Lissu: Magufuli anatulisha matango pori, toka mwaka 1999 alikuwa anaunga mkono uuzwaji wa migodi, hicho kishika uchumba Accacia wako mahakamani

Kuna kitu hakiko sawa. Barric ni mwanahisa mkubwa katika Accacia. Accacia ina bodi yake ambayo inapaswa kukaa na kufanya maamzi ili yaweze kutekelezwa. Barric wanasema watalipa, Accacia wanasema hawana taarifa. Accacia wanafungua kesi mahakani Barric hawasemi kitu!

Kumbuka Accacia wako listed na wanahisa wana maslahi katika maamzi yatakayowanufaisha. Hivyo kauli za wanahisa zina matokeo ama chanya au hasi katika thamani ya hisa kwenye solo la London. Ni nani mkweli...Barric hawawezi kuamua peke yao na Accacia pia hawawezi kufanya maamzi peke yao. Kauli na vitendo vyao vinavyokinzana vinatoa picha gani?
 
Lissu utaambiwa si mzalendo, wakati ule mnapiga kelele kwamba wahuni wa CCM wanauza rasilimali, mr mzalendo alikuwa anapiga vigelegele kumpongeza mkapa ..
leo eti hayumo, na kwamba hata nyumba za umma hakuwahonga yeye akina Mussa,mtoto wa dada !

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Salaam,
Nakutakia afya njema na nakuombe upone katika operesheni yako ya 23.

Masuala ya JPM Barrick, Accacia mwachie Mwenyewe, aliyeyaanzisha ndiye atakayeyamaliza, kama wewe unaendelea na ya kwako endelea!! Hujalazimishwa kulalamikia mambo yanayofanywa na mtu mwingine.

Yeye anafanya katika kile ambacho anaona sawa, kwa maana nyingine siyo lazima atumie ushauri wako katika kushughulikia mambo hayo. Umekuwa na tabia ya kuingilia namna Rais anavyofanya kazi zake sio sawa, mwache ashindwe au aweze mwenyewe, kama yeye amehakikishiwa watalipa basi subiri uone nini kitatokea, acha maneno maneno yako.
Ndugu! Upo sirias kwamba kiongozi aachwe afanye kama anavyoona inafaa? Kwani hii nchi ni mali ya mtu mmoja au waTZ wote?

Kwani ni kosa kiongozi kukosolewa?

Hakika Tanzania tuna safari ndefu juu ya wananchi kujitambua!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo point yake ni nini sasa? Magufuli aachane na hawa wazungu au.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu muulizeni kwanza anakutana lini na Trump na Papa?.., baada ya kuwika kwa wiki mbili BBC,DW,VOA.. CNN na ALJAZEERA wakamtolea nje, anatafuta namna ya kuwika tena. Lissu hana jipya na ndo kwisha habari yake. Niliwaambia zile zilikuwa kelele,Sasa anaanza kurudia story zake zilezile za 1999.
 
Anaandika #Tundu_Lissu

21.02.2019

'Nateseka' na hili suala kwa sababu 'nimeteseka' nalo toka mwaka 1999, wakati Magufuli 'akiunga mkono' juhudi za Rais Mkapa za kuuza utajiri wetu kwa wageni. Huu ni mwaka wangu wa 20 'nateseka' nalo na nitaendelea kuteseka nalo as long as nina pumzi.

Mnadanganywa na tunadanganywa na Magufuli na watu wake. Alipokuja President John Thornton mwaka jana, tuliambiwa Barrick watalipa 'kishika uchumba' (á la Prof. Kabudi) cha dola 300m.

Hawakulipa. Kwa nini??? Kwa sababu Acacia Mining walikataa. Badala yake walitufungulia kesi ya kuvunja mikataba yao ICSID, wanakotudai mabilioni ya dola.

Sasa amekuja President Willem Jacobs. Naye amesema Barrick watalipa 'kifuta machozi' cha dola 300m, lakini mpaka kwanza 'independent board of directors' ya Acacia Mining wakubali. Hao hao waliokataa kulipa mwaka jana wanatakiwa wakubali kulipa sasa.

Halafu kwenye press release yao iliyotolewa jana hiyo hiyo, Barrick wanasema ahadi zao hizo kwa Magufuli ni 'forward looking statements' ambazo, kwa kifupi, sio makubaliano yoyote yenye nguvu za kisheria. Hawafungwi na chochote walichokisema kwenye makubaliano yao na Serikali ya Tanzania.

