List ya Waliomwagwa Uwaziri+Unaibu

List ya Waliomwagwa Uwaziri+Unaibu

Watu wengi sana mmetoa dukuduku lenu kuhusu baraza hili. Asilimia kubwa ya wadau hapa hawajaridhika na uteuzi wa baadhi ya mawaziri na manaibu. Sasa tatizo la msingi sio uteuzi bali na fursa iliyotolewa kikatiba kwamba mawaziri watateuliwa na mtu mmoja ambae ni Rais. Kwa hali ya sasa hivi wewe au mimi hatuwezi kubadili chochote lakini tuna jukumu la kuhakikisha kwenye katiba mpya tunayoitarajia kosa hili halijirudii. Kwa iyo ndugu mwanaJF usipige tu politiki hapa jamvini, hakikisha unatumia fursa yako ya kutoa mawazo yako ya msingi katika katiba iweje ikiwa ni pamoja na kuondoa mamlaka makubwa kama haya kwa mtu mmoja!
Tafakari chukua hatua!

Umenena mkubwa
 
Mie nashindwa kumwelewa JK sijui ni mtoto, mwoga au vipi??

Mwandosya anaumwa, angemwacha tu... ajiuguze kwanza, kama ni kwa ajili ya kumsaidia akiumwa ingekuwa akiwa nje

ya uwaziri.

Sijui jk anafanyaje kazi!!! jamani raisi huyu!!! basi angetueleza kwanini mtu ambaye ni mbojwa kampa kazi ya nanmna

ile??

Sio mara ya kwanza kuwapa watu vyeo wakiwa wagonjwa,sasa sijui huwa ana sababu gani za kumpelekea kufanya hivyo. Nakumbuka wakati Kulwa Massaba anaumwa hoiiii akapewa ujaji,maskini mzee wa watu akaenda Ikulu kwenye wheel chair yake akaapishwa,haikufika hata miezi 4 akafariki,haya Mwendwa nae ndio hiyo.......naona iliyobaki tuwaombee tu hawa wagonjwa wapone ili waweze kutumikia vyeo vyao.
 
Plate namba ya gari lake (lazima litakuwa jipya) itasomeka W AW (Waziri Asiye na Wizara)! Sijui jengo la wizara yake litakuwa wapi na wizara sijui itakuwa na watumishi wangapi. Sanaa bana!
Nadhani anatakiwa akae eneo la wazii, kaa uwanja wa Uhuru vile woote tumwone, teh teh.
 
By Paulo
Kilichofanyika baraza la mawaziri ni kubadili mvinyo katika chupa ya zamani na kuweka katika chupa mpya ladha inabaki kuwa ile ile.Serikali ibadili mfumo.
 
nyota ya Nundu imezimika kwa kasi ya ajabu,huyu mzee ukisoma cv yake utaogopa sijui pepo hili limemtokea wapi,Tanga mnagundu kweli.Mtoa msomi mwenye CV International,ameishia kwenye fedhea ya ubadhirifu.Arudi ulaya sasa,hehehehehehe JK nomaame mTIDO kudadeki.

Mimi Eng. Nundu kanisikitisha sana, nadhani atakua anajililahumu kwa nini alirundi nchini - kama wengine walio rudi nchini wakiweka mbele uzalendo; wakati wengeweza kukaa nje na kufanya kazi kwa heshima bila fitina,majungu na kugombania vyeo. Mh. Nundu nakushauri inuka jipanguse life goes on, wewe umewahi kuishi nje, je, uliwahi kushudia mambo ya ajabu kama haya kwa wenzetu, sasa kwa nini Watanzania tushangae kuona miaka takribani hamsini na ushee tangu tupate uhuru bado tanabaki kuwa omba omba wakati nchi kama: Korea ya kusini, Malaysia, Thailand zinapeta kwa nyanja za sayansi na tekinolojia wakati nao walipata uhuru karibu muda hule hule i.e 1960s.

JK anapashwa kufumua mfumo wa uwajibikaji katika Serikali yake the soonest, nakuhakikishia akichelea kufanya mabadiriko ataishia kubadilisha mawaziri wake kila mwaka, mbona enzi za Mh. Mkapa ilikuwa ni nadra sana kufanya mabadiriko kila mara. Mh. Raisi watendaji wakuu wa wizara na wakurugenzi wake ndiyo tatizo kubwa! Usipo wabadilisha watawawekea vikwazo mawaziri uliyo wateua sasa hivi, wata wakwamisha Mh.JK usipo lishughulikia hili. Mimi nashangaa kwa nini washauri wako walishindwa kukueleza kwamba ungetanguliza kwanza kuwaondoa watendaji wakuu na wakurugenzi kwenye wizara zinazo fanya madudu kila kuchwao hili Mawaziri watakao teuliwa wasiwakute walasimu hawa wasio kuwa na uzalendo hata kidogo, wanajali maslia yao TU!

