Lipumba awavaa viongozi CHADEMA

Nilimuheshimu sana Prof. na kuamini kwamba uprofesa wake haukuwa wa kubumba. Lakini kama sasa hivi kaishiwa mpaka anaanza kuimba sifa za ccm na kuanza kuina cdm kama adui wa cuf, uh, naogopa kama huku ndo kuzeeka, basi bora tufe tukiwa vijana na akili zilizonyooka kuliko kuliko kufikia uzee na kuzeeka vibaya kama Lipumba.
 
Mtamaliza matusi ote lakini Prof Ni msomi aliyebobea kwenye uchumi na ana uzoefu mkubwa sana na siasa za tanzania.

Ukweli unaumaaaaaa eheeeeeeee, badilikeni muwe na uso wa kitaifa sio ukanda, ukabila na udini.

Hafif, siku hizi CUF wamebadilika na kuwa Chama cha Kitaifa badala ya Chama cha Kidini na Wapemba? Umenyweshwa mvinyo na ndoa ya mkeka ya CUF na CCM ukalewa. Ama kweli madaraka matamu.

KUMBUKA TUNDU LISU ALISEMA: SHERIA ZA TANZANIA ZINATAMBUA NDOA YA WAKE WENGI, LAKINI HAZITAMBUI NDOA YA WAUME WENGI.
 
Kisha cdm walifanya press na kueleza kuwa cuf ni ccm b halafu cdm wakaanza maandamano kanda ya ziwa,katika kila hotuba walikuwa wakiiponda cuf kuliko hata ccm,sasa mimi kitu ambacho sielewi wanajamvi wanakitafuta ni juu ya nini cuf ifanye? Mimi nadhani cuf wako sahihi kujibu mashambulizi ya cdm, cdm waendelee kuwaita cuf kuwa ni ccm b na cuf watueleze kwa nini wao sio ccm b na watueleze ccm b ni nani, nadhani tuwaache cuf wajibu waliyopakwa..
 
Anatumiwa na CCM kweli moto wa CDM unatisha.
 
Huyu naye ndumilakuwili juzi katoka kumkashifu mkulu leo Chadema hizi njaa zitawauwa. Yaani Prof.mzima anadiriki kuongea kama mtoto mdogo akipewa peremende basi atakupamba kwa kila namna. Kila siku anaimba CUF CUF amekaa Dar es Salaam wakati wenzie wanatembea huku na huko kujua hali halisi ya maisha ya mtanzania. Udini utakumaliza mzee wangu. Fanya lililo jema kwa nchi yako na watanzania kwa ujumla bila kujali dini utafanikiwa lakini kwa mtindo wako huo utaishia kuimba imba tu.
 
kaka worry not wacha huyu educated fool aendelee kuiponda CDM, kwa kufanya hivyo ainakiongezea CHADEMA credit. huyu Prof Ubwabwa anatakiwa akisaidie kijiji chake kisicho na maendeleo ndo aje kuisaidia Tanzania as charity begins at home. tatizo la vijamaa kama wazee wa Gahawa ni njaa alafu wanapenda kufichiana UOZO.
 
lakini hapa tunajadili nin? kwa sbb cdm ndo walilianzisha tuwaache wenzao wajibu, nasi tusiwe mbele kutaka cdm iwe malaika tu, kwenye mikutano yote ya cdm kanda ya ziwa walikuwa wakiwaponda cuf nadhan wana haki ya kujibu kila kitu walichoguswa and to me i think they are bringing a big challenge to cdm lakin wakikaa kimya watajimaliza,
Bette the one who speak out.
 
ahahahha amegusa pabaya kichizi nampa pole mzee wetu huyu cha zaidi aende tabora ajiandalie mahali pakupumzikia siku si nyingi atahitajika kupumzika na wajukuu wakmchezea na kulushiana mpira na wajukuu zake kwa sababu kwisha habari yake pia ajiandae kukabidhi uenyekiti kwa mtu atakaye ondoa udini kwenye chama chake ili kiweze kupata wanachama wa aina tofauti
 
Yaliyopita si ndwele,tunaganga yajayo.
Kuna kipindi kulikuwa na tofauti na kutiliana shaka.
Sasa vyama vyetu vimekubaliana kuwa kuna kipindi walipotoka,wamejifunza na hawapotoki wala kugombanishwa tena.
Go go UKAWA
 
Hapa ndio watu wanatakiwa wajifunze rangi halisi ya hivi vyama
 
Hii Hotuba ya Lini? toa link kwanza kabla watu hawajachangia..
 
Makamanda wenzangu tusipanic hivi ni chanzo gani cha hiyo habari?
Je ni kweli hayo yamesemwa na Prof lipumba? Mimi sitaki kuamini hadi niaminishwe kwanza chanxo cha hii habari! Kwani hii habari ni ya lini?
Isije ikawa ni habari ya enzi hizo wakati ws ujima wakati vyama havijatambua adui yao ni yupi!
Enzi hizi za ukawa hayo hayawezi kuwa maneno ya Lipumba hata kidogo
 
Makamanda wenzangu tusipanic hivi ni chanzo gani cha hiyo habari?
Je ni kweli hayo yamesemwa na Prof lipumba? Mimi sitaki kuamini hadi niaminishwe kwanza chanxo cha hii habari!
Umeona jinsi watu wenu wanavyokurupuka? ndio ujue nini hasa kipo moyoni mwao yaani kuwavuruga UKAWA rahisi sana. Mimi nimeisoma hii tu nikasema haiwezekani mleta mada atupe link maana najua maneno haya Lipumba kayasema zamani sana kama sii uchaguzi wa 2005..
 
Makamanda wenzangu tusipanic hivi ni chanzo gani cha hiyo habari?
Je ni kweli hayo yamesemwa na Prof lipumba? Mimi sitaki kuamini hadi niaminishwe kwanza chanxo cha hii habari!
Uzi wa enzi hizo za utengano mwaka 2011
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…