Lissu anafikiri siasa ni sheria tu

Lissu anafikiri siasa ni sheria tu

kmbwembwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
10,931
Reaction score
7,828
Mwanasheria Lissu anafikiri siasa ni sheria tu. Anataka kutuaminisha haki ni sawa na sheria. Lengo la kuwepo sheria ni ili kuwepo utawala wa haki. Ili kupata haki kunapotokea mtu kuvunja sheria kunakuepo wanasheria kutafsiri sheria.

Haki ni sawa na kweli, ipo tu. Uanasheria ni taaluma ya kutafsiri sheria ili kujua haki au kweli iko wapi. Kwa bahati mbaya taaluma hiyo hutumika pia kudhulumu haki na kweli. Wapo wanasheria hugeuza kweli kuwa uongo na kupora haki ya mtu. Mara nyingi ni kutokana na rushwa au kumpa haki asiyostahili mteja wao. Kuna watu wachache kutokana na uwezo wao wa kuhonga wanapora haki ya wasiokua na uwezo wa kuhonga.

Kwa hiyo siasa sio sheria tu ila inahusu pia kupambana na dhuluma. Lissu anafikiri kuwaacha watu dhulumati kuishi na mali ya dhuluma ni utawala wa sheria na hasa kama mali iliyodhulumiwa ni ya umma. Anataka watu wenye tuhuma za kudhulumu mali ya umma waachiwe toka gerezani kwa kua uchunguzi wa kesi zao unachukua muda mrefu.

Anataka tusiwaite mabeberu kwa jina lao beberu kwa kua eti wanatufadhili wakati wa njaa na kutukopesha hela. Kwakua eti vitu tunavyotumia vinatengenezwa na wao. Anataka tuwasujudie wazungu. Hivyo ndio vipaumbele vya Lissu.
 
Huko upande wa pili wakisikia jina la Lissu nguo zina wapwelepweta.
 
Lissu anafikiri kuwaacha watu dhulumati kuishi na mali ya dhuluma ni utawala wa sheria na hasa kama mali iliyodhulumiwa ni ya umma. Anataka watu wenye tuhuma za kudhulumu mali ya umma waachiwe toka gerezani kwa kua uchunguzi wa kesi zao
Tunajuaje kuwa huyu amedhulumu? Kuna vigezo tulivyojiwekea vya kuamua kuwa huyu ni dhulumati au la! Kama vigezo hivyo hujavifikia, basi wewe hujadhulumu! We do not entatain guess work on deciding who is a thief! Vigezo hivyo ni SHERIA ZETU! DHANA HAIPATANI NA UKWELI, UNATAKA TUTUMIE DHANA KUAMUA NANI AMEDHULUMU? NO!
 
Sisi watu masikini ni wapumbavu sana huwa tuna omba tajiri afilisiki tuwe sawa badala ya kuomba upande kama yeye. Waafrica tuna laana haswa, tajiri akifilisika wewe utakosa ajira, hutauza mazao yako, huwezi kupata huduma za msingi n.k
 
Tunajuaje kuwa huyu amedhulumu? Kuna vigezo tulivyojiwekea vya kuamua kuwa huyu ni dhulumati au la! Kama vigezo hivyo hujavifikia, basi wewe hujadhulumu! We do not entatain guess work on deciding who is a thief! Vigezo hivyo ni SHERIA ZETU! DHANA HAIPATANI NA UKWELI, UNATAKA TUTUMIE DHANA KUAMUA NANI AMEDHULUMU? NO!
Mkuu ni visasi vya kijinga sana kuamini kila tajiri amedhulumu mali unaanza kumtesa kisa una dola, mpeleke mahakamani na mahakama iamue.
 
kmbwembwe,

Kwahiyo wewe kwa uelewa wako, Unataka watu wawachukie wazungu kwa sababu gani wakati ndio waliokusomeshemi ndio walikutoa tongo tongo.
 
kmbwembwe,
Raisi mzuri duniani utokana na fani ya sheria, diplomasia, biashara au uchumi nje ya hapo huwa ni waborongaji tafiti
 
kmbwembwe,

Mliosoma syllabus za zamani mlipandikizwa chuki za kuwachukia wazungu na watawala wa kiafrica baada ya kushindwa kuwaletea waafrika maendeleo,sisi si kisiwa tuwe na maendeleo bila kushirikiana na wengine.

Ishu sio kukaa ndani tatizo wasio na chapa ndo ukaa ndani wengine dabo standard.

Raisi mzuri duniani utokana na fani ya sheria, diplomasia, biashara au uchumi nje ya hapo huwa ni waborongaji tafiti
 
Back
Top Bottom