Elections 2010 Lipumba atangaza kugombea urais 2010

lipumba atadunda hadi atafia kwenye siasa zisizo na mafanikio hivyohivyo, kwasababu ya udini. ungunguli na kufanya mikutano kwenye misikiti. ataishia kupata vidili vya kufundisha vyuo nje kama visiting prof. tu alipwe milioni moja au mbili kwa safari zake aendelee kujaza mafuta kwenye magari...akili ya uchumi kichani anayo sana, lakini akili ya kuiunganisha na kuiendesha tz kama nchi ya watu wenye dini tofauti, sina imani naye kabisa.
 
Lipumba%2816%29.jpg

Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba

Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amesema ataviandikia vyama vingine vya upinzani barua rasmi, kuviomba visisimamishe wagombea urais, badala yake vimuunge mkono yeye katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu.
Profesa Lipumba alisema hayo wakati akiwashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa CUF, kwa kumpitisha kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho katika uchaguzi huo Alisema anakusudia kuwasilisha maombi hayo kwa vile haoni kama kuna mtu katika vyama hivyo mwenye uwezo wa kukabiliana na mgombea wa kiti hicho kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, kulingana na hali ya kisiasa ilivyo nchini.
Profesa Lipumba aligombea urais katika uchaguzi wa mwaka 1995, 2000 na 2005 na kushindwa huku baadhi ya watu wakivitaka vyama vya siasa kusimamisha mgombea mmoja, lakini viongozi wa upinzani mara zote kushindwa kukubaliana.
Profesa Lipumba ambaye alipitishwa kwa kupata asilimia 99.7 ya kura zote zilizopigwa, alisema iwapo chama chake kitafanikiwa kushinda katika uchaguzi huo, miongoni mwa mambo makuu yatakayotekelezwa, ni pamoja na kuunda serikali ya umoja wa kitaifa. Jana CUF walitangaza kwamba Lipumba alikuwa amepata ushindi wa asilimia 98.97, lakini baadaye usiku wakasema kulikuwa na makosa katika ukokotoaji hivyo kubainika kwamba alikuwa amepata asilimia 99.7.
Kadhalika, chama hicho kilisema kuwa ukokotoaji wa ushindi wa Maalim Seif nao ulikuwa umekosewa kuwa asilimia 96.38 badala ya asilimia 98.88.
Alisema pia, ataboresha elimu kufikia viwango vya kimataifa na atahakikisha mafisadi wote wanashughulikiwa ipasavyo.
"Naamini kwa uwezo nilionao, ninaweza kutatua matatizo ya nchi hii, na nina hakika ya kupata tuzo ya utawala bora," alisema Profesa Lipumba na kushangiliwa na karibu ukumbi mzima wa mkutano huo.

CHANZO: NIPASHE

Mimi binafsi yangu Nakubaliana na wewe waweza kushindana na CCM. Je Mnasemaje Wakuu wenzangu wa J.F?

I do not having any Problem with him personal, and i dont doubt his potential and ability... he is the Candidate of its Kind... tatizo ni hicho chama msingi ya toka mwanzo ilyokuwa imeipandikiza ndio imewaharibia, i dont see him winning , as i dont see any of this so called political parties unite, kwanza achilia mbali kuwa na priority tofauti katika ILANI zao lakini misingi ya ukabila na udini unaviua hivi vyama bila kujijua na ndio silaha ambayo wanaitumia CCM katika kuvimaliza.... huwezi ukatengeneza gari jipya kwa kutumia vifaa vya GARI chakavu utaliitaje hilo jipya na imara... sasa hivi vyama Wamepaste almost 90% ya mambo mengi kutoka CCM, and to make thing even worse wameingiza ukabila na udini... what the hell do u expect.... CCM is not as strong as ppl seems to think... its just use ur own weakness to destroy U... the problem u keep point on their weakness "which is the same weakness as of urs" and thats left voters with no choice and exception and the keep voting for CCM... THEY SIMPLY DO NOT SEE ANY THING NEW..ANYTHING TO CONVINCE THEMTO VOTE 4 U ....jisafisheni kwanza then ndio mje kwetu otherwise it simply the old same story....anyway i am no FAN of this political stuff , i am afraid of being a "Serial Killer"....

HAYO ni MAWAZO WANGU.....
 
Ukweli ubakishwe kuwa ukweli ,Lipumba ni mmoja kati ya wagombea ambae anaweza na ameweza kutoa chalenge kwa CCM na serikali yake ni kweli kabisa amefanya kosa kama alitamka kuwa vyama vingine havina wagombea wanaoweza kugombea nafasi hio,hapo atakuwa amechemsha ,ila kwa wagombea wa vyama vingine basi Lipumba ni bora zaidi na anakubalika kirahisi sana au kwa lugha ingine anauzika ,ni mgombea pekee alieweza kutoa guarantee ya kuitoa Tz katika umasikini ikiwa atafanikishwa kuwa Raisi wa Inchi hii.

Unajua huyu mtu ana uzunguuzungu kidogo kwa maana ya kutomuonea haya mtu yeyote yule ,yaani yupo siriyazi kabisa ,kwa maana kwa wenzetu huko uzunguni hakuna cha kuhifadhiana au kulindana ,watu wanakukacha mchana kweupe na zaidi watakwambia ...sorry we can not help you...!!!

Ipo haja ya kulijaribu hili kiuzalendo kabisa ili kuiweka Tz katika msatari baada ya kuwa hapa ilipo inakwenda zigzaga !!!
 
CCM wanakampeni kuwa CUF ni chama cha kidini, na CHADEMA cha wachaga, kwa hili wamewashinda wengi. Na wengine wanaingia katika mkumbo ule ule wakiwa katika jahazi la kuiondoa CCM madarakani, wanaanza kuimba propaganda zilezile za CCM na kunyoosheana vidole.

Kwa jinsi hii kuja kuitoa CCM madarakani itakuwa miujiza.
.. ...Kwa utaratibu huu CCM haitotoka Madarakani Maisha. Hadi ujinga ututoke vichwani...wale wanaouponda Uongozi wa JK ni wale waliokosa Fursa za Kufanya Ufisadi. They dont wan real change...!!!
 
You are absolutely right. Hakuna shaka kwamba CUF kina mwelekeo wa kuwa chama cha kidini. Hata kampeni zao wanapigia zaidi misikitini.

CUF kinaweza kutoa Rais wa Zanzibar lakini hakiwezi kutoa Rais wa Tanzania. Lipumba agombee ubunge. Hatakaa awe Rais wa Tanzania.
....Hivi kama chama kina Udini kwanini kiwepo? Why dont you make a petition chama Kifungiwe?...halafu wewe mwalim wa Chuo Kikuu...is it?
Hivi kama mtu yuko proved Mdini kwanini umpe fursa tena agombee Ubunge?

Labda Utusaidie kututajia Misikiti ambayo Lipumba amekuwa akihubiri mawaidha ya Chama chake...!!!

kama Hijabu na Bagharashia zinakuudhi kuonekana ktk Mikutano ya CUF, hebu tafuta Kalenda za mwanzo after Uhuru uone picha za Mikutano ya TANU na Umoja wa Wanawake wa TANU...labda zaweza kukusaidia kuona Hali ilikuwaje wakati huo...!!!
 
..Prof.Lipumba ni msukule tu wa Maalim Seif Sharrif Hamad.

..ni Mtanganyika wa aina gani anaweza kuvumilia na kuwa mwenyekiti wa chama kinachoi-demonize Tanganyika na wananchi wake kama CUF ya Maalim Seif Sharrif?

..sidhani kama Prof.Lipumba ana nia ya dhati ya kum-challenge na kumuondosha JK madarakani. mwenendo na matamshi yake kuhusu KIkwete na uongozi wake hayaashirii kama kweli anaamini Tanzania inastahili Raisi mwingine other than Kikwete.
 
JokaKuu hivi lini utaacha kuabudu watu?...Hivi leo Maalim Seif akifa...Lipumba atakuwa msukule tena wa nani? Acha kumuogopa Seif..yeye ni binadam km binadam wengine, wamepita kabla yake watu maarufu, mashuhuri na wenye nguvu kuliko yeye...!!wapo leo hii? chini ya kaburi.

Unavyotaka wewe Tanganyika iweje? kwanza Tanganyika yenyewe ipo? acha umakengengeza bro khs Muungano...kama waznz wanaterms wanataka zijadiliwe, Let us discuss with them.kutokubali ukweli wa kelele zao si salama for better future of Muungano...Hivi hizi Kelele za Muungano zitaacha lini? hebu basi tuzimalize, then tufocus ktk matatizo ya Jumla ya Taifa yanatukabili sote.

Labda uwasaidie watz wote kuwajulisha ni nani yu-serious kuwaondoa CCM or JK baada ya Prof.Lipumba...!!!
 
ila kwa wagombea wa vyama vingine basi Lipumba ni bora zaidi na anakubalika kirahisi sana a

!

Vyama Gani hivyo?Coz Mpaka sasa hivi ni CUF ndio wametangaza Mgombea wao. BTW Huyu Mheshimiwa sasa hivi si yuko DOM kwenye NEC ya CCM anakula Per Diem au
 
Chuma said:
JokaKuu hivi lini utaacha kuabudu watu?...Hivi leo Maalim Seif akifa...Lipumba atakuwa msukule tena wa nani? Acha kumuogopa Seif..yeye ni binadam km binadam wengine, wamepita kabla yake watu maarufu, mashuhuri na wenye nguvu kuliko yeye...!!wapo leo hii? chini ya kaburi.

Unavyotaka wewe Tanganyika iweje? kwanza Tanganyika yenyewe ipo? acha umakengengeza bro khs Muungano...kama waznz wanaterms wanataka zijadiliwe, Let us discuss with them.kutokubali ukweli wa kelele zao si salama for better future of Muungano...Hivi hizi Kelele za Muungano zitaacha lini? hebu basi tuzimalize, then tufocus ktk matatizo ya Jumla ya Taifa yanatukabili sote.

Labda uwasaidie watz wote kuwajulisha ni nani yu-serious kuwaondoa CCM or JK baada ya Prof.Lipumba...!!!

Chuma,

..sina uwezo wa kujua nani kati ya Maalim na Nguyuru atatangulia mbele ya haki kabla ya mwenzake. kwa msingi huo siwezi kujibu swali lako.

..lakini kwa hali ilivyo sasa hivi Nguyuru ni msukule tu wa Maalim.

..binafsi sikatai masuala ya Muungano kujadiliwa, tena ingekuwa amri yangu ningeuvunjilia mbali.

..kinachonikwaza mimi ni hii hali ya CUF kutu-demonize wa-Tanganyika kila kukicha, na "mwenyekiti" Nguyuru Lipumba kukaa kimya kama vile ni msukule. hana hata ujasiri wa ku-disagree respectfully.

..jinsi Maalim anavyowa-demonize wa-Tanganyika ni sawasawa na Mtikila anavyowa-demonize wa-Zenj. sasa sijui wewe utamuelewaje m-Zenj mwenye ushirika wa kisiasa na Christopher Mtikila.

NB:

..kelele za muungano haziishi kwasababu wanaozijadili siyo wa kweli to begin with.

..wengi wao wanapiga makelele kwa maslahi ya kisiasa tu na si vinginevyo.
 
Umakini wake uko wapi na Wakati na yeye Amekimbilia Pilau ya CCM Dodoma

Kaka upo nchi gani? kila chama kikifanya mkutano wake Mkuu kinawaalika wageni either from Vyama vingine au from Mabalozi...You need to go back to school.
 
Kaka upo nchi gani? kila chama kikifanya mkutano wake Mkuu kinawaalika wageni either from Vyama vingine au from Mabalozi...You need to go back to school.

Mimi Niko Bongo Mkuu, niambie ni Chama katika Nchi gani kimehudhuria Mkutano wa Chama kikingine halafu Kiongozi wake akatukanwa na Kudhalilishwa naye akaendela kukenua Meno
 
Chuma,

..sina uwezo wa kujua nani kati ya Maalim na Nguyuru atatangulia mbele ya haki kabla ya mwenzake. kwa msingi huo siwezi kujibu swali lako.

..lakini kwa hali ilivyo sasa hivi Nguyuru ni msukule tu wa Maalim.

..binafsi sikatai masuala ya Muungano kujadiliwa, tena ingekuwa amri yangu ningeuvunjilia mbali.

..kinachonikwaza mimi ni hii hali ya CUF kutu-demonize wa-Tanganyika kila kukicha, na "mwenyekiti" Nguyuru Lipumba kukaa kimya kama vile ni msukule. hana hata ujasiri wa ku-disagree respectfully.

..jinsi Maalim anavyowa-demonize wa-Tanganyika ni sawasawa na Mtikila anavyowa-demonize wa-Zenj. sasa sijui wewe utamuelewaje m-Zenj mwenye ushirika wa kisiasa na Christopher Mtikila.

NB:

..kelele za muungano haziishi kwasababu wanaozijadili siyo wa kweli to begin with.

..wengi wao wanapiga makelele kwa maslahi ya kisiasa tu na si vinginevyo.

Jokakuu labda neno Msukule hulijui ndio maana umeendelea kulitumia. Ukiwa hujui nani atatangulia kaburini...Ikiwa tutalitumia kwa dhana yako, Je nawe umewekwa Msukule na CCM?....basi endelea kuwa "Msukule" wa CCM hadi hapo utakapo mpapata Mganga aje akutoe ktk Usukule wa CCM"

Kama umeshindwa kusema Unataka Tanganyika iweje, Unataka Lipumba asemaje khs Tanganyika/Muungano? Msimamamo wa CUF upo so clear ktk Issues za Muungano...!!! unataka Lipumba a-disagree na Seif kwa lipi?...Issues za Mtikila ni Tofauti, pamoja na kuwa one thing in common ya kuhitaji Tanganyika...Labda Utovu wako wa Nidhamu ndio unaokupelekea kumwita majina mabaya Prof. Lipumba..mara msukule....na mengine..au tu ni chuki zako zilizokujaa.

So far umeshindwa kuwasaidia Watz kuwajuza nani anaweza pambana na CCM kwa wakati huu.
 
Mimi Niko Bongo Mkuu, niambie ni Chama katika Nchi gani kimehudhuria Mkutano wa Chama kikingine halafu Kiongozi wake akatukanwa na Kudhalilishwa naye akaendela kukenua Meno
NU...Pitia humu JF vizuri uone namna ya Chadema na CUF zilivyofanya mikutano yao na akina nani walialikwa...Issues za Kutukanwa Sijui. Labda unijuze Matusi gani yalitolewa ktk mkutano huo wa CCM.
 
NU...Pitia humu JF vizuri uone namna ya Chadema na CUF zilivyofanya mikutano yao na akina nani walialikwa...Issues za Kutukanwa Sijui. Labda unijuze Matusi gani yