Ulinzi wa rasilimali za Taifa, Magufuli kiboko!, hataki mchezo kabisa!, Boss wa Acacia anyimwa viza kuingia Tanzania, Barrick yafunguka kila kitu!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,575
Wanabodi,

Kufuatia mgogoro wa Acacia na serikali yetu ulipelekea rais Magufuli kupiga marufuku usafirishaji wa makinikia ya Acacia, kulikopelekea baba wa Acacia Barrick kuingilia kati na hatimaye kufanyika mazungumzo na serikali yetu hadi kufikia makubaliano, lakini kabla makubaliano hayo hayatiwa saini ili yatekelezwe na Acacia, serikali akiandika barua kutoitambua Acacia, hivyo kuilazimisha Barrick kuinunua Acacia asilimia 100%, Acacia afungashe virago, ndipo makubaliano yasainiwe na kutekelezwa.

Jana Barrick wameweka wazi kila kitu, katika uwazi huo, wameonyesha kuwa rais Magufuli na serikali yake, katika suala la kulinda rasilimali za taifa, ni kiboko, sio mtu wa mchezo mchezo, hataki masikhara wala hakuna cha mswalie Mtume!. kumbe baada ya barua zile za kutoitambua Acacia, Boss wa Acacia akataka kuja Tanzania kuweka mambo sawa, lakini amekataliwa viza, hivyo hawezi kuingia Tanzania, hali ambayo inailazimu Barrick kuinunua Acacia ili hili jambo limalizike rasmi.

Siku ya jana Barrick wametoa Press Releases kuhusu jambo hili hili Acacia wakitoa press release yao

Update: Acacia Mining plc – Situation in Tanzania and Review of Acacia Mine Plans – June 18, 2019

Update: Acacia Mining plc – Extension of PUSU Deadline - June 18, 2019

Kwanza Barrick waliomba kwa Acacia kuongeza muda wa kutoa firm offer ya kuinunua Acacia, ambapo kwa tangazo la awali, tarehe ya jana ndio ilikuwa tarehe ya mwisho kwa Barrick kutoa a firm offer, lakini kabla ya kutolewa kwa firm offer, lazima Acacia wakubali kununuliwa.

Tangu offer ya Barrick kutolewa, Acacia amegoma kukubali kununuliwa kwa hoja kuwa offer ya Barrick ni kiduchu sana huko Acacia akionyesha jinsi alivyo na thamani hivyo Bariick waongeze dau.

Barrick katika taarifa yao, wameendelea kushikilia kuinunua Acacia kwa bei kituchu ile ile na kutoa taarifa yao ya utafiti kuwa Acacia anajithaminisha kwa thamani ya juu kuliko halisia, hivyo Barrick amemwaga hadharani kila kitu kuhusu Acacia, na akawasisitiza kuwa hilo dau ni very fair kwa situation ya Acacia na tena kwenye firm offer wanaweza kushuka, anayetaka auze, asieataka itakula kwake kwa sababu Acacia haiwezi kufanya kitu tena Tanzania.

Hawa Barrick wanasema na hapa ninanukuu,
"GoT unwilling to enter into settlement with Acacia As set out in the announcements made by Barrick and Acacia on May 21 and 22, 2019, the GoT negotiating team has written to Acacia’s three Tanzanian operating companies (the “TMCs”) to indicate that the GoT is resolved that it will not proceed to execute final agreements for the resolution of Acacia’s disputes if Acacia is one of the counterparties to the agreements. While a basis for a settlement has been developed, the terms have not yet been finalized and therefore still carry significant risk. Importantly, as highlighted by statements made by a GoT spokesperson and prominently reported in Tanzanian press, “the Government does not want the presence of Acacia in any form in the country” 2 and “the Government has demanded that under no circumstances can Acacia be party to the agreements”

