Lissu: Serikali ya Magufuli imejaa wapigaji

Lissu: Serikali ya Magufuli imejaa wapigaji

Alisema jana kuwa ananyoosha nchi kwanza, kwa mfumo wa nchi yetu, Rais ndiye kila kitu, hivo Mh. Rais anajua kabisa akiondoka tu hali inaweza kubadilika huku nyumbani.

Kikwete aliwaachia uhuru wa kutosha mawaziri na watendaji wake serikalini yeye akawa anazurura tu nje ya nchi, yaliyotokea kila mtu anayajua
Ww unadhani Kikwete alikuwa anazurura? Ukikaa ndani kuna fursa nyingi sana, hata za mali na maarifa mapya utayakosa. Mbona watu wanaishi na panya ndani nyumba moja, mwenye nyumba safiri, usisafiri panya kazi yao ni uharibifu baada ya shibe. Hivyo bora kusafiri, maana panya hawachungiki kama mifugo.
 
Naona kabisa makamu wa raisi akikataa kuendelea kugombea uchaguzi ujao
 
Lisu subiri mtakopopata rais wenu haya mnayosema saiz wala hajengi chama chenu mtabaki kulalamika tu bila kufanya jitihada za kujenga chama mnachemka,majukwaaa mnayotumia kumsakama rais na serikali yake hebu yatumieni kuuza Sera mbadala kwa wananchi,Huo ulalamishi na kusubiri Magu afanye/aseme kitu ndipo mponde msidhani kutawapa credit kwa wananchi waliowengi.Hatukatai kushauri lakini namna mnayoitumia kushauri siyo sahihi.OVER
 
Aende nje kwani ndiko waliko waliomchagua?kule akachukue nini kwa mfano?shauriyeni kalieni kumjadili 2020 sio mbali Mara 2025 hiyo hapo.
 
Alivyoenda Ethiopia kwahiyo hakuogopa wapigaji ?

ziliandaliwa process za kuagiza vile vichwa vya treni sasa jamaa hatok wote wameingia mtini kwenda kuvifuata.
 
Lisu subiri mtakopopata rais wenu haya mnayosema saiz wala hajengi chama chenu mtabaki kulalamika tu bila kufanya jitihada za kujenga chama mnachemka,majukwaaa mnayotumia kumsakama rais na serikali yake hebu yatumieni kuuza Sera mbadala kwa wananchi,Huo ulalamishi na kusubiri Magu afanye/aseme kitu ndipo mponde msidhani kutawapa credit kwa wananchi waliowengi.Hatukatai kushauri lakini namna mnayoitumia kushauri siyo sahihi.OVER

kwa hiyo ni sahihi akitoka anaibiwa?
 
Heshim kwenu wakuu,

Mbunge Tundu Lissu, amehoji Maswali Mawili;

1. Kama Rais Magufuli hawezi kusafiri nje kwa kuogopa wapigaji, maana yake ni kwamba serikali yake yote, kuanzia Makamu wa Rais, ni wapiga dili.

2. Hivi Juliana Shonza na MaCCM wenzake wataweza kuja kutoa ushahidi mahakamani kwa mashtaka ambayo wamewafungulia wabunge wa CHADEMA leo?

WAKATI utawala wa Rais Dk. John Magufuli ukikaribia mwaka wa pili, huku akiwa amesafiri nje ya nchi mara chache ikilinganishwa na watangulizi wake, amevunja ukimya akisema kwamba anataka kwanza kumaliza wapiga dili ambao akiondoka wataweza kufanya mambo ya ajabu.

Amesema tangu aingie madarakani amepata mialiko zaidi ya 60 kwenda nje ya nchi, lakini ameikataa kwa sababu anataka kuishughulikia Tanzania kwanza.

Rais Magufuli alitoa kauli hiyo jana wakati akizindua mradi wa uboreshaji maji wa Sengerema akiwa katika ziara yake mkoani Mwanza.

“Ndiyo maana mimi sitembei sana, nikienda huko watafanya ya ajabu, ngoja nidili nao kwanza, lazima nihakikishe nasafisha kwanza.

“Leo (jana) nilitakiwa niwe Ethiopia kwenye mkutano wa AU, nimeona nimtume makamu wangu (Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan), ameniwakilisha na anafanya kazi vizuri, mimi ngoja nidili na ya watu kwa sababu nilichaguliwa kwa ajili ya Watanzania, safari nitaenda nikishastaafu.

“Ngoja nizifanyizie safari humu humu ndani kwani ningejuaje kama kuna Sh bilioni mbili za maji zimeibwa na kama wapo walioziiba waanze kuzirudisha.

“Kabla sijaondoka vyombo vyangu vitaanza kufuatilia kwa sababu nina Serikali iko hapa. Lazima mali za watu masikini ziende kuwanufaisha watu, ndio wajibu wangu na ndio haki yao,” alisema.

Wakati huo huo leo Viongozi wa Juu na Wabunge wa Chadema wamefurika nje ya jengo la Makakama Kuu Mjini Dodoma kusubiri kesi ya shambulio la mwili inayomkabili Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea.

Kubenea anashitakiwa kwa kosa la kumshambulia Mbunge wa Viti Maalum, Juliana Shonza.
Ukweli anaogopa kuongea kizungu na wenzake
 
Kama Samia anafanya vizuri na anamuamini anaogopa nini kumuacha Ili aendeleze kazi ya kupambana na wapiga dili?.
Nadhani hujamwelewa mkuu, yeye anaamini watz wote ni wapiga dili, na mwenye uwezo wa kupambana nao ni yeye tu. Huko nje anawatuma kwa sababu hakuna kupiga dili huko, lakini wakibaki hapa na yeye akatoka watapiga tu. Hayo ndio mawazo yake na anachoamini yeye.
 
Unapojitegemea mwenyewe kunyoosha nchi utafeli,atengeneze institutions strong yeye awepo asiwepo watu wanafuata taratibu na kuwajibika wanaposhindwa. Hizi kauli za marudio kila siku ukizitafakari unashindwa kuona vision pana ya kiongozi. Unatumbua unaweka watu wengine bila ku address gaps zilizopo ukiamini wataogopa kutumbuliwa kumbe watu sasa wanajipanga hata kabla ya kuanza ufisadi.
Tusiwe na papara nia ni njema basi tujipange na isiwe kama tunatafuta utukufu wa muda mfupi
 
Hizo so called 'institutions strong' zinatengenezwaje?
 
Sio tena anakwepa gharama bali kwa sasa anapambana n wapigaji!Nachokumbuka alishapata kusema hatasafiri na hasafiri kwa sababu ya GHARAMA na yeye anabana matumizi
Kuwa muongo ni gharama sana, hilo alishasahau
 
Mbona Rwanda, Kenya na Ethiopia huko huko alienda. Je hakukuwa na wapigaji?
 
Lissu kila akimsikia Magufuli anaonge lazima ajibu. Mbowe anaangalia sinema tu lakini anajua wapi korongo lilipo.
Kwa vile ndiye mtu pekee ccm na mifumo yake yote imemshindwa, imesurrender kwa lissu. Imechoka kumfukuza kwa defender za polisi imebaki vita ya matusi na kejeli za majukwaan huku wakijifunika na koti la uzalendo uchwara
 
Wapiga dili ni kina Nani hass, wanatoka ccm au upinzani?
 
Back
Top Bottom