Wizara ya Kilimo, Utalii na Mali Asili, Miundo mbinu, Nishati na Madini ndizo wizara zilizo bobea katika ulasimu, kufanya kazi kwa mazoea na watendaji wakuu kujifanya Miungu watu, wanafanya watakalo na kutegeana - mimi nimewahi kushuhudia kwa macho yangu kwenye Wizara ya Kilimo na Miundo Mbinu - kama wizara zote ziko hivyo naona Mh. Raisi una kazi ya ziada - panatisha sana.
 
Wadau ebu tutajieni list ya waliomwagwa Unaibu na Uwaziri.

Naanza na
1.Ngeleja
2.Maige
3.Nundu
4.Chami
5....
6...
7.Mkulo

Huyo namba 1, alikuwa anabebwa kwa sababu gani? Maana amafanya mabaya mengi sana. Nafikiri aliwaambukiza wenzake. Rushwa mpaka katika budget.
 
waziri bila wizara maalum hii ndio Tanzania bwana , watu wanagawiana vyeo na kujazana maofisini hata kama hawana umuhimu wowote!

waziri siyekua na wizara maalum hana ofisi wala wafanyakazi, wasaidizi hiki ni cheo kuingia kwenye cabinet meeting kutoa mawazo yako na kusaidia kumshauri rais..Jk kamuonea huruma Prof kwa afya yake wizara full asingeiweza so ameona aendelee kumpa perks za uwaziri ikiwemo na kutibiwa nje..sioni ubaya hapa
 
William Malecela ameteuliwa wapi?

Na kujipendekeza kote ****** kamtosa LE Baharia, kampa shavu mwenzie walioshindwa wote kugombea ubunge wa Afrika Mashariki Janet Mbene ambae sasa amekuwa waziri mdogo wa fedha!!!
 
Orodha nzima ya mawaziri na manaibu waziri waliotemwa iwekwe hapa pamoja na makosa yao ili tujadili adhabu wanazostahili. Hili likifanyika litasaidia kutuelewesha na kuwapa nguvu mawaziri wapya
 
Kwa kuwa pinda hajajiuzulu, ile hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu bungeni itaendelea?
 
Jamaa nilijua ni mchapakazi kweli maana kila akienda kukagua shule lazima haikatae kumbe ni fisadi tu kelele nyingi kwenye TV kumbe ufanyaji kazi zero.

Tuwe makini wakuu. Mwanri yupo kwenye kiti chake kilekile pale TAMISEMI
 
Mimi Eng. Nundu kanisikitisha sana, nadhani atakua anajililahumu kwa nini alirundi nchini - kama wengine walio rudi nchini wakiweka mbele uzalendo; wakati wengeweza kukaa nje na kufanya kazi kwa heshima bila fitina,majungu na kugombania vyeo. Mh. Nundu nakushauri inuka jipanguse life goes on, wewe umewahi kuishi nje, je, uliwahi kushudia mambo ya ajabu kama haya kwa wenzetu, sasa kwa nini Watanzania tushangae kuona miaka takribani hamsini na ushee tangu tupate uhuru bado tanabaki kuwa omba omba wakati nchi kama: Korea ya kusini, Malaysia, Thailand zinapeta kwa nyanja za sayansi na tekinolojia wakati nao walipata uhuru karibu muda hule hule i.e 1960s.

JK anapashwa kufumua mfumo wa uwajibikaji katika Serikali yake the soonest, nakuhakikishia akichelea kufanya mabadiriko ataishia kubadilisha mawaziri wake kila mwaka, mbona enzi za Mh. Mkapa ilikuwa ni nadra sana kufanya mabadiriko kila mara. Mh. Raisi watendaji wakuu wa wizara na wakurugenzi wake ndiyo tatizo kubwa! Usipo wabadilisha watawawekea vikwazo mawaziri uliyo wateua sasa hivi, wata wakwamisha Mh.JK usipo lishughulikia hili. Mimi nashangaa kwa nini washauri wako walishindwa kukueleza kwamba ungetanguliza kwanza kuwaondoa watendaji wakuu na wakurugenzi kwenye wizara zinazo fanya madudu kila kuchwao hili Mawaziri watakao teuliwa wasiwakute walasimu hawa wasio kuwa na uzalendo hata kidogo, wanajali maslia yao TU!

Wizara ya Kilimo, Utalii na Mali Asili, Miundo mbinu, Nishati na Madini ndizo wizara zilizo bobea katika ulasimu, kufanya kazi kwa mazoea na watendaji wakuu kujifanya Miungu watu, wanafanya watakalo na kutegeana - mimi nimewahi kushuhudia kwa macho yangu kwenye Wizara ya Kilimo na Miundo Mbinu - kama wizara zote ziko hivyo naona Mh. Raisi una kazi ya ziada - panatisha sana.

nionavyo mm tatizo ni katiba mbovu hata kama wakiletwa watu toka wapi au wakibadilishwa vipi ugonjwa ni ule ule rais ana majukumu mengi san
 
Prof. Mwandosya. Kutokuwa na wizara maalum ni sawa na kupigwa nje.
Huyu ndo boss wa mawaziri wote, ukichelewa kazini utamkuta kakalia kiti chako ! Yeye hachaguwi wizara, yeye
ni maalum kudhibiti mawaziri wazembe !
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom