Tuambie Mechi yako Bora zaidi ya soka ambayo umewahi kuishuhudia

Fohadi

JF-Expert Member
Jul 24, 2020
770
2,408
Nimekuwa shabiki wa soka kwa muda mrefu sana. Kwa muda wa miaka 20 sasa. Nimeangalia mechi nyingi sana na za kutosha, zaidi ya 1000 hadi leo hii.

Toka enzi za goli la dhahabu hadi leo hii ambapo goli la ugenini limefutwa kwenye mashindano ya Ulaya na technolojia ya VAR inatumika.

Nimeangalia fainali 6 za kombe la dunia, toka 2002 hadi 2022. Nimeangalia zaidi ya fainali 14 za Uefa Champions league. Nimeangalia mechi nyingi sana za mashindano tofauti tofauti na zenye matukio ya kusisimua na matokeo ya kustaajabisha....Jaribu kuwaza,,

Nani amesahau kuhusu usiku wa Liverpool dhidi ya Ac Milan 2005?..Je ile comeback ya Barcelona dhidi ya PSG 2017?...vipi kuhusu usiku wa Drogba pale Allianz Arena 2012?....Bila shaka wote tunakumbuka goli la Iniesta lilivyowapa ubingwa Spain mbele ya Uholanzi pale Soccer city kwa madiba....Na vipi kuhusu ile Acrobatic ya Wayne Rooney dhidi ya Man city dakika za kuelekea mwisho kabisa kwenye mechi muhimu ya kuamua bingwa wa EPL 2010/2011...Mungu amlaze pema Cheikh Tiote anayetukumbusha Comeback ya Newcastle dhidi ya Arsenal game ambayo Newcastle wanatoka nyuma kwa bao 4 na kufanya matokeo kuwa 4 kwa 4...vip kuhusu Madrid dhidi ya City UCL mwaka jana?

Hakika kuna mechi nyingi sana ambazo tumezishuhudia na kuzifurahia. Na ambazo zilituacha na kumbukumbu nzuri sana mioyoni mwetu. Lakini pamoja na hayo, kuna mechi moja ambayo kwangu mimi nimeiweka katika kilele cha ubora. Ndiyo, ni Mechi Bora zaidi ya soka ambayo nimewahi kuishuhudia. Unataka kuifahamu?

Usipate tabu, rudisha kumbukumbu zako hadi Jioni ya Tarehe 18.12.2022 pale Qatar...ARGENTINA vs FRANCE....Dakika 120 za dhahabu. Ni mechi kubwa iliyoamuliwa na wachezaji wakubwa katika hatua kubwa ya mshindano makubwa zaidi ya soka duniani.

Kwangu mimi Argentina Vs France ndio mechi yangu bora zaidi ya soka niliyowahi kuishuhudia toka nimeanza kuangalia soka....

Tuambie kwa upande wako, ipi mechi bora kwako!!!
 
Kolo Muani anakosa goli baada ya kubaki na kipa dakika ya 119. Mechi inaisha 3-3 baada ya exra time.

Kwenye mikwaju ya penati, Argentina anabeba ndoo ya Dunia.
Yes, ni bonge la mechi. Na hasa utamu wa mechi hii unanogeshwa na ukweli kwamba mimi ni TEAM MESSI lia lia....shabiki ambaye namkubali messi kama GOAT wa soka...niliangalia ile game nikiwa na presha kuanzia dakika ya 1 hadi ya mwisho. Hata pale Argentina alikuwa akiongoza bao mbili bado niliamini haijaisha hadi iishe....Ile save ya Martinez dhidi ya Kolo Muani ni Mungu tu anayejua.
 
1. Yanga 1 Simba 2 (Msimu wa 2016 au 2017)baada ya Besala Bukungu kula umeme kipindi cha kwanza, Mavugo na Kichuya wanafunga magoli mhimu ya ushindi
2. Bayern vs Chelsea finali Uefa 2012

Hizi zilikuwa mechi tamu sana zenye matokeo ya kusisimua na kuhuzunisha kwa wakati mmoja
 
Nimekuwa shabiki wa soka kwa muda mrefu sana. Kwa muda wa miaka 20 sasa. Nimeangalia mechi nyingi sana na za kutosha, zaidi ya 1000 hadi leo hii.

