Lissu kuhutubia Bunge la Marekani mwezi April 2019, atakuwa mbunge wa Kwanza mtanzania kuhutubia Congress ya Marekani

Farijianeni kwa maneno hayo - muongee kimya kimya kwa kuwa baba yenu CCM atawasikia

Hata akihutubia shirikisho gani bado mpigwe tu kwenye uchaguzi mkuu ujao
 
Hata angeenda baraza la mawaziri la marekani na hata akiitwa white house na trump bado hana impact yeyote ile kwa sovereignity country kama tanzania

wataishia kumsikiliza na kumsindikiza airport arudi zake ubelgiji kwa matibabu zaid na story itaishia hapo kama mwenzie maalim seif.
Mdharau mwiba mguu huota tende. Angalia shilingi inavyoporomoka, hiyo Ni moja ya impact kubwa sana, uchumi unaanguka halafu wajinga wanasema Hakuna impact!!! Kwa akili ndogo wanadhani 20 za Machinga zitaendesha nchi!
 
Kabisa na haitakaa itokeee
Lakini cha ajabu Waafrika bado tunaishi kwenye ndoto za kudhani kwamba wanamsaada kwetu
Ndo maana kila shida ama changamoto zinapojitokeza kwenye nchi zetu bado wapo wanaodhani kwamba suruhisho na migogoro yetu ni kwenda kwa Wazungu
Mbaya sana hii

Sent using Jamii Forums mobile app
CCM hawajawahi na hawatawahi kuwa suluhisho afadhali wazungu wanatuletea hata ARVs

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ikitokea ikawa hivyo, hili litakuwa ni tukio la kipekee kabisa , kama ilivyokuwa kwa tukio la mtu kuchakazwa risasi zaidi ya kumi na kuendelea kudunda.

Lakini hasa upekee utakuwa ni juu ya Tanzania kuwekewa umhimu wa namna hiyo. Nadhani hasa kichocheo kitakuwa ni jinsi watawala wanavyozidi kuchochea kuminywa kwa haki kwa wananchi wao. Na hili linategemewa kuongezeka kadri uchaguzi mkuu unavyosogelea.

Hata kama hapatasemwa chochote baada ya tukio hilo kama kweli litakuwepo, taa ya njano itakuwa imeiangaza Tanzania yetu dunia nzima.

Kama ingetokea safari hiyo ikawepo na kupewa heshima ya namna ya pekee hiyo kuwahi kutokea, jambo la kuombea lingekuwa moja tu. Wananchi wa Tanzania wasaidiwe kuwachagua viongozi wao bila ya kushawishiwa na mtu yeyote wa nje, na bila kuwepo mizengwe ya chama kimoja kujitwalia madaraka ya kuendesha uchaguzi huo.

Wakiweza kutusaidia kwa hili, watakuwa wamefanya jambo jema sana.

Hata akiweza kuongea na Kamati tu ya Cngress, na isiwe Congress nzima, ingetosha kabisa kuchukua heshima kubwa.
Hiyo heshima kubwa itampatia urais? Itakusaidia nn ww zaidi sana atawaomba watunyime misaada, ndugu zako kule kijijini wapate tabu.
Haya mambo mnayaangalia juu juu sana, mnaona wazungu miungu watu kwamba kuhutubia kwao ni heshima kuubwa.
Mnasikitisha sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata angeenda baraza la mawaziri la marekani na hata akiitwa white house na trump bado hana impact yeyote ile kwa sovereignity country kama tanzania

wataishia kumsikiliza na kumsindikiza airport arudi zake ubelgiji kwa matibabu zaid na story itaishia hapo kama mwenzie maalim seif.

Shillingi imeshuka kwa sababu ya misaada kusitishwa (BOT wamesema), misaada imesitishwa kwa sababu ya mambo ya uhuru wa kisiasa (EU wametoa maazimio).

sasa utasemaje ya Lissu hayana impact kwa nchi hii?

uko kwenye denial, au huna ufahamu wa lolote linaloendelea nchini, unajiongelea tu
 
Marekani haina Bunge.
#Mpya

MH. TUNDU LISSU KUONGEA NA CONGRESS MAREKANI.

Mh. Tundu Antipas Mwigwai Lissu anatarajiwa kurudi United States of America kuongea na Bunge la Marekani mwezi wa nne mwaka huu.

Akiongea kutokea ofisi zake za Bunge Washington DC leo Ijumaa asubuhi Rep. Christopher Smith- New Jersey amesema Mh. Lissu atapata nafasi ya kulieleza Bunge la Marekani changamoto za Demokrasia Tanzania.

Zaidi, Rep. Smith ameseam Mh. Lissu atatumia muda huo kulieleza Bunge la Marekanai mkasa wote wa tukio la kupigwa risasi kumi na sita.

Mh. Lissu anatarajiwa kurudi USA wiki ya pili ya mwezi wa nne.View attachment 1035689
 
Lissu The Greatest
 
Good for him, hilo linatikea wakati wowote, na umedanganya kuwa Lissu atakuwa mbunge wa kwanza wa Tanzania kufanya hivyo. 1978 - 79 kulikuwa na mbunge wa kitanzania alialikwa na ajazungumza hapo congress, huyo mbunge alialikwa na congressman aliyesima nae chuoni usa.

Nitajaribu kulikumbuka jina na natalileta hapa. Pia 1999 wabunge wawili wa Somaliland nchi ambayo haijatambuliwa , walipewa fursa ya ku,ungumza na congress kwa kulihutubia baraza la Congress.

Hiyo fursa hupewa kina mwana congress, anaweza mkaribisha hata shetani, bira atimize masharti na muda uwe muafaka.

Sent using Jamii Forums mobile app

Huo mwaka 1978-79 nusu ya watanzania walikuwa hawajazaliwa.
 
Back
Top Bottom