Lisemwalo lipo . | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lisemwalo lipo .

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Babylon, Mar 11, 2010.

 1. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2010
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Warioba, Maalim Seif waibua utata

  [​IMG]
  Mwandishi Wetu​
  Machi 10, 2010 [​IMG]
  UTATA umegubika afya za wanasiasa wawili wenye nguvu nchini, Waziri Mkuu na Makamu wa Rais mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad ukihusishwa na mikakati ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
  Wanasiasa hao wanaotajwa kuwa na nguvu kubwa ya kisiasa na ambao kwa namna moja ama nyingine wanahofiwa kuwa na majibu katika mwelekeo wa kisiasa nchini, wameibua mjadala, na zaidi umehusu taarifa zisizo sahihi ambazo baadhi zimetokea serikalini na nyingine zikiwa hazifahamiki chanzo chake zilizoenea kwa kasi.
  [​IMG]

  Waziri Mkuu mstaafu, Joseph Warioba
  Jaji Warioba ambaye kwa sasa yuko na mkewe nchini Afrika Kusini, wakifanyiwa uchunguzi wa kawaida wa afya, hali yake haitatanishi na wala hakwenda nchini humo kwa dharura kama ilivyoelezwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa, aliyesema kwamba alipelekwa baada ya kubainika alihitaji uangalizi wa haraka.
  Akizungumza na Raia Mwema, kutoka Afrika Kusini, Jaji Warioba alisema kwamba yu mzima, kwamba madaktari walikuwa wakifanya uchunguzi wao na kwamba kabla ya kwenda huko alipatwa na kwikwi ambayo ilidhibitiwa kabla ya safari hiyo.
  Profesa Mwakyusa alinukuliwa na gazeti moja wiki iliyopita akisema kwamba Warioba amepelekwa nchini Afrika Kusini kutibiwa baada ya kulalamikia maumivu ambayo yalihitaji uchunguzi wa haraka akisema;
  "Kusema ni kwa ajili ya kumfanyia check up (kumpima) si sahihi; mpango uliokuwapo ulikuwa ni kumpeleka Afrika Kusini kwa ajili ya investigation (uchunguzi) baada ya kulalamika kuhusu maumivu mwilini mwake."
  Kauli hiyo ya serikali pamoja na taarifa za awali za ugonjwa wake kuenea kwa kasi zimewashitua yeye mwenyewe na walio karibu naye kwa kuwa kimsingi hakukuwa na tishio kwa afya yake.
  Jana Jumanne katika mazungumzo ya simu, Warioba aliiambia Raia Mwema kwamba afya yake ni imara na kwamba alikuwa anasubiri taarifa ya uchunguzi wa madaktari.
  Kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu Novemba 5, 1985 na Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, mwanasiasa huyo aliyezaliwa Septemba 3, 1940 alipata kushika nyadhifa mbalimbali kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Waziri wa Sheria.
  Alikuwa Waziri Mkuu hadi Novemba 9, 1990 wakati Mwinyi alipovunja baraza la mawaziri na nafasi yake ikachukuliwa na John Samuel Malecela na yeye akateuliwa kuwa Waziri wa Nchi Tawala wa Mikoa na Serikali za Mitaa. Januari 17, 1996 wakati wa Serikali ya Rais wa Awamu ya Tatu, Jaji Warioba aliteuliwa na rais wa wakati huo, Benjamin Mkapa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Kuchunguza Mianya ya Rushwa, ambayo ripoti yake ilimjengea umaarufu na heshima kubwa katika jamii.
  [​IMG]

  Maalim Seif
  Wakati hayo yakijiri, Maalim Seif mwishoni mwa wiki iliyopita alipatwa na mshituko na akalazwa katika hospitali ya Hindu Mandal iliyopo katikati ya jiji la Dar es Salaam, kabla ya kuibuka kwa uvumi wa kwamba mwanasiasa huyo amefariki dunia, taarifa ambazo pia hazikufahamika chanzo chake.
  Kuugua kwa Maalim Seif kuliibua hofu zaidi kutokana na kuwa mmoja wa watu muhimu katika siasa za Zanzibar kwa sasa aliyebadilika kwa haraka kwa kuanza kumuunga mkono mpinzani wake mkubwa, Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume.
  Hadi jana, hali ya afya ya Maalim Seif ilielezwa kuimarika pamoja na kuwa alianza kulalamika maumivu ya kifua, tatizo ambalo hakuwa nalo awali. Alifikishwa hospitalini hapo kwa tatizo la shinikizo la damu, ambalo amekiri kuwa nalo muda mrefu.
  Maalim Seif, aliugua ghafla wakati akijiandaa kupanda ndege kwenda Mascut, Oman, Ijumaa wiki iliyopita katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam na kukatisha safari hiyo.
  Kabla ya kuingia Upinzani, Maalim Seif amewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwa ni pamoja na kuwa Waziri Kiongozi wa Zanzibar, na amekuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa katika siasa za Visiwani.
  Aligombea urais katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995 ambako alishindwa na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Dk. Salimin Amour, kabla ya kushindwa tena mara mbili na Karume, mwaka 2000 na mwaka 2005, na mara zote Seif na chama chake wamekuwa wakielezea kutoridhishwa na matokeo wakilalamikia ukiukwaji wa taratibu.
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Mar 11, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,890
  Trophy Points: 280
  "Wanasiasa hao wanaotajwa kuwa na nguvu kubwa ya kisiasa na ambao kwa namna moja ama nyingine wanahofiwa kuwa na majibu katika mwelekeo wa kisiasa nchini"

  Seif ana majibu, Warioba hana hata moja

  Seif is the man! kafanya mambo ya kihistoria uko visiwani.

  Warioba kama wana CCM wengine wengi (kama si wote) anaingia kwenye godown la mafisadi wenye sura ya kondoo ambao kwao CCM ni mama na baba wa hatima ya maisha yao!

  Seif ana majibu lakini Warioba hana majibu, ila nawatakia afya njema!  Anyway, poleni jamani mtapona! tunawaombea
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Waberoya,
  What a comment! Yaani kwa sababu Warioba bado yuko CCM anaingia kwenye godown la mafisadi ilhali tunawafahamu mafisadi ni akina nani? What a comment!
   
 4. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #4
  Mar 11, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135


  Nahisi mwandishi hakuwa sahihi kumpa Warioba koti lisilomstahiki. Kwa kipindi sasa Warioba amekuwa haeleweki na hakuna impact yoyote anayoleta kwa matamshi yake ya kitatanishi.
  Ama kwa Seif pengine kwa vile ni kiongozi wa Chama chenye nguvu angalau anaweza akaleta impact kwenye mustakabali wa Taifa.
   
 5. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #5
  Mar 12, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  Hebu wajamani tukumbushane kwa walio na kumbukumbu ya herufi zile alizozitabiri mnajimu sheikh Y. Zinaanza je?
  WE ARE PRAYING FOR YOU AND WISHES U GET WELL SOON DEAR MAALIM AND JOSEPH.
   
 6. D

  Donrich Senior Member

  #6
  Mar 12, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  i dont believe on Shekh Yahya,it was political propaganda..
   
Loading...