Estmeed Reader
Senior Member
- Mar 19, 2010
- 134
- 0
Tatizo ni chama chake? we need a liberal party na si chama chenye mwonekano wa kidini kama CUF. Mikutano yao ni kama forum ya walimu na wanafunzi wa madrassa. Na ndiyo sababu ccm inashinda maana watu wanaona ni bora jini ulijualo kuliko usilolijua.
Hakuna kiongozi yeyote wa upinzani anayeweza kukubali kuiunga mkono CUF kwa sababu ya mwonekano wa Udini ilionao.
Kweli anaweza kushindana na siyo kushinda sisi tunataka mshindi. Hii itakuwa ni mara ya ngapi vile?
hakuna njia ya haki ambayo wananchi wanaweza kuhusishwa kumchagua mgombea wanae mtaka kutoka upinzani kuliko Lipumba kujipigia pande mwenyewe kwamba yeye ndio anafaa?
Hakuna Udini wala ukabila katika Uchaguzi mkuu Sisi tunachotaka kwamba Apatikane Kiongozi atakaye weza Kushindana Na Mzee J.Kikwete. wewe Unafikiri Mtu kama Mzee Mrema,Mtikila, na viongozi wengine ukimtowa Proffesor Lipumba kuna Mtu yoyote anayeweza kusimama na Mzee Kikwete na akamshinda katika Uchaguzi Mkuu? Tutakuwa kila siku Washindikizaji wa CCM, na hiyo CCM kila ukifanyika uchaguzi watakuwa wao ndio Washindi wakuu. Kwa Ushauri wangu mimi vyama vyote vya upinzani vimuunge Mkono Proffesor Lipumba kwanza na jambo la pili vyama vya Upinzani kama vitaungana kuwa kitu kimoja basi vinaweza kushinda katika Uchaguzi Mkuu. Asanteni sana.UDINI! UDINI! UDINI! Chama chake kimejaa udini na hii nchi haina dini, we unazani itakuaje? aendelee kupiga makelele jukwaani na kuikosoa serikali ili siku ziende lakini si yeye wala chama chake cha kuitawala nchi. afu mi nashangaa kama vile hawaoni wajirekebishe..
Jamaa ili linaweza ila shida yangu ni kuwa kwenye mikutano ya siasa ya CUF baraghashea na ijabu ni nyingi sana!!!
Hivi Chadema ilishinda lini vile Urais?lolKweli anaweza kushindana na siyo kushinda sisi tunataka mshindi. Hii itakuwa ni mara ya ngapi vile?
Afanye hata hayo madudu wanayofanya CCM lakini bora yeye utakuwa ni ukurasa wake wa kwanza wa madudu.wamsimamishe ili afanye nini?
Alisema anakusudia kuwasilisha maombi hayo kwa vile haoni kama kuna mtu katika vyama hivyo mwenye uwezo wa kukabiliana na mgombea wa kiti hicho kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, kulingana na hali ya kisiasa ilivyo nchini.
wamsimamishe ili afanye nini?
Ndiyo maana huyu mheshimiwa hafanikiwii. Hana hulka ya kisiasa wala maneno ya kidoplomasia. Utaombaje vyama vingine visi simamishe wagombea na kuunga mkono chama chako kwa kusema kuwa vyama vyao hawana watu wenye uwezo? Ana fikiri kuna chama kita kacho kubali kuambiwa kuwa hamna mgombea mwenye uwezo tokea chama chao?
You are absolutely right. Hakuna shaka kwamba CUF kina mwelekeo wa kuwa chama cha kidini. Hata kampeni zao wanapigia zaidi misikitini.
CUF kinaweza kutoa Rais wa Zanzibar lakini hakiwezi kutoa Rais wa Tanzania. Lipumba agombee ubunge. Hatakaa awe Rais wa Tanzania.
You are absolutely right. Hakuna shaka kwamba CUF kina mwelekeo wa kuwa chama cha kidini. Hata kampeni zao wanapigia zaidi misikitini.
CUF kinaweza kutoa Rais wa Zanzibar lakini hakiwezi kutoa Rais wa Tanzania. Lipumba agombee ubunge. Hatakaa awe Rais wa Tanzania.