Toka enzi za goli la dhahabu hadi leo hii ambapo goli la ugenini limefutwa kwenye mashindano ya Ulaya na technolojia ya VAR inatumika.

Nimeangalia fainali 6 za kombe la dunia, toka 2002 hadi 2022. Nimeangalia zaidi ya fainali 14 za Uefa Champions league. Nimeangalia mechi nyingi sana za mashindano tofauti tofauti na zenye matukio ya kusisimua na matokeo ya kustaajabisha....Jaribu kuwaza,,

Nani amesahau kuhusu usiku wa Liverpool dhidi ya Ac Milan 2005?..Je ile comeback ya Barcelona dhidi ya PSG 2017?...vipi kuhusu usiku wa Drogba pale Allianz Arena 2012?....Bila shaka wote tunakumbuka goli la Iniesta lilivyowapa ubingwa Spain mbele ya Uholanzi pale Soccer city kwa madiba....Na vipi kuhusu ile Acrobatic ya Wayne Rooney dhidi ya Man city dakika za kuelekea mwisho kabisa kwenye mechi muhimu ya kuamua bingwa wa EPL 2010/2011...Mungu amlaze pema Cheikh Tiote anayetukumbusha Comeback ya Newcastle dhidi ya Arsenal game ambayo Newcastle wanatoka nyuma kwa bao 4 na kufanya matokeo kuwa 4 kwa 4...vip kuhusu Madrid dhidi ya City UCL mwaka jana?

Hakika kuna mechi nyingi sana ambazo tumezishuhudia na kuzifurahia. Na ambazo zilituacha na kumbukumbu nzuri sana mioyoni mwetu. Lakini pamoja na hayo, kuna mechi moja ambayo kwangu mimi nimeiweka katika kilele cha ubora. Ndiyo, ni Mechi Bora zaidi ya soka ambayo nimewahi kuishuhudia. Unataka kuifahamu?

Usipate tabu, rudisha kumbukumbu zako hadi Jioni ya Tarehe 18.12.2022 pale Qatar...ARGENTINA vs FRANCE....Dakika 120 za dhahabu. Ni mechi kubwa iliyoamuliwa na wachezaji wakubwa katika hatua kubwa ya mshindano makubwa zaidi ya soka duniani.

Kwangu mimi Argentina Vs France ndio mechi yangu bora zaidi ya soka niliyowahi kuishuhudia toka nimeanza kuangalia soka....

Tuambie kwa upande wako, ipi mechi bora kwako!!!
Liverpool vs ac Milan kwangu ilikuwa mechi bora

Ingawa hata France vs Argentina ilikuwa moto
 
Sitausahau usiku ule sitausahau usiku wa Messi sitausahau usiku wa Argentina they deserved it
 
Kwangu binafsi mechi mbili zinabaki kumbukumbu kubwa kwangu;Simba SC vs Mufurila Wanderes,DSM Simba SC inakufa 4-0,uwanja wa Taifa, Marudiano ndani ya Zambia Simba SC 5,Mufurila Wanderes 0(Salute salute George Best &Co),ninashuhudia game pale Arusha nikiwa primary school, Vita FC vs Pan African, computer Sunday Manara analetwa rasmi kwa game hiyo, na anaonyesha why alipewa hiyo nickname;mpira wa sasa huu wa kufundishwa ni shida tupu...Kassim Manara akiweka mpira ndani ya miguu yake hata mkija 5hamchukui ule mpira,.....George Masatu anafuta magoli kwenye msitari....ohoooo Tanzania tulipotea wapi kama nchi?
 
Real Madrid 4 vs atletico Madrid 1 -hii ilikuwa fainali ambapo atletico aliongoza Hadi dk ya 94.

Madrid wakapata kona, aisee Sergio Ramos ni zaidi ya fundi, cr7 akaimaliza mechi.
Naikumbuka vyema Diego Semeone alipoona imefika dakika ya tisini anawaapigia kelel mashabiki washangilie akijue mechi imeisha, ikatokea kona ambayo hatakaa aisahau maisha yake yote. Mabeki wakamkaba CR7 wakaishia kulizwa na Ramos. Extra time Marcelo, Bale na CR7 wakapigilia misumari hadi Semeone alipanic ile mechi akaleta fujo
 
mechi ambayo kwangu ilikuwa bora ilikuwa ni ya uholanzi vs spain ilikuwa ni mechi ya makundi ambapo spain anaishia kutolewa makundi na uholanzi 2014 nchini Brazil,,
ile mechi huwa naikumbuka kwa sababu ilikuwa ni mechi ya kisasi kwa uholanzi baada kufungwa fainali ya 2010,,
goal la Argen Robben ambalo alimfanya casilass atambae kama mbwa hua nalirudia mpaka leo YouTube,,ile mechi uholanzi waliingia wameweka sura ya mnyama walikua na hasira sana,, hakika ilikuwa ni mechi ya kupania,,

nyingine: Bayern munich vs Chelsea UEFA fainal 2012
 
M
Real Madrid 4 vs atletico Madrid 1 -hii ilikuwa fainali ambapo atletico aliongoza Hadi dk ya 94.

Madrid wakapata kona, aisee Sergio Ramos ni zaidi ya fundi, cr7 akaimaliza mechi.
Hii mechi pepe aligombana na Simeone, maana atletico walihisi game imeisha
I nadhani aliyeimaliza hii game ni Di maria....kipindi game iko 1 bila....Atletico walikuwa wanaupiga mwingi sana. Baada ya kusawazishiwa, wakahisi kama wameonewa so wakapanic....extra time wakajikuta wanakula goals nne....Di Maria akiiua game
 
Kwangu binafsi mechi mbili zinabaki kumbukumbu kubwa kwangu;Simba SC vs Mufurila Wanderes,DSM Simba SC inakufa 4-0,uwanja wa Taifa, Marudiano ndani ya Zambia Simba SC 5,Mufurila Wanderes 0(Salute salute George Best &Co),ninashuhudia game pale Arusha nikiwa primary school, Vita FC vs Pan African, computer Sunday Manara analetwa rasmi kwa game hiyo, na anaonyesha why alipewa hiyo nickname;mpira wa sasa huu wa kufundishwa ni shida tupu...Kassim Manara akiweka mpira ndani ya miguu yake hata mkija 5hamchukui ule mpira,.....George Masatu anafuta magoli kwenye msitari....ohoooo Tanzania tulipotea wapi kama nchi?
Mkuu....hizi games unazozielezea kwangu mimi ni historia....sikuwepo kipindi hicho. Ila natamani sana nielewe kuhusu Sunday Manara na kwanini aliitwa Computer....Nipe japo ufafanuzi kidogo
 
International level : Argentina Vs France, 2022 worpd cup final.

Club level: Bayern Munich Vs Atletico Madrid 2016 UEFA nusu fainali ya pili pale Allianz Arena, baada ya mechi ya kwanza kuisha kwa ushindi wa moja bila kwa Atletico. Wakarudiana pale Allianz Arena, Pep Guardiola akaweka pembbeni mpira wa kihispaniola, akawaacha akina Frank Ribery wapige ule msako wa kijerumani.

Upande wa pili, Diego Simeone alienda na mission moja tu, kupaki bus. Hili ndicho kipindi ambacho Atletico Madrid walikua na defense bora zaidi duniani.

Ulipigwa mpira mwingi sana. Ilikua ni pressure kuanzia dakika ya kwanza, hadi ya mwisho. Bayern walishinda 2-1, ila wakatolewa kwa aggregate.

NB: Comeback ya Barcelona Vs PSG, ilikua ni total domination. Barca iliwazidia PSG kila kitu, ndio maana siioni kama ni mechi bora.
 
Back
Top Bottom