Lipumba awavaa viongozi CHADEMA

Lipumba awavaa viongozi CHADEMA

Ni kweli, lakini ninachojifunza hapa ni kwamba watu wamechoshwa sana na mfumo dhalimu wa utawala uliopo, na UKAWA ndo suluhisho kwa serikali dhalimubya CCM, ndio maana yeyote au chochote chenye kutia mashaka au kutishia mparanganyiko wa UKAWa hakiwezi kufumbiwa macho kama ulivyoona
 
Weka source vinginevyo wewe ni mgombanishi tu. mods ondoeni huu uchonganishi
 
Na Benedict Kaguo, Pangani

MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba amesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hakina nia thabiti ya kupambana na ufisadi kutokana kuchochea mgawanyiko wa Watanzania.


Alisema chama chochote cha siasa kilichoshindwa kuthamini matakwa ya wananchi wake hakina nia ya dhati ya kuwaletea ukombozi wa kweli wanaouhitaji Watanzania kwa sasa.


Profesa Lipumba alitoa kauli hiyo wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika mji wa Pangani katika mwendelezo wa mikutano ya chama hicho 'kuwazindua Watanzania katika kujenga demokrasia ya kweli hapa nchi'.


Alisema wafanyabiashara wa Chadema hawawezi kuongoza mapambano dhidi ya ufisadi kwa kuwa tayari wako katika mazingira ya kukumbatia rushwa, hivyo ni vigumu wao kuongoza mapambano hayo kama wanavyodai.


“Ndugu zangu wafanyabiashara na wapiga disko wa Chadema wanataka kuwang'oa mapapa ya ufisadi wa CCM ili wao manyangumi ya ufisadi waweze kuingia madarakani, hawana nia thabiti ya kupambana na rushwa,” alisema Profesa Lipumba.


Alisema aliingia kwenye siasa kwa lengo la kuwasaidia Watanzania sio kutafuta sifa kama walivyo baadhi ya wanasiasa wa Chadema.


"Sikuingia kwenye siasa kutafuta sifa, nimeingia kutumia elimu yangu kuwatafutia ukombozi Watanzania wenzangu, sasa hawa Chadema hawawezi kuiondoa CCM kwa kuwa wanachochea mgawanyiko mkubwa ndani ya nchi kwa kuwatukana Wanzanzibari waliokubali Serikali ya Umoja wa Kitaifa,” alisema Profesa Lipumba.


Awali, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Bw. Julius Mtatiro alisema taifa linaangamia kwa kukosekana uongozi ulio madhubuti sasa ni wakati wa Watanzania kuzinduka ili uchaguzi mkuu ujao waweze kukipa ridhaa chama makini cha CUF.


“Maisha yamekuwa ya kubabaisha huduma za afya hospitalini mama zangu mnatakiwa mwende na nyembe mnapotaka kujifungua, serikali inashindwa kununua wembe lakini wakati wa uchaguzi inaweza kununua kitenge kwa kila mwanamke Tanzania nzima,” alisema Bw. Mtatiro.


Alisema wakati wa mabadiliko ndio huu na wananchi hawana budi kukiunga mkono chama hicho ili kiweze kuongoza mapambano dhidi ya rushwa, matumizi mabaya ya fedha za umma ili kuwakomboa wananchi.

weka source mkuu
 
Mtaleta mpaka nyuzi za miaka ya 1980 ambayo Dr. Slaa alikuwa akisifia CCM,, huu ni uthibitisho wa dawa kuwaingia.....! Go go UKAWA
 
Kuweni makini na wanfiki na wasaliti wa Demokrasia,hiyo habari ni ya muda mrefu sana,je Mtatiro bado ni naibu katibu mkuu?
 
Acheni uchochezi.post ya kipumbavu hainamantiki kwa msomaji.tafuta nyingine.
 
Hivi sijui hawa wanasiasa huwa wanatuchukuliaje sie wananchi,yani pamoja na yote hayo ila mwishoni wamekuwa kitu kimoja. Mie huwa najiuliza sasa hayo aliyoyasema Lipumba kuhusu chadema hivi sasa yamefutika au aliyaongea kisiasa siasa tu? Na uccm B wa cuf uliyoelezwa na chadema nao umeishia wapi?
 
Source ya hii habari ni vipi. Mbona Picha hakuna. Hata audio.
 
huu ndo muungano wa ukawa eti.!

Hawa wanategwa tu na chadema kwa kamba ya UKAWA ; Kiukweli chadema ni malaghai wa siasa, cuf kuweni macho. Japo uzi huu ni muda kidogo lakini ndio unaonyesha taswira halisi ya chagadema.
 
Already expired....we are now talking about UKAWA. Loading.......for October
 
Kweli nimeamini kwenye siasa hakuna adui wala rafiki wa kudumu ikiwa vyama vilivyotoleana matusi ya namna hii leo wanakaa meza moja na kukubaliana,
Kweli wanasiasa wekeni akiba ya maneno.
 
Hivi sijui hawa wanasiasa huwa wanatuchukuliaje sie wananchi,yani pamoja na yote hayo ila mwishoni wamekuwa kitu kimoja. Mie huwa najiuliza sasa hayo aliyoyasema Lipumba kuhusu chadema hivi sasa yamefutika au aliyaongea kisiasa siasa tu? Na uccm B wa cuf uliyoelezwa na chadema nao umeishia wapi?

Ndio hapo sasa, akili za kuambiwa changanya na zako. Usimwamini mwanasiasa yoyote mpaka afe.
 
Sielewi nini hatma ya ukombozi WA nchi hii,kama wanaojiita wakombozi wanaendelea kugawanyika,na wapi ktk umoja ,kwa Kweli Nina Mashaka sana na mchezo wa siasa za tanzania
 
Profesa hakukurupuka huyo lazima kaona ukweli...Cdm wafadhili wake sio wema sana. Ni kitu kibaya kufadhiliwa na wafanyabiashara baadae watawalipa nini..
 
mleta mada umevurugwa! mada ya lini? hutupati Ukawa ndio tumaini letu. ccm ni janga.
 
Back
Top Bottom