Lissu: Magufuli anatulisha matango pori, toka mwaka 1999 alikuwa anaunga mkono uuzwaji wa migodi, hicho kishika uchumba Accacia wako mahakamani

Udhaifu wa Magufuli ulianza baada ya kula rambi rambi za tetemeko kagera .. ..

Hawezi kufanikisha chochote laana na mikosi juu ya manung'uniko ya watu waliopata janga lile atobaki salama...

Kwanza kwa wale wanaenda mgodini arusha watanielewa2 jinsi madini yanavyotoroshwa sasa hv.........

Yaani yanatoroshwa kwa mbwembwe na escort juu tena adi ambulance wanatumia..

Hii maana yake alitupa hasara kujenga ukuta....

Ukiongea unaambiwa sio mzalendo....

Sasa tuliambiwa trion400 sasa ni bilion600 halafu tunashangilia........


Elimu + Shule ni muhimu kwa watanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anaandika #Tundu_Lissu

21.02.2019

'Nateseka' na hili suala kwa sababu 'nimeteseka' nalo toka mwaka 1999, wakati Magufuli 'akiunga mkono' juhudi za Rais Mkapa za kuuza utajiri wetu kwa wageni. Huu ni mwaka wangu wa 20 'nateseka' nalo na nitaendelea kuteseka nalo as long as nina pumzi.

Mnadanganywa na tunadanganywa na Magufuli na watu wake. Alipokuja President John Thornton mwaka jana, tuliambiwa Barrick watalipa 'kishika uchumba' (á la Prof. Kabudi) cha dola 300m.

Hawakulipa. Kwa nini??? Kwa sababu Acacia Mining walikataa. Badala yake walitufungulia kesi ya kuvunja mikataba yao ICSID, wanakotudai mabilioni ya dola.

Sasa amekuja President Willem Jacobs. Naye amesema Barrick watalipa 'kifuta machozi' cha dola 300m, lakini mpaka kwanza 'independent board of directors' ya Acacia Mining wakubali. Hao hao waliokataa kulipa mwaka jana wanatakiwa wakubali kulipa sasa.

Halafu kwenye press release yao iliyotolewa jana hiyo hiyo, Barrick wanasema ahadi zao hizo kwa Magufuli ni 'forward looking statements' ambazo, kwa kifupi, sio makubaliano yoyote yenye nguvu za kisheria. Hawafungwi na chochote walichokisema kwenye makubaliano yao na Serikali ya Tanzania.

Ndio maana nimesema someni hiyo disclaimer vizuri. Wazungu hawa sio wajinga. Wanasema hizo 'forward looking statements' zao zinaweza kuathiriwa na kesi au mashauri yanayoendelea mahakamani. Maana yake ni nini??? Wakitushinda kwenye kesi waliyotufungulia ICSID hawatatulipa.

Wanasema hizo 'forward looking statements' zao zinaweza kuathiriwa na faida au hasara katika uwekezaji wao. Maana yake ni nini??? Wakipata hasara hawatatulipa.

Sheria ya sasa ya Madini inasema mkataba wowote unaohusu madini unatakiwa kuwasilishwa Bungeni. Kama hawatulishi matango pori watayawasilisha makubaliano haya bungeni. Wasipoyawasilisha ujue ni matango pori.
Hongera Lisu kama sasa umeanza kujua kuwa wazungu sio watu wazuri kwetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lissu anasema wazungu sio wajinga alafu na yeye ndo yupo uko uko anawalilia shida zake pumbavu zake.
Aje sasa alirarue bunge kwa izo hoja zake sio kuongelea chooni.
Kiki zimeanza kupungua mvuto unaisha. Ivi intaviuz zimeisha cku izi au mbona kmyaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu baba anahangaika na Magufuli duuh, angekuwa mwanamke tungesema alitemwa angali pado anapenda. Kweli JPM amejua kumnyima usingizi, badala ya kuwaza matibabu, pango,ada, malazi yeye 24/7 Magufuli. Nahisi hata wife akishindwa kupafomu atadai Magufuli. Shit!
 
Back
Top Bottom