Lissu: Si mara ya kwanza tunaahidiwa kuwekewa mikataba wazi. Kumuunga mkono Rais si lazima

Hivi nyie viongozi wetu kuchambana mtamaliza lini..?? Kila kukicha vichwani mwenu mnawaza " Nimjibuje Lissu, Nimjibuje Magu, Nimjibuje Polepole..,, Hayo maendeleo ya nchi yetu mnayawaza masaa mangapi kwa siku..?? Punguzeni kunyoosheana vidole na kuchambana ifike muda mfikirie mbinu za kututoa kwenye huu umaskini jamani...!!


Khaa..!! Watu tutakufa tufufuke bado Tanzania iko hapahapa mmekazania Kuchambuana washenzi nyie., Tumewaamini aminikeni bhasi na nyie, Tukisema kila mmoja aone mabaya atake kuchukua nchi Patatosha kweli...??
Sasa kama wanaleta mipasho waachwe hivi hivi haiwezakaniki, tena wanatumia vitisho.
 
Ifike mahali mfanye mambo kwa uzalendo na maelewano. Hii kupayuka kila siku inakuwa sawa na the boy who cried wolf. Inachosha!

TLS huu ndiyo wakati wa kuonyesha who they are kwa kuweka mwongozo wa kitaalamu kisheria kuhusu sakata hili. Hata usipofuatwa ni sawa lakini hii kupayuka kila leo hii dah!
 
Lissu Take Care , unapotaka kuelekea ni kujipotezea Heshima yako ulioijenga kwa Nguvu kubwa na kwa mda mrefu pia.

Unajaribu kupinga kitu ambacho hata hujui unakioinga kwa namna gani.
Acha kua chambo kwenye kila kitu.
 
Lissu huwenda unahoji vyema , sema.una haraka mno. Mambo yote uliyoyahoji ni mapendekezo ya sasa ya Rais kuokoa Jahaza jili lililotoboka , ila umejaribu kuyahoji kimmhemuko sana na kwa speed ya hali ya juu.Kila jambo litatendekea kwa utaratibu wake, sidhani kama hayo yote uliyojaribu kuyahoji yangeweza kufanyika leo.

2. Unapose kipindi fulani mlihoji kuhusu mikataba mkapuuzwa , je mngependelea kuendelea kupuuzwa ? Au ni ipi Logic ya kile unachotaka kukihoji.
Tatizo sisonje analeta siasa uchwala za kuchafuana na uongo, sasa hakuna mtu atakayekubali, hivi angewasilisha bila kuchafuana mbona isingekuwa tatizo
 
mmh! Namwelewa Tundu Lisu lakini hatoi mapendekezo. Hapo ndipo nguvu ya upinzani inapokosekana. Lisu na wenzake wanapaswa kuja na mapendekezo mbadala kama hayo aliyoagiza Mkuu wetu yana kasoro na siyo maneno tu kama hivi.
Kuna haja gani ya kutoa mapendekezo ambayo hayafuatwi? For 19 years wametoa mapendekezo na yanabezwa hadi leo ndio wanagundua kuwa walikosea kutoyafuata?
 
mmh! Namwelewa Tundu Lisu lakini hatoi mapendekezo. Hapo ndipo nguvu ya upinzani inapokosekana. Lisu na wenzake wanapaswa kuja na mapendekezo mbadala kama hayo aliyoagiza Mkuu wetu yana kasoro na siyo maneno tu kama hivi.
Mapendekezo yapo mengi sana, lakini tatizo kwenye uchambuaji mapendekezo yao yatatupiliwa mbali na wao pia kuswekwa nje kisa akisimamia ukweli anaambiwa ameroporoka.
 
Ninachosoma ni hoja zilizojaa jazba na masuala ambayo kwa sasa ni dead letter.

Naona Lissu anakomaa eti serikali ikajiondoe kwenye MIGA na BITs ili mipango ya uwekezaji nchini isifanikiwe. Serikali imesema haijiondoi kwenye MIGA na BITs kwa sababu ya kampuni moja.

Hii dhana ya kusema ''mimi nilipigania sana hizi sheria zifutwe'' ni unafiki fulani kwa maslahi na mtaji wa kisiasa.

Kwa hiyo kama alipigania ndio wengine wasipiganie?
Kadri siku zinavyoonda maneno "mnafiki" na "msaliti" yanakosa maana au watumiaji hawajui maana yake!
 
Everything has its limit iron ore cannot be educated into gold.

Please TL muache Sizonje hana uwezo wa kuchanganua mambo kama haya kwa sasa anatafuta huruma tu ili tusahau kua aligonga meza kwa shangwe wakati anapitisha sheria kandamizi kwa rasilimali zetu.
 
Mm nimeshangaa tu pale kelele za wezi..wezi...wezi zilivyopigwa na Mwenyekiti wa kamati...mpaka na kwenye mapendekezo nikasikia Acacia wachukuliwe hatua za kisheria kwa kituibia.

Mwenye kamati naye aliposimama akaimba wezi...wezi....wezi na akakubaliana na mapendekezo yote ya kamati ila alipohitimisha akasema tukae tena na wezi kwenye majadiliano tuone ni jinsi gani wanatulipa hela yetu waliyotuibia...hapo ndipo nilichoka na kuchoka Kabisa.

Tutaomba mrejesho wa mazungumzo kati ya wezi na maafisa wa serikalini kama hayo mazungumzo yatafanyika lakini isije ikawa ni danganya toto tu ya kutafuta sifa mbele ya viongozi wa dini.
 
Back
Top Bottom