Wenzangu naombeni mnisaidie msikute ni mimi ndio nilipitwa na hii habari, ni lini msemaji wa serikali yetu alitangaza hayo na kuwa prominently reported in Tanzania Press?. Hivi iliwahi kutolewa statement yoyote na serikali yetu kuwa “the Government does not want the presence of Acacia in any form in the country”?,

Masikini Barrick, wao wanajua kuwa Watanzania tuliambiwa na msememaji wa serikali yetu, kumbe hawajui kuwa masikini sisi Watanzania, haya mambo ndio tunayasikia kutoka kwao, tangu lile la serikali yetu kuandika barua, tumelisikia kwao, na sikumbuki kama tumewahi kuelezwa chochote na serikali yetu mpaka sasa.

Barrick akaendelea kueleza mambo makubwa matano ambayo bado ni kikwazo kwa Acacia na hapa ninanukuu.

Operating environment and loss of social license The operating environment in Tanzania is increasingly challenging for the TMCs and there are no signs that this situation is improving. Indeed, Barrick’s own assessment is that the situation may deteriorate further if no near-term settlement can be secured. Examples of how difficult the operating environment has become include:
  1. Export ban: the continuing ban on the export of metallic mineral concentrates announced by the GoT in March 2017
  2. Bulyanhulu on care & maintenance: Bulyanhulu remains on care and maintenance, other than some reprocessing of tailings
  3. Criminal charges and detentions: Criminal charges have been brought against the TMCs in Tanzania and against three current Acacia employees and a former employee. Three of those individuals charged continue to be held in custody under non-bailable offences
  4. CEO unable to enter Tanzania: Barrick understands that the Interim CEO of Acacia has not been able to visit Tanzania since October 2018 and that no one from the senior management or Board of the Company has been able to engage with the GoT at a senior governmental level regarding the issues in dispute between Acacia and the GoT
  5. Environmental investigations: there remains the threat of additional environmental penalties and environmental protection orders being levied in relation to North Mara Barrick believes that unless a solution is found to the current impasse in the short term there is the real risk of catastrophic loss of value for all stakeholders, and that the solution it has proposed to the Independent Directors of Acacia represents the only credible option to preserve, to the extent possible, the value of Acacia’s assets.
Wanachoeleza hapa ni kuwa
  1. Makinikia ya Acacia bado yapo na yameshikiliwa na bado ile export ban inaendelea, hakuna ku export
  2. Viongozi wakuu watatu waandamizi wa Acacia bado wanashikiliwa mahabusu kwa mashitaka ambayo hayana dhamana.
  3. Mgodi wa Bulyanhulu uliokuwa ukizalisha makinikia ni kama umesimama kwa kuendelea na kazi ndogo ndogo.
  4. Boss wa Acacia amenyimwa visa ya kuingia nchini kuja kufanya lolote
  5. Mgodi wa North Mara umepigwa faini ya kufa mtu ya mambo ya mazingira
Hapa Barrick wanawaeleza shareholders wa Acacia kuwa hali bado ni tete, bora wakubali kununua kwa hizo fedha kiduchu vinginevyo watapoteza kila kila.

Pia Barrick wamekumbushia kilichokubaliwa na tumeisha kizungumza sana humu.
"Draft settlement and sustainable framework for future operations are expected to result in significant value transfer to GoT The key principle of the draft settlement agreements under discussion is that going forward
  1. the GoT and the TMCs will share the economic benefits derived from the Tanzanian mines on a 50/50 basis, based on the life of mine plans of the TMCs.
  2. The GoT will receive its share of economic benefits through taxes, royalties, fees and other fiscal levies and through the GoT’s 16% free carried interest in all distributions (including shareholder loan repayments) from the TMCs and
  3. a new Tanzanian management company.
  4. The 50/50 sharing arrangement will be reviewed annually to seek to ensure that the actual and projected sharing of economic benefits is in accordance with the 50/50 principle.
  5. The agreements also provide for payment by the Acacia group of the aggregate sum of US$300 million in consideration for the full, final and comprehensive settlement of all existing disputes between the GoT and the Acacia group including all liability to taxation and a waiver of actual or potential claims on a mutual basis.
  6. This US$300 million payment is outside of (and therefore not taken into account for the purposes of) the 50/50 sharing of the economic benefits over time.
  7. The draft settlement does involve a significant value transfer from Acacia to the GoT but this has been critical to agreeing potential draft settlement terms with the GoT and the creation of a viable operating framework for the TMCs going forward.
Hitimisho.
Kwa jinsi wazungu hawa wanavyolia lia na kuhenya henya, inaonyesha wazi kabisa katika suala la ulinzi wa rasilimali zetu, rais Magufuli yuko very serious, sio mtu wa mchezo mchezo, japo hili sio jambo zuri kwenye investment climate yetu kuifanya Tanzania ni risk country to invest, msimamo huu wa Rais Magufuli hauna budi kuungwa mkono na wazalendo wote wa kweli wa taifa letu, kama ni mwekezaji kuja, ajue kabisa tunataka wawekezaji wa ukweli wa kugawana faida kwa a win win situation na sio wawekezaji wa kuja tuu kuchuma Tanzania kwa kutufanya ni shamba la bibi!.

Kwa hili, hongera sana rais Magufuli na serikali yako kwa misimamo isiyo yumba, na japo tumekubali kusamehe deni lote la dola bilioni 190, na kukubali kupokea kile kishika uchumba tuu cha dola milioni 300, something is better than nothing!, ni bora tupokee milioni 300 za ukweli kuliko bilioni 190 za matumaini hewa!.

Mungu mbariki Magufuli na serikali yake washinde vita hii na waweze kuikomboa Tanzania kichumi.
Mungu ibariki Tanzania.

Jumatano Njema.

Paskali.
Update.
Leo Acacia wametoa press release kukanusha taarifa ya Barrick
Rejea
https://www.jamiiforums.com/threads...akubaliano-yoyote-na-tanzania.1551527/page-20
 
Madhara hayataonekana sasa, ila muda utatoa majibu, Haya maamuzi ya Kisukuma ya Kukurupuka kila jambo na Kutukana Washauri wako (Mawaziri) halafu tukaja kupaa Kiuchumi ni ndoto, Barrick wanaonekana Wanaume kwa sasa ila hakuna kitakachobadilika, Magu Amekuwa Bungeni zaidi ya Miaka 20 Sikuwahi kumsikia akiongelea Rasilimali za Nchi .
 
I knew Pascal kuna vitu kapenyeza kwenye bandiko lake....mfano fuatilia hapo chini
====
...japo tumekubali kusamehe deni lote la dola bilioni 190, na kukubali kupokea kile kishika uchumba tuu cha dola milioni 300....,
Huu msamaha ulitangazwa lini?
...japo hili sio jambo zuri kwenye investment climate yetu kuifanya Tanzania ni risk country to invest,...
US wana worst investment kuliko sisi...huoni wanavyoyumbisha uchumi wa Dunia na kuvunja vunja mikataba ya kimataifa iliyokubalika na pande mbili na hii ndiyo their poor investment climate...UK the same, wamepora dhahabu za Caracas, Canada usiseme...wamemfunga CEO wa fedha wa HUWAWEI...Sasa hawa nilowataja wakifanya hivyo hawavurugi investment climate yao...ila sisi (Tanzania) tukilinda rasilimali zetu ndiyo tunavuruga investment climate yetu. Mkuu Paskali, sikuelewi ujue!!! Mkuu yawezekana mimi sielewi 'conducive investment climate' naomba ufafanuzi.
 
I knew Paskal kuna vitu kapenyeza kwenye bandiko lake....mfano fuatilia hapo chini
====
Huu msamaha ulitangazwa lini?
US wana worst investment kuliko sisi...huoni wana youmbisha uchumi wa Dunia na kuvunja vunja mikataba ya kimataifa iliyokubalika na pande mbili na hii ndiyo their poor investment climate...UK the same, wamepora dhahabu za Caracas, Canada usiseme...wamemfunga CEO wa fedha wa HUWAWEI...Sasa hawa nilowataja wakifanya hivyo hawavurugi investment climate yao...ila sisi (Tanzania) tukilinda rasilimali zetu ndiyo tunavuruga investment climate yetu. Mkuu Paskali, sikuelewi ujue!!! Mkuu yawezekana mimi sielewi 'conducive investment climate' naomba ufafanuzi.
Kwa hiyo wewe unajifaninisha na Canada,Marekani na Waingereza?

Halafu nani kakuambia kuwa Kila linalofanywa na hao jamaa ni sahihi?

Hao jamaa ni level nyingine kabisa. Sisi tunapaswa kufikiri tofauti sana. Work smarter not harder .

Tukishakuwa na nguvu za uchumi tunaweza hata sisi kufanya kiburi kama cha hao jamaa. Misimamo ya kikomonist kwa sasa haitatusaidia. Nyerere alijaribu sana hakufanikiwa.
 
Wanabodi,

Kufuatia mgogoro wa Acacia na serikali yetu ulipelekea rais Magufuli kupiga marufuku usafirishaji wa makinikia ya Acacia, kulikopelekea baba wa Acacia Barrick kuingilia kati na hatimaye kufanyika mazungumzo na serikali yetu hadi kufikia makubaliano, lakini kabla makubaliano hayo hayatiwa saini ili yatekelezwe na Acacia, serikali akiandika barua kutoitambua Acacia, hivyo kuilazimisha Barrick kuinunua Acacia asilimia 100%, Acacia afungashe virago, ndipo makubaliano yasainiwe na kutekelezwa.

Jana Barrick wameweka wazi kila kitu, katika uwazi huo, wameonyesha kuwa rais Magufuli na serikali yake, katika suala la kulinda rasilimali za taifa, ni kiboko, sio mtu wa mchezo mchezo, hataki masikhara wala hakuna cha mswalie Mtume!. kumbe baada ya barua zile za kutoitambua Acacia, Boss wa Acacia akataka kuja Tanzania kuweka mambo sawa, lakini amekataliwa viza, hivyo hawezi kuingia Tanzania, hali ambayo inailazimu Barrick kuinunua Acacia ili hili jambo limalizike rasmi.

Siku ya jana Barrick wametoa Press Releases kuhusu jambo hili hili Acacia wakitoa press release yao

Update: Acacia Mining plc – Situation in Tanzania and Review of Acacia Mine Plans – June 18, 2019

Update: Acacia Mining plc – Extension of PUSU Deadline - June 18, 2019

Kwanza Barrick waliomba kwa Acacia kuongeza muda wa kutoa firm offer ya kuinunua Acacia, ambapo kwa tangazo la awali, tarehe ya jana ndio ilikuwa tarehe ya mwisho kwa Barrick kutoa a firm offer, lakini kabla ya kutolewa kwa firm offer, lazima Acacia wakubali kununuliwa.

Tangu offer ya Barrick kutolewa, Acacia amegoma kukubali kununuliwa kwa hoja kuwa offer ya Barrick ni kiduchu sana huko Acacia akionyesha jinsi alivyo na thamani hivyo Bariick waongeze dau.

Barrick katika taarifa yao, wameendelea kushikilia kuinunua Acacia kwa bei kituchu ile ile na kutoa taarifa yao ya utafiti kuwa Acacia anajithaminisha kwa thamani ya juu kuliko halisia, hivyo Barrick amemwaga hadharani kila kitu kuhusu Acacia, na akawasisitiza kuwa hilo dau ni very fair kwa situation ya Acacia na tena kwenye firm offer wanaweza kushuka, anayetaka auze, asieataka itakula kwake kwa sababu Acacia haiwezi kufanya kitu tena Tanzania.

Hawa Barrick wanasema na hapa ninanukuu,

Wenzangu naombeni mnisaidie msikute ni mimi ndio nilipitwa na hii habari, ni lini msemaji wa serikali yetu alitangaza hayo na kuwa prominently reported in Tanzania Press?. Hivi iliwahi kutolewa statement yoyote na serikali yetu kuwa “the Government does not want the presence of Acacia in any form in the country”?,

Masikini Barrick, wao wanajua kuwa Watanzania tuliambiwa na msememaji wa serikali yetu, kumbe hawajui kuwa masikini sisi Watanzania, haya mambo ndio tunayasikia kutoka kwao, tangu lile la serikali yetu kuandika barua, tumelisikia kwao, na sikumbuki kama tumewahi kuelezwa chochote na serikali yetu mpaka sasa.

Barrick akaendelea kueleza mambo makubwa matano ambayo bado ni kikwazo kwa Acacia na hapa ninanukuu.

Wanachoeleza hapa ni kuwa
  1. Makinikia ya Acacia bado yapo na yameshikiliwa na bado ile export ban inaendelea, hakuna ku export
  2. Viongozi wakuu watatu waandamizi wa Acacia bado wanashikiliwa mahabusu kwa mashitaka ambayo hayana dhamana.
  3. Mgodi wa Bulyanhulu uliokuwa ukizalisha makinikia ni kama umesimama kwa kuendelea na kazi ndogo ndogo.
  4. Boss wa Acacia amenyimwa visa ya kuingia nchini kuja kufanya lolote
  5. Mgodi wa North Mara umepigwa faini ya kufa mtu ya mambo ya mazingira
Hapa Barrick wanawaeleza shareholders wa Acacia kuwa hali bado ni tete, bora wakubali kununua kwa hizo fedha kiduchu vinginevyo watapoteza kila kila.

Pia Barrick wamekumbushia kilichokubaliwa na tumeisha kizungumza sana humu.

Hitimisho.
Kwa jinsi wazungu hawa wanavyolia lia na kuhenya henya, inaonyesha wazi kabisa katika suala la ulinzi wa rasilimali zetu, rais Magufuli yuko very serious, sio mtu wa mchezo mchezo, japo hili sio jambo zuri kwenye investment climate yetu kuifanya Tanzania ni risk country to invest, msimamo huu wa Rais Magufuli hauna budi kuungwa mkono na wazalendo wote wa kweli wa taifa letu, kama ni mwekezaji kuja, ajue kabisa tunataka wawekezaji wa ukweli wa kugawana faida kwa a win win situation na sio wawekezaji wa kuja tuu kuchuma Tanzania kwa kutufanya ni shamba la bibi!.

Kwa hili, hongera sana rais Magufuli na serikali yako kwa misimamo isiyo yumba, na japo tumekubali kusamehe deni lote la dola bilioni 190, na kukubali kupokea kile kishika uchumba tuu cha dola milioni 300, something is better than nothing!, ni bora tupokee milioni 300 za ukweli kuliko bilioni 190 za matumaini hewa!.

Mungu mbariki Magufuli na serikali yake washinde vita hii na waweze kuikomboa Tanzania kichumi.
Mungu ibariki Tanzania.

Jumatano Njema.

Paskali.
Rejea
https://www.jamiiforums.com/threads...akubaliano-yoyote-na-tanzania.1551527/page-20
Kweli huyu kwa kulinda rasilimali ni kiboko ndio mana TWIGA kawasogeza karibu na nyumbani ili awalinde kwa ukaribu zaidi.
 
Bado natafakari maneno "Kulinda rasilimali" na kumnyima mtu visa sioni kama yanarandana. Kwani wakati Tanzania inaingia mikataba na hayo makampuni hao mabosi walikuwa humu nchini?
 
Tusemeje Sasa?
748868178.jpeg
 
Back
Top Bottom