List ya Waliomwagwa Uwaziri+Unaibu

Mbona hamuongelei ulinzi na usalama na mambo ya ndani zinahusu au mahsusi kwa wazanzibari tu?
 
aisee chingereza bana kina kona nyingi.

cock
Noun:A male bird, esp. a rooster.
Noun:A small pile of hay, straw, or other material, with vertical sides and a rounded top.
Verb:Tilt (something) in a particular direction.

Kilengesa ni kipana hakina maana moja nadhani yeye anaijua ile ya kimarekani tu.
 
Ndo tatizo lenu kukurupukia mambo, jamaa yupo pale pale.

Mkuu usije ukawa wewe ndio umekurupuka? Rejea zitto alivyomwambia kwamba bunge lililopita kwenye hansard aliyasema yaleyale aliyoyasema bunge hili so maneno ni mengi kwa huyo mh mwamri lkn utekelezaji hamna.
 
kwahiyo akiwa anaenda ofisini atakuwa anaripoti ofisi gani? au leo huku kesho kule kila siku atakuwa anahama wizara?

yap, hiyo ndo maana ya kutokuwa na wizara maalum, kotekote anatwanga. teh he he
 
  1. Aliyekuwa Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo
  2. Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja
  3. Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige
  4. Aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi, Omary Nundu
  5. Aliyekuwa Waziri wa Afya, Dkt. Hadji Mponda
  6. Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami

Fagio la chuma limewapitia.
 
Omary Nundu maskini wa watu JK alimchukua nje akaacha project zake za maana, leo kabwagwa..alijitahidi kuonyesha kuwa tatizo ni naibu wake JK amefumba macho kampiga teke....ha ha ha ha ha...
 
Jk hanatulia,maana hata alipokuwa anatangaza baraza jipya la wala (keki)hakuwa anajiamini kabisa.NAHISI LAANA YA WTZ IMEANZA KUMTAFUNA.
 
Plate namba ya gari lake (lazima litakuwa jipya) itasomeka W AW (Waziri Asiye na Wizara)! Sijui jengo la wizara yake litakuwa wapi na wizara sijui itakuwa na watumishi wangapi. Sanaa bana!

Mkuu hii ya waziri kutokuwa na wizara maalum nadhani hii iko Tanzania peke yake,yani pamoja na watu kupiga makelele serikari ipunguze matumizi bado tunakuwa na waziri asiye kuwa na kazi duh...
 
Wamemfanyia heshima afe akiwa waziri azikwe kwa heshima za kiwaziri manake ni marathi ndo yamemkwaza ila ni mchhapa kazi mara mia angemtupa wizara ya afya akasaidia kule huku anatibiwa

acha kutabilia kifo binadamu mwenzio,
Uckute ukatangulia ww
 
hakuna hatua maana kwa maelezo ya mheshimiwa kasema kuwa wamewajibika kisiasa

Ndo kulindana na hakuna mtoto wa kigogo/ rafiki kuumizwa ndo maana watoto wa vigogo lazima waendelee kuwepo katika utawala kwani nyie baba zetu walisaidiaje nchi hii kupata uhuru?
kama baba hajulikani usitegemee wewe kuwepo ndani ya utawala na je wewe umewahi kukaa walau karibu na nyumba nyeupe au kufanya kazi nyumba nyeupe? Je nyumba yenu imewahi kulindwa na wenye kuruhusiwa kuua?
Kama jibu NDIO utakupwepo katika utawala wa nchi hii maana watoto hao wanabusara kuliko wasiowahi kufanya kazi nyumba nyeupe jimbo la uchaguzi lote! na Kama hapana basi jua kama mtoto wa kigogo mmoja ni bora kuliko watu waliosoma wote katika nyanja zote za jimbo la uchaguzi lote basi maisha yako yote utakaa tu kusubiri taarifa toka vyombo vya habari na hutakaa na wala kufikiria kuingia nyumba nyeupe kwa kuitwa na mwenye nchi.
 
bado najiuliza inakuwaje mponda na nkya wakachinjiwa baharini lakini kwenye wizara ya nishati na madini akaumia ngeleja lakini malima akapona? hmmm...!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom