Lissu: Si mara ya kwanza tunaahidiwa kuwekewa mikataba wazi. Kumuunga mkono Rais si lazima... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lissu: Si mara ya kwanza tunaahidiwa kuwekewa mikataba wazi. Kumuunga mkono Rais si lazima...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tundu Lissu, Jun 13, 2017.

 1. T

  Tundu Lissu Verified User

  #1
  Jun 13, 2017
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 9
  Likes Received: 310
  Trophy Points: 3
  For the Record: What Goes Around Comes Around!!!

  Leo wapinzani wa Serikali ya Magufuli tumesemwa sana na kutishiwa kushughulikiwa bungeni na nje ya Bunge.

  Kwa sababu hiyo, naomba niweke rekodi ya masuala haya sawa sawa.

  Mwezi Machi '97 Bunge lilipitisha Sheria 2 kwa siku moja kwa kutumia Hati ya Dharura.

  1) Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbali mbali za Fedha ya '97 ilifuta au kupunguza kodi nyingi kwa ajili ya makampuni ya kigeni ya madini.

  2) Sheria ya Uwekezaji Tanzania '97 iliwapa wawekezaji wa kigeni ulinzi mkubwa na manufaa mengi kama vile kuondosha nje fedha na faida yote wanayopata kwa uwekezaji wao nchini.

  Mwaka '98 Bunge lilipitisha Sheria ya Madini '98 ambayo ilitamka kwamba mwenye milki ya madini na fedha yote itokanayo na mauzo ya madini ni mwenye leseni ya kuchimba madini hayo.

  Sheria hizo tatu nimeziita 'Utatu Usio Mtakatifu' (Unholy Trinity) katika maandiko yangu mbali mbali, na nimezichambua sana tangu mwaka '99 nilipoanza harakati dhidi ya sekta ya madini ya aina hii.

  Kwa miaka yote hii hadi leo, Sheria hizi za madini zimeungwa mkono na kupigiwa debe na kila kiongozi na mbunge wa CCM, Magufuli included.

  Watu hawa, with very few and minor exceptions, ndio wamekuwa washangiliaji wakubwa wa unyonyaji wa makampuni ya kigeni ya madini katika nchi yetu.

  Na ukweli ni kwamba watu hawa na Chama chao ndio wamefaidika sana na utaratibu huu katika sekta ya madini.

  Wachache tuliopinga utaratibu huu tuliitwa kila aina ya majina mabaya na uzalendo wetu ulihojiwa kama unavyohojiwa leo na Magufuli.

  Kwa mfano, Rais Mkapa alidai, wakati anazindua Mgodi wa Bulyanhulu, kwamba upinzani wetu ulikuwa ni 'ujinga uliofichama katika kivuli cha taaluma.'

  Baadhi yetu, kama mimi na Dr. Rugemeleza Nshala, tulikamatwa na kushitakiwa mahakamani kwa uchochezi. Tulikabiliwa na kesi hiyo kuanzia Mei '01 hadi '08 ilipofutwa kwa kukosekana ushahidi.

  Kama ilivyokuwa wakati wa Mkapa mwaka '01, leo pia Rais Magufuli ametukebehi na kuahidi kutushughulikia 'tukiropoka' nje ya Bunge.

  Tunaambiwa ni lazima tumuunge mkono Rais wetu katika hii 'vita ya uchumi.' Ni sheria ipi ya Tanzania inayotulazimu kumuunga mkono Rais wetu hata kama tunaona amekosea???

  Hebu naomba tuitafakari hii 'vita ya uchumi' kidogo. Je, nani hasa ni maadui zetu katika 'vita' hii??? Ni makampuni ya madini ya kigeni??? Kama ni hivyo, fikiria yafuatayo:

  1) Wakati tuko vitani, Rais Magufuli na serikali yake wameiruhusu Acacia Mining (tunayoambiwa hata haijasajiliwa!!!) kuendelea kuchimba, kusafisha na kusafirisha nje ya nchi dhahabu kutoka Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara Tarime.

  Amezuia magwangala yasisafirishwe nje kwenye makontena lakini dhahabu yenyewe hamna shida ikisafirishwa na wezi hawa!!!!!

  2) Wakati mapambano ya 'vita ya uchumi' yakiendelea, dhahabu yote inayochimbwa Geita Gold Mine (Mgodi mkubwa kuliko yote nchini) inaendelea kuchimbwa, kusafishwa na kusafirishwa nje ya nchi.

  3) Wakati tuko vitani, Rais Magufuli na serikali yake ameruhusu kila mgodi wa dhahabu nchini kuwa na kiwanja chake binafsi cha ndege ili wezi hawa waweze kutorosha 'dhahabu yetu' kwa urahisi zaidi.

  4) Wakati tungali vitani, 'Utatu Usio Mtakatifu' wa sheria zetu za kodi, uwekezaji na madini uko pale pale ulipokuwa mwaka '97-'98, cosmetic changes excepted.

  Aidha, licha ya kuwa vitani, sisi bado ni signatories wa MIGA Convention na bilateral investment treaties (BITs) zinazowalinda hawa tunaoaminishwa kuwa ni wezi na maswahiba wao wa miaka yote.

  5) Wakati tuko kwenye hii vita kubwa ya uchumi, jemedari wetu mkuu na serikali yake hawajatengua mkataba hata mmoja wa uendelezaji madini (Mineral Development Agreements - MDAs) walizosaini hawa anaowaita wanyonyaji na serikali za watangulizi wake Jakaya Kikwete na Ben Mkapa.

  6) Wakati tunahamasishwa kumuunga mkono jemedari huyu shupavu, bado hatujaonyeshwa mkataba hata mmoja waliosaini na wanyonyaji hawa tangu miaka ya mwanzo ya '90.

  Leo Jemedari Mkuu ameahidi kwamba mikataba hiyo italetwa bungeni. Safi sana.

  Lakini je, hii ni mara ya kwanza tunaahidiwa hayo???

  Mwaka '08 Jemedari Mkuu wa kabla yake alituahidi hivyo hivyo. Tuwe na subira kabla ya kuanza kushangilia prematurely.

  7) Nimemsikia Magufuli akielekeza wahusika wote wa uchafu huu washughulikiwe. Kweli???

  (a) Je, Jakaya Kikwete aliyesaini leseni za Bulyanhulu na Nzega mwaka '94 anaponaje???

  (b) Je, Ben Mkapa aliyekuwa Rais na Mwenyekiti wa Cabinet wakati haya yanafanyika anaachwaje???

  (c) Je, waliokuwa mawaziri na manaibu wao wote wakati haya yanatokea wanasalimikaje???

  (d) Je, wale washangiliaji na wapiga meza wa bungeni, ambao waliunga mkono kila walicholetewa bungeni na kukipitisha kilivyo wanakosaje lawama???

  8) Nimesikia Acacia Mining hawana hata leseni/usajili wa kuendeshea shughuli zao hapa nchini. Labda. Hata hivyo, jiulize yafuatayo:

  (a) Hivi wamekuwa wanalipa kodi kama PAYE, SDL, income tax, withholding tax, mrahaba, n.k., kwa kutumia jina gani miaka yote hii???

  (b) Je, wana akaunti yoyote katika benki za Tanzania??? Kama ndio, wamezifungua kwa jina gani???

  Kama hapana, wanalipaje mishahara ya wafanyakazi wao wa Kitanzania au watoa huduma mbali mbali wa Kitanzania???

  (c) Je, wanalipa bili za umeme kwa TANESCO au za simu kwa Vodacom, Tigo, Airtel, n.k. kwa kutumia jina gani???

  (d) Je, wamesajiliwaje katika Soko la Hisa la Dar kama Acacia kama wanaendesha shughuli zao kihuni hivi???

  (e) Kuna kitu kinaitwa 'estoppel' katika Sheria yetu ya Mikataba (the Law of Contract Act, Cap. 345) na katika Sheria yetu ya Ushahidi (the Law of Evidence, Cap. 6).

