Lissu: Magufuli anatulisha matango pori, toka mwaka 1999 alikuwa anaunga mkono uuzwaji wa migodi, hicho kishika uchumba Accacia wako mahakamani

Anaandika #Tundu_Lissu

21.02.2019

'Nateseka' na hili suala kwa sababu 'nimeteseka' nalo toka mwaka 1999, wakati Magufuli 'akiunga mkono' juhudi za Rais Mkapa za kuuza utajiri wetu kwa wageni. Huu ni mwaka wangu wa 20 'nateseka' nalo na nitaendelea kuteseka nalo as long as nina pumzi.

Mnadanganywa na tunadanganywa na Magufuli na watu wake. Alipokuja President John Thornton mwaka jana, tuliambiwa Barrick watalipa 'kishika uchumba' (á la Prof. Kabudi) cha dola 300m.

Hawakulipa. Kwa nini??? Kwa sababu Acacia Mining walikataa. Badala yake walitufungulia kesi ya kuvunja mikataba yao ICSID, wanakotudai mabilioni ya dola.

Sasa amekuja President Willem Jacobs. Naye amesema Barrick watalipa 'kifuta machozi' cha dola 300m, lakini mpaka kwanza 'independent board of directors' ya Acacia Mining wakubali. Hao hao waliokataa kulipa mwaka jana wanatakiwa wakubali kulipa sasa.

Halafu kwenye press release yao iliyotolewa jana hiyo hiyo, Barrick wanasema ahadi zao hizo kwa Magufuli ni 'forward looking statements' ambazo, kwa kifupi, sio makubaliano yoyote yenye nguvu za kisheria. Hawafungwi na chochote walichokisema kwenye makubaliano yao na Serikali ya Tanzania.

Ndio maana nimesema someni hiyo disclaimer vizuri. Wazungu hawa sio wajinga. Wanasema hizo 'forward looking statements' zao zinaweza kuathiriwa na kesi au mashauri yanayoendelea mahakamani. Maana yake ni nini??? Wakitushinda kwenye kesi waliyotufungulia ICSID hawatatulipa.

Wanasema hizo 'forward looking statements' zao zinaweza kuathiriwa na faida au hasara katika uwekezaji wao. Maana yake ni nini??? Wakipata hasara hawatatulipa.

Sheria ya sasa ya Madini inasema mkataba wowote unaohusu madini unatakiwa kuwasilishwa Bungeni. Kama hawatulishi matango pori watayawasilisha makubaliano haya bungeni. Wasipoyawasilisha ujue ni matango pori.

Ƙwa kuwa Jiwe na wafuasi wake wamekataa maarifa na ufahamu uletao ushindi waachwe katika njia waliƴochagua mpaka watakapotambu wao wenyewe na mɗa hautakuwa upande wao tena!
 
wakati anayasema hayo dawa ya lignocaine (ganzi) ilikuwa imeisha mwilini, au bado hajajitambua

TL aliyoyasema amewalenga watu wenye akili na utambuzi kama yeye; wanaoijua kesho yao; hakuwalenga vichwa panzi kama wewe maana anaelewa hutamuelewa, TL sio calibre ya Kichaa mpya kama wewe na wenzako wa aina yako!
 
Kuna watu wanajua wanadanganywa ila hawana la kufanya zaidi ya kumsadia kudanganya

Jiwe yupo point of no return maana akirudi kuyafanyia kazi maneno ya Lissu basi itakua kakubali Lissu hakua mpotoshaji bali yeye
Sidhani hata huwa anamfikilia.
 
wakati anayasema hayo dawa ya lignocaine (ganzi) ilikuwa imeisha mwilini, au bado hajajitambua
Umepeleka umbea wa uzi wa kuomba magufuli sijui amsamehe mbowe cjui afanye nini na nini... now upo kupambia huku tena.... wewe ni kaburi...ushabiki ni mbya sana... ichaji akili yako kwanza
 
Back
Top Bottom