Ndio maana nimesema someni hiyo disclaimer vizuri. Wazungu hawa sio wajinga. Wanasema hizo 'forward looking statements' zao zinaweza kuathiriwa na kesi au mashauri yanayoendelea mahakamani. Maana yake ni nini??? Wakitushinda kwenye kesi waliyotufungulia ICSID hawatatulipa.

Wanasema hizo 'forward looking statements' zao zinaweza kuathiriwa na faida au hasara katika uwekezaji wao. Maana yake ni nini??? Wakipata hasara hawatatulipa.

Sheria ya sasa ya Madini inasema mkataba wowote unaohusu madini unatakiwa kuwasilishwa Bungeni. Kama hawatulishi matango pori watayawasilisha makubaliano haya bungeni. Wasipoyawasilisha ujue ni matango pori.
Ndio maana haponi huyu, mishono inahitaji atulie yeye kutwa nzima kufungua bakuli.
Si kadai anafanyiwa operation nyingine aka dressing ya kidonda huyu?
 
Mkuu muulizeni kwanza anakutana lini na Trump na Papa?.., baada ya kuwika kwa wiki mbili BBC,DW,VOA.. CNN na ALJAZEERA wakamtolea nje, anatafuta namna ya kuwika tena. Lissu hana jipya na ndo kwisha habari yake. Niliwaambia zile zilikuwa kelele,Sasa anaanza kurudia story zake zilezile za 1999.

Vipi mmeshawalipa wauza koroshow
 
Anaandika #Tundu_Lissu

21.02.2019

'Nateseka' na hili suala kwa sababu 'nimeteseka' nalo toka mwaka 1999, wakati Magufuli 'akiunga mkono' juhudi za Rais Mkapa za kuuza utajiri wetu kwa wageni. Huu ni mwaka wangu wa 20 'nateseka' nalo na nitaendelea kuteseka nalo as long as nina pumzi.

Mnadanganywa na tunadanganywa na Magufuli na watu wake. Alipokuja President John Thornton mwaka jana, tuliambiwa Barrick watalipa 'kishika uchumba' (á la Prof. Kabudi) cha dola 300m.

Hawakulipa. Kwa nini??? Kwa sababu Acacia Mining walikataa. Badala yake walitufungulia kesi ya kuvunja mikataba yao ICSID, wanakotudai mabilioni ya dola.

Sasa amekuja President Willem Jacobs. Naye amesema Barrick watalipa 'kifuta machozi' cha dola 300m, lakini mpaka kwanza 'independent board of directors' ya Acacia Mining wakubali. Hao hao waliokataa kulipa mwaka jana wanatakiwa wakubali kulipa sasa.

Halafu kwenye press release yao iliyotolewa jana hiyo hiyo, Barrick wanasema ahadi zao hizo kwa Magufuli ni 'forward looking statements' ambazo, kwa kifupi, sio makubaliano yoyote yenye nguvu za kisheria. Hawafungwi na chochote walichokisema kwenye makubaliano yao na Serikali ya Tanzania.

Ndio maana nimesema someni hiyo disclaimer vizuri. Wazungu hawa sio wajinga. Wanasema hizo 'forward looking statements' zao zinaweza kuathiriwa na kesi au mashauri yanayoendelea mahakamani. Maana yake ni nini??? Wakitushinda kwenye kesi waliyotufungulia ICSID hawatatulipa.

Wanasema hizo 'forward looking statements' zao zinaweza kuathiriwa na faida au hasara katika uwekezaji wao. Maana yake ni nini??? Wakipata hasara hawatatulipa.

Sheria ya sasa ya Madini inasema mkataba wowote unaohusu madini unatakiwa kuwasilishwa Bungeni. Kama hawatulishi matango pori watayawasilisha makubaliano haya bungeni. Wasipoyawasilisha ujue ni matango pori.
HAWAAMINIKI HAO.nI KIKI ZISIZO NA MASHIKO KISHERIA.KABUDI ALIPOKUWA ANAONGEA "BODY LANGUAGE" ILIKUWA WAZI ALIKUWA ANADANDANYA!'
 
Back
Top Bottom