Lipumba awavaa viongozi CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lipumba awavaa viongozi CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 23, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Na Benedict Kaguo, Pangani

  MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba amesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hakina nia thabiti ya kupambana na ufisadi kutokana kuchochea mgawanyiko wa Watanzania.


  Alisema chama chochote cha siasa kilichoshindwa kuthamini matakwa ya wananchi wake hakina nia ya dhati ya kuwaletea ukombozi wa kweli wanaouhitaji Watanzania kwa sasa.


  Profesa Lipumba alitoa kauli hiyo wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika mji wa Pangani katika mwendelezo wa mikutano ya chama hicho 'kuwazindua Watanzania katika kujenga demokrasia ya kweli hapa nchi'.


  Alisema wafanyabiashara wa Chadema hawawezi kuongoza mapambano dhidi ya ufisadi kwa kuwa tayari wako katika mazingira ya kukumbatia rushwa, hivyo ni vigumu wao kuongoza mapambano hayo kama wanavyodai.


  "Ndugu zangu wafanyabiashara na wapiga disko wa Chadema wanataka kuwang'oa mapapa ya ufisadi wa CCM ili wao manyangumi ya ufisadi waweze kuingia madarakani, hawana nia thabiti ya kupambana na rushwa," alisema Profesa Lipumba.


  Alisema aliingia kwenye siasa kwa lengo la kuwasaidia Watanzania sio kutafuta sifa kama walivyo baadhi ya wanasiasa wa Chadema.


  "Sikuingia kwenye siasa kutafuta sifa, nimeingia kutumia elimu yangu kuwatafutia ukombozi Watanzania wenzangu, sasa hawa Chadema hawawezi kuiondoa CCM kwa kuwa wanachochea mgawanyiko mkubwa ndani ya nchi kwa kuwatukana Wanzanzibari waliokubali Serikali ya Umoja wa Kitaifa," alisema Profesa Lipumba.


  Awali, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Bw. Julius Mtatiro alisema taifa linaangamia kwa kukosekana uongozi ulio madhubuti sasa ni wakati wa Watanzania kuzinduka ili uchaguzi mkuu ujao waweze kukipa ridhaa chama makini cha CUF.


  "Maisha yamekuwa ya kubabaisha huduma za afya hospitalini mama zangu mnatakiwa mwende na nyembe mnapotaka kujifungua, serikali inashindwa kununua wembe lakini wakati wa uchaguzi inaweza kununua kitenge kwa kila mwanamke Tanzania nzima," alisema Bw. Mtatiro.


  Alisema wakati wa mabadiliko ndio huu na wananchi hawana budi kukiunga mkono chama hicho ili kiweze kuongoza mapambano dhidi ya rushwa, matumizi mabaya ya fedha za umma ili kuwakomboa wananchi.
   
 2. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,701
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  dah! Kweli siasa mchezo mchafu ni kuharibiana kwa kwenda mbele,kumbe ufisadi hautoisha?
   
 3. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2011
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Prof. Uchwara, with his education what did he do during his tenure as President Mwinyi advisor? au kunywa gahawa tu na majungu, mtu wa majungu utamuona tu, whom does he fight? Deep Green au CDM?
   
 4. Kiherehere

  Kiherehere JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Hawa ndio wanakazania tuunde nao baraza kivuli... kweli hii nchi kila mtu kamuoa mwenzie ....
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  So suddenly Chadema is the enemy. Naona rafiki yangu profesa kachanganyikiwa.
   
 6. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Hawa CUF sio watu kabisa..,....Hawa jamaa hawafai kabisa na inabidi CHADEMA wakae nao mbali kabisa maana hawana mpango........Vigeu geu kama watoto
   
 7. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Wakti siku zote hutoa nafasi ya kujua nani yuko upande gani.

  Hebu fikiria chama fulani cha upinzani kingepata ushindi mika 5 iliyopita unategemea kungekuwa na mabadiriko ya maana kama mtu na PhD yake ana upeo finyu namna hii wa kujenga chama chake kwa kukumbatia Chama tawala kilichoshindwa??

  Wakati siku zote hufichua watu waovu wenye hila nia mbaya ya kuendelea kutweza Watanzania makali ya maisha.

  Yaani huyu Senior Bachelor Muhuni asiye na mke anaongea kama kaahidiwa demu bomba na CCM??

  Kutumia muda mwingi Kushambulia chama cha CDM wakati Uovu wote Tanzania unafanywa na Serikali ya CCM inasaidia vipi kuwapa mwamko wananchi wa Tanzania?

  CUF inapambana na CDM ili kutwaa madaraka yapi wakati CDM iko bench kama wao?? Au inapambana na CCM huku ikipinga yenyewe binafsi kama chama kwani ina hisa za ndani kwa ndani huko CCM??

  Lakini hata hivyo CUF ime sign mkataba wa kiuchumi na kisiasa na chama cha CCM kwa kipindi cha miaka 5, CUF kuwashambulia CCM ni sawa na kuishambulia CUF yenyewe. Kwa vile ni lazima wanasiasa wa CUF kukishambulia chama fulani wakati wa mikutano ya kisiasa ili kuvuta hisia za wananchi kisiasa, CUF wanaona ni vema kukishambulia CDM ili kupoza hasira ya kukataliwa ndoa ya wake wawili.
   
