LIVE: Barca VS AC Milan...Barca akifudhu ntajing'ata mgongoni

LIVE: Barca VS AC Milan...Barca akifudhu ntajing'ata mgongoni

Gang Chomba

Platinum Member
Joined
Feb 29, 2008
Posts
20,734
Reaction score
4,871
klabu yenye mafanikio na makombe meengi zaidi ya kimataifa hapa nalazimika kuitaja Klabu ya AC Milan yenye maskani yake katika Barabara ya Turati iliyopo Sansiro katika Wilaya ya Milan usiku wa leo inaingia katika uwanja wa Nou Camp kwenda kupambana na Barcelona ambao tayari wako nyuma kwa goli mbili kwa bila.

Numero uno Milan wakiwa kwenye kiwango kizuri wanatarajiwa kuhitimisha safari ya Barca hii leo, kwani kwa matokeo yaliopo sasa yanaonyesha wazi kuwa Barca ashabakwa na leo wanalazimika tu kwenda kukamilisha ratiba.

katika mechi ya mwanzo iliofanyika wiki kadhaa zilizopita Milan waliwasasambua Barca na kuwacharaza goli 2-0 huku Milan ikimkosa siku hiyo mshambuliaji wake mahiri waliemsajili mwezi Januari Super Mario Balotelli ambaye kafunga magoli 6 ktk mechi 6 lakini Barca nao walimkosa mshambuliaji wao Lionel Messi ambaye alicheza lakini akafunikwa bila kuwa na Madhara yoyote.

Makamo mwenyekiti wa AC Milan Adriano Galiani ameweka wazi kuwa hata Barca wakipanga golini makipa wao wote wawili haitawazuia Milan kupata Goli leo.
na kuongeza kuwa ni jukumu la Refa kuwa Fair...hatutegemei maamuzi kuwa mabovu na yenye kuwabeba Barcelona kama yaliyofanyika msimu uliopita.

Milan wamelibeba kombe hili la klabu bingwa barani ulaya mara 7, mara mbili nyuma ya Madrid na wachambuzi wa maswala ya Soka wamewataja kuwa wanao uwezo wa kulibeba msimu huu.

Milan wanaingia uwanjani huku wakimkosa mshambuliaji wao Gianpaolo Pazzo Pazini aliyepata majeraha katika mechi ya ligi walioshinda goli 2-0 ijumaa iliopita.

Its Final Battle between Gutierez VS Gang Chomba.

MY PREDICTION...
Watashindana lakini hawatashinda...
Forza Milan.
Per Sempre Noi
Grande Milan
 
Nipo barca,tunaichukulia poa lakini mpira dakika 90,lolote laweza kutokea
 
Timu bora ya soka ulimwenguni leo inaingia ikiwa na hasira ya kufungwa na timu inyosemekana ni kibonde kuliko zote zilizofuzu raundi hii zaidi ya kujivunia historia,utabiri leo ushindi upo kwa wanacatala ukipenda watoto wa la masia,ila sijui wa ngapingapi,kwahiyo huenda tukapita au kutolewa ila ushindi upo animo Barcelona
 
leo mi ni mtazamaji tu maana najua hapa lolote linaweza kutokea...
 
Nimekusubiri uandike thread tokea asubuhi kwa sababu leo upo uwanjani kwako lakini ukaingia chini ya kibao cha mbuzi na kujificha.

Sasa hivi unajitokeza na kuanza kuleta mikwara yako...hah hah haaaah haya nakuachia jamvi na Nigga hapo mliongoze na kujimwayamwaya.

mie nilitamba Sansiro.
 
Nipo barca,tunaichukulia poa lakini mpira dakika 90,lolote laweza kutokea

Hah hah haaah leo ndio unajuwa mpira Dakika 90?
1st leg we si ulisema Milan lazima wajambe?
Matokeo yake ukapiga mbizi kwenye pipa la lami...
Hah hah hah chezea Buluda wewe!
 
Hata mimi Mdunguaji leo nitashuhudia hiyo mechi nikiwa huku Shimoni, Mombasa.
 
leo mi ni mtazamaji tu maana najua hapa lolote linaweza kutokea...

Ndetichia unamwamini Mungu niamini na mimi.
Barca ashachana yakhe...
Na yakitokea maajabu na wao kufudhu basi ntajing'ata mgongoni.
 
Timu bora ya soka ulimwenguni leo inaingia ikiwa na hasira ya kufungwa na timu inyosemekana ni kibonde kuliko zote zilizofuzu raundi hii zaidi ya kujivunia historia,utabiri leo ushindi upo kwa wanacatala ukipenda watoto wa la masia,ila sijui wa ngapingapi,kwahiyo huenda tukapita au kutolewa ila ushindi upo animo Barcelona

i bet the champions league final will be juve na bayern aka bavarian..
 
Leo Milan anatoka, hata kwa bahati mbaya Milan hawezi kusonga mbele.
 
Hah hah haaah leo ndio unajuwa mpira Dakika 90?
1st leg we si ulisema Milan lazima wajambe?
Matokeo yake ukapiga mbizi kwenye pipa la lami...
Hah hah hah chezea Buluda wewe!
hah hah hah hah mkuu naona unaucheza mpira kwa maneno
leo barca wakifungwa na millan natafuna maji
 
Back
Top Bottom