Lionel Messi ambaye alicheza lakini akafunikwa bila kuwa na Madhara yoyote.

Makamo mwenyekiti wa AC Milan Adriano Galiani ameweka wazi kuwa hata Barca wakipanga golini makipa wao wote wawili haitawazuia Milan kupata Goli leo.
na kuongeza kuwa ni jukumu la Refa kuwa Fair...hatutegemei maamuzi kuwa mabovu na yenye kuwabeba Barcelona kama yaliyofanyika msimu uliopita.

Milan wamelibeba kombe hili la klabu bingwa barani ulaya mara 7, mara mbili nyuma ya Madrid na wachambuzi wa maswala ya Soka wamewataja kuwa wanao uwezo wa kulibeba msimu huu.

Milan wanaingia uwanjani huku wakimkosa mshambuliaji wao Gianpaolo Pazzo Pazini aliyepata majeraha katika mechi ya ligi walioshinda goli 2-0 ijumaa iliopita.

Its Final Battle between Gutierez VS Gang Chomba.

MY PREDICTION...
Watashindana lakini hawatashinda...
Forza Milan.
Per Sempre Noi
Grande Milan

Messi anapiga hat-trick + 1.

Barca to progress!
 
Messi anapiga hat-trick + 1.

Barca to progress!


Mpaka unaandika hayo ambayo wewe unayaamini huyo Nesi kacheza mechi 11 dhidi ya timu za Italia na kafunga magoli 3 ambayo yooote ni ya penati.

unantafuta nianze kubwabwaja shombo mapema.
Tafadhali naomba ufute hiyo post yako.
 
The True Friend of Truth is TIME...
Wakti muntaradad unazidi kusogea...
 
Gang Chomba unachonishangaza ni kuanza kumtaja refa kabla ya mechi..ni kama unaandaa pa kuegemea!! si tusubiri baada ya game kama refa atakuwa ameuma tutaona! Binafsi naamini kwa uchezaji wa Barca leo game itakuwa ngumu kwenu mnaweza hata kupata red maana mwaweza pigwa vyenga na kugongewa pasi za maudhi na hatari..natabiri Milan kulowa pale Camp Nou leo na Messi kushine!! Wapi Companero

amesahau lile goli la kunawa pale kwao.
 
Last edited by a moderator:
Gang Chomba mzee wa Gaucho...yule mwana wa kujidai na mpira jinsi atakavyo....yule aliyefanya watu wengi waipende La masia....leo unaikataa wazi wazi Barca.....nakuhakikishia Milan leo watautafuta mpira kwa tochi...kila wakiupata itakuwa pale wanapoutoa nyavuni kwenda kuanza pale kati kati.....Barca balaa hata ikiwa na makocha wasaidizi tupu...

Anaondoka na Mkono.
 
Last edited by a moderator:
....Timu yangu Arsenal inajikongoja kesho..... siipendi kabisa Barcelona
 
Mpaka unaandika hayo ambayo wewe unayaamini huyo Nesi kacheza mechi 11 dhidi ya timu za Italia na kafunga magoli 3 ambayo yooote ni ya penati.

unantafuta nianze kubwabwaja shombo mapema.
Tafadhali naomba ufute hiyo post yako.

Mkuu,
With due respect...mpe HESHIMA yake Messi.
 
Leo hatumwi mtoto dukani...ila Barca wana kazi saaaaaaaana kuwatoa millan...maana inabidi wapige goli tatu..unless kama AC milan watakuwa wamelala?
 
hah hah hah hah mkuu naona unaucheza mpira kwa maneno
leo barca wakifungwa na millan natafuna maji

Wacheni maneno mengi yasiyotekelezeka mara mtu atajiuma mgongo hii haiwezekani na we wa kutafuna maji unatuchora tu haitekelezeki hiyo.
 
Back
Top Bottom