 8. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Kwanini Chama Cha CCM wasimpe Cheo Chochote? Sababu Viongozi wenzake wote Wazanzibari wana Vyeo Serikalini

  He feels out and isolated why not him???
   
 9. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #9
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Ukimtumikia kafiri hachelewi kukugeuza Yandani.

   
 10. m

  maselef JF-Expert Member

  #10
  Mar 23, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hayo ndo matatizo ya ndoa ya mkeka kati ya CCM na CUF
   
 11. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #11
  Mar 23, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Eleleeleeeeeeeeee iiiiiiiiiiiiiiiiii uuuuuuuuuuuuuuuuuu walisema aolewi mbona kaolewa hiiiiiiiiiii
  wenye wivu wajinyonge uuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
  mbola aolewa awoooooooooo
  atakama muoaji ni sho, aijalishiiiiiiiiiiiiiii mbona kaolewa uuuuuuuuwiiiiiiiiii
  MKE ALAZIMA AMTETEE MME WAKE hili apate chakula
   
 12. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #12
  Mar 23, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Nina wasi wasi na Phd yake, sidhani kama anastahili kuitwa associate professor, sasa tumegundua kumbe siyo CCM tu ndiyo adui wa waTanzania ni pamoja na na hivi vyama vya ovyo ovyo kama CUF
   
 13. m

  mozze Senior Member

  #13
  Mar 23, 2011
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 185
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  well, Ushauri wngu kwa CHADEMA, msithubutu hata kidogo kujibu hoja za CUF, mkitaka wajione wajinga na wasiojua kitu kaeni Kimya msijaribu kusema anything. Huo ni mtego, CUF inaonekana imekuwa taasisi ya CCM kama zilivyo UVCCM, BAKWATA, etc wao wanafuata kuhimiza yale aliyosema Kikwete.

  Ukijibizana na kichaa na wewe utaonekana Kichaa! Please Be careful
   
 14. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #14
  Mar 23, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 916
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35

  Hii sasa imetulia, yaani hahitaji hata cheti cha VETA kujua kama mwenyekiti wa CUF huenda na CUF yenyewe ni chama cha kisiasa chenye lengo la kumkomboa Mtanzania kutoka kwenye makucha ya mafisadi -CCM. Labda kama tutapewa ushahidi wa kauli anazozitoa huyu m/kiti wa CUF. Akiwa miongoni wa wasomi, ingependeza umwage ushahidi adharani na siyo kuongea kama m-uuza gahawa. Wenzio walipotoa orodha ya mafisadi walikuwa na takwimu to the last dot; wewe Prof unatoa vibwagizo vya taarabu.

  Mti wenye maembe lazima upigwe mawe; hilo ndilo linalotokea hivi sasa Tz; nchi inaelekea kana kwamba inaongozwa na CDM indirectly; na kila chama kinang'ang'ana kutafuta kukiondoa CDM ktk nafasi kilichomo. Kaaaazi kweli kweli; na sinema inazidi kunoga.
   
 15. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #15
  Mar 23, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Naona huu ni mpango ambao umesukwa kwa kushirikisha CCM na washirika wake hususani CUF. Kutokana na CCM na Serikali yake kusakamwa sana na CDM, wanaona wakibishana nao ndiyo wanazidi kujiharibia kwani kila mtu ndani ya CCM na serikalini anakuja na matamko tofauti jambo ambalo linatokana na makundi yaliyopo CCM. Mbinu mpya ni kutumia washirika wake kama CUF kurusha mashambulizi kwa CDM ili CCM ipumue.

  Mtego ni kwa CDM kuanza kujibishana na CUF,jambo ambalo CDM hawapaswi kulifanya kwa sasa, CDM walishawamaliza CUF siku nyingi, kwanza kuwapoka nafasi ya upinzani mkuu, pili kufanikiwa kuonesha taswira halisi ya CUF kuwa ni CCM-B na tatu kutowashirikisha katika baraza kivuli la mawaziri.
   
 16. E

  ESAM JF-Expert Member

  #16
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 962
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Please CHADEMA leadership,

  "Don't argue with the fool because people may not notice the difference between you and the fool."

  Get blessed.
   
 17. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #17
  Mar 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mom, I remember your words, I will live them; you said,

  'in life don't talk bad about the dead and the stupid...'

  I will keep quite.
   
 18. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #18
  Mar 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mtatiro, je Zanzibar kina mama hawaendi hospitali na viwembe? Ni bara peke yake? Huo uozo wa CCM upo upande mmoja tu wa nchi hii? Anayedharau hapa ni nani?
   
 19. Naloli

  Naloli JF-Expert Member

  #19
  Mar 23, 2011
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 416
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  PROF. LIPUMBA Kapoteza muelekeo kabisa wa kisiasa na kiuongozi, Kweli usipofikia malengo ya kisiasa unapagawa na kuchanganyikiwa kweli leo CDM wamekuwa mafisadi NYANGUMI na CCM ndio mafisadi PAPA? Hata kama mimi sio Prof. huyo Prof wa CUF kachemsha na ana wivu wa chama chake kupoteza muelekeo na nafasi yake kuchukuliwa na CDM. Ila wakumbuke wananchi ndio waamuzi na wanajua chama gani makini kwa sasa. Kujiunga na ccm ktk serikali na kuwa kitu kimoja Bungeni.
   
 20. M

  Mzalendoo Member

  #20
  Mar 23, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Teh teh teh,ebwana huyo ndo prof mapumba,mlikuwa hamumjui?
   
Loading...