  Je, estoppel haituhusu kwenye suala hili la leseni au usajili ya Acacia???

  Kama estoppel inahusika, je, hoja hii ya ukosefu wa usajili ina uzito gani, kama upo, kisheria???

  9) Nimesikia Sheria za Madini zinatakiwa kufanyiwa marekebisho makubwa. Sawa kabisa.

  Lakini je, kwanini Rais Magufuli hajasema chochote juu ya Sheria za Gesi Asilia na Mafuta ambazo zilipitishwa haraka haraka kwa Hati ya Dharura baada ya sisi 'waropokaji' kutimuliwa bungeni na Spika Anna Makinda mwaka '15???

  Au Rais wetu anaamini kwamba Sheria za Gesi Asilia na Mafuta hazina matatizo licha ya kupitishwa kwa utaratibu ule ule uliotumika kwa Sheria za Madini???

  10) Wakati tunaingojea kwa hamu mikataba ya madini iletwe bungeni, hebu na tujiulize yafuatayo:

  (a) Mikataba ya uchimbaji gesi asilia na mafuta nayo iko wapi???

  (b) Mikataba ya manunuzi ya Bombardier na Dreamliner za Magufuli nayo italetwa bungeni au itabidi tusubiri aondoke madarakani kwanza kama ilivyokuwa kwa JK na BM???

  (c) Mikataba ya ujenzi wa airport Chato na Reli ya Standard Geji ya Waturuki au Wachina na mabarabara kibao nayo italetwa bungeni au ndio basi tena tusubiri Bwana mkubwa atakapoondoka madarakani???

  Wakati tukisubiri kufukuzwa bungeni na Spika Ndugai kwa maelekezo ya bosi wake, na wakati tukisubiri dhahama ya Bwana Mkubwa nje ya Bunge, hebu na tujiulize hivi nani hasa ndiye mzalendo wa kweli wa nchi hii???

  Hebu na atutajie majina na namba za simu za wale wote ambao amedai wamekuwa wanawasiliana na Acacia na lini walifanya mawasiliano hayo na yalihusu kitu gani. Kutoa hukumu kwa innuendo peke yake haitoshi, tunahitaji ushahidi thabiti kutoka kwa Rais Magufuli.

  Sijazungumzia bado plagiarism ya taarifa mbali mbali za kiserikali na zisizo za kiserikali katika Taarifa ya Kamati ya Prof. Osoro. Hili ni la baadae.
   
 2. marcus rojo

  marcus rojo JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2017
  Joined: Mar 19, 2017
  Messages: 1,499
  Likes Received: 5,211
  Trophy Points: 280
  Nitasoma asubuhi hizi saint anne zishapanda kwenye medulla
   
 3. KikulachoChako

  KikulachoChako JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2017
  Joined: Jul 21, 2013
  Messages: 14,768
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280
  Lissu ni mwanasheria msomi lakini sifa na majivuno vinamfanya akose breki.....

  Ni mtazamo tu....
   
 4. sizonjemadawa

  sizonjemadawa JF-Expert Member

  #4
  Jun 13, 2017
  Joined: Feb 11, 2017
  Messages: 1,068
  Likes Received: 1,268
  Trophy Points: 280
  Greeting

  Tumezoea Kuona maneno ya viongozi wakubwa wa nchi yanavyoishi mfano mwl Julius Nyerere maneno yake yanaishi hadi Leo, ukisikiliza maongezi yake ya miaka ya nYuma utafikili alikuwa anaona leo itakuwaje,

  Si jambo jepesi ni watu wachache wanaweza ila kwa sasa ni Tundu lisu Maneno ya Tundu lisu yanaishi, anachokiongea Banda ya miezi/miaka kadhaa kuna jambo linalofanana na maneno yake linatokea

  #hongera Tundu Lissu Mungu akulinde#
   
 5. Deejay nasmile

  Deejay nasmile JF-Expert Member

  #5
  Jun 13, 2017
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,949
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Duuuh
   
 6. marcus rojo

  marcus rojo JF-Expert Member

  #6
  Jun 13, 2017
  Joined: Mar 19, 2017
  Messages: 1,499
  Likes Received: 5,211
  Trophy Points: 280
  Imebidi nisome tu, wewe lissu utatuulia huyu mtu give him a break!
   
 7. MsemajiUkweli

  MsemajiUkweli JF-Expert Member

  #7
  Jun 13, 2017
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 9,804
  Likes Received: 14,277
  Trophy Points: 280
  The pillock is walking on sound bites!

  Ninachosoma ni hoja zilizojaa jazba , kejeli na masuala ambayo kwa sasa ni dead letter.

  Mkubali tu kuwa ajenda ya uzalendo mliuza siku ambayo mlimpokea yule mlituambia ni fisadi papa na genge lake.

  Mzalendo gani anayetuambia kwa miaka minane kuwa fulani ni fisadi na anashangaa kwa nini anapewa fomu za kugombea Urais halafu baada ya huyo fisadi kukatwa, yeye ndie anamchukua na kumfanya mgombea Uraia.

  Pesa zikiwekwa mezani uzalendo wake unakuwa historia.

  Mzalendo Lissu wa sasa hawezi hata kudiriki kuwataja mawaziri wakuu waliokuwepo wakati wa utawala wa marais Mkapa na Kikwete. Chezea pesa wewe!

  Naona Lissu anakomaa eti serikali ikajiondoe kwenye MIGA na BITs. Huu ni ushauri wa kijinga. Unataka mipango ya uwekezaji/wawekezaji nchini isifanikiwe. Serikali imesema haijiondoi kwenye MIGA na BITs kwa sababu ya kampuni moja.

  Suala la ushauri wake kuhusu MIGA and BITs niliwahi kulielezea hapa;

  GONGA LINK>>Ushauri wa Tundu Lissu kwa serikali niwa kijinga na serikali itakuwa ya kijinga kuukubali

  Hii dhana ya kusema ''mimi nilipigania sana hizi sheria zifutwe'' ni unafiki fulani kwa maslahi na mtaji wa kisiasa. Kwa hiyo kama alipigania ndio wengine wasipiganie?

  Kwa wakiristo wanafahamu hata Sauli (Paulo) aliyekuwa falisayo kwenye biblia alishangaza hata mitume wa Yesu achilia mbali wayahudi wengine kwa sababu ya kuanza kutenda mambo ambayo kabla yake alikuwa anawaua wale waliokuwa wanayatenda. Kwa leo hii ni mmoja wa mitume wa Yesu waliofanya kazi kubwa ya kueneza neno la Mungu (Matendo Ya Mitume 8:1-14)

  Rais Magufuli kuanza kushughulikia kikamilifu sekta ya maliasili haina tofauti na alichokifanya Sauli (Paulo) huku akiwashangaza CCM na wapinzani.
   
 8. kichakaa man

  kichakaa man JF-Expert Member

  #8
  Jun 13, 2017
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 2,470
  Likes Received: 1,884
  Trophy Points: 280
  Hii nchi inatia hasira sana
   
 9. tutafikatu

  tutafikatu JF-Expert Member

  #9
  Jun 13, 2017
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,603
  Likes Received: 1,430
  Trophy Points: 280
  Duh! Mnatuchanganya bwana.
   
 10. The Hyper

  The Hyper JF-Expert Member

  #10
  Jun 13, 2017
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 885
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  Mmmh Lissu......
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Jun 13, 2017
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,464
  Likes Received: 117,261
  Trophy Points: 280
  Sijawahi kuziona sifa wala majivuno ya Kamanda Lissu.

   
 12. SHAMAC

  SHAMAC JF-Expert Member

  #12
  Jun 13, 2017
  Joined: Feb 9, 2017
  Messages: 1,354
  Likes Received: 3,488
  Trophy Points: 280
  Hivi nyie viongozi wetu kuchambana mtamaliza lini..?? Kila kukicha vichwani mwenu mnawaza " Nimjibuje Lissu, Nimjibuje Magu, Nimjibuje Polepole..,, Hayo maendeleo ya nchi yetu mnayawaza masaa mangapi kwa siku..?? Punguzeni kunyoosheana vidole na kuchambana ifike muda mfikirie mbinu za kututoa kwenye huu umaskini jamani...!!

  Khaa..!! Watu tukifa leo tukaenda mbinguni Mungu akatuuliza " Umewaacha viongozi wako wanafanya nini..? Ntampa jibu rahisi tu " WANACHAMBANA" Tumewaamini jamani aminikeni bhasi na nyie, Tukisema kila mmoja aone mabaya atake kuchukua nchi Patatosha kweli...??
   
 13. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #13
  Jun 13, 2017
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,916
  Likes Received: 1,219
  Trophy Points: 280
  mmh! Namwelewa Tundu Lisu lakini hatoi mapendekezo. Hapo ndipo nguvu ya upinzani inapokosekana. Lisu na wenzake wanapaswa kuja na mapendekezo mbadala kama hayo aliyoagiza Mkuu wetu yana kasoro na siyo maneno tu kama hivi.
   
 14. Eliaskante

  Eliaskante Member

  #14
  Jun 13, 2017
  Joined: Jun 4, 2017
  Messages: 12
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 5
  Unachanganywa na kipi mkuu
   
 15. mirisho pm

  mirisho pm JF-Expert Member

  #15
  Jun 13, 2017
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 2,599
  Likes Received: 3,586
  Trophy Points: 280
  Kuna mambo ukitafakari unahisi nchi ina watu wajinga wengi kama kabla ya uhuru

  Ukweli ni kwamba wakati mikataba hii inasainiwa, zaidi ya robo tatu ya wabunge wote wa upinzani ama walikuwa shuleni au shughuli binafsi/ au wanaharakati.... leo hadhira ile ile iliyoshangilia na kupitisha/ kusaini sheria na mikataba mibovu ya uwekezaji ndio ile ile inayoshangilia ripoti za matokeo ya kazi zao miaka takribani 20 iliyopita tena kwa ukali na kujivika koti la "uzalendo"... its nonsense

  Nikimuangalia Ndungai hadi naona aibu

  Kesho akija mwingine watashangilia tena... Kweli CCM ni ile ile.
   
 16. KikulachoChako

  KikulachoChako JF-Expert Member

  #16
  Jun 13, 2017
  Joined: Jul 21, 2013
  Messages: 14,768
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280
  Sawa...ndugu

  Tumetofautiana mitazamo na maoni hata mambo yenye taswira za kufanana......
   
 17. wambagusta

  wambagusta JF-Expert Member

  #17
  Jun 13, 2017
  Joined: Nov 28, 2014
  Messages: 1,728
  Likes Received: 463
  Trophy Points: 180
  Lissu anatetemeka sasa
   
 18. mandella

  mandella JF-Expert Member

  #18
  Jun 13, 2017
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 2,744
  Likes Received: 1,947
  Trophy Points: 280
  Lissu huwenda unahoji vyema , sema.una haraka mno. Mambo yote uliyoyahoji ni mapendekezo ya sasa ya Rais kuokoa Jahaza jili lililotoboka , ila umejaribu kuyahoji kimmhemuko sana na kwa speed ya hali ya juu.Kila jambo litatendekea kwa utaratibu wake, sidhani kama hayo yote uliyojaribu kuyahoji yangeweza kufanyika leo.

  2. Unapose kipindi fulani mlihoji kuhusu mikataba mkapuuzwa , je mngependelea kuendelea kupuuzwa ? Au ni ipi Logic ya kile unachotaka kukihoji.
   
 19. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #19
  Jun 13, 2017
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 23,611
  Likes Received: 14,670
  Trophy Points: 280
  Mbona hazungumzii ukwepaji kodi wa acacia?
   
 20. pumzihaiuzwi

  pumzihaiuzwi JF-Expert Member

  #20
  Jun 13, 2017
  Joined: Mar 27, 2015
  Messages: 2,552
  Likes Received: 1,931
  Trophy Points: 280
  Lisu kaliamsha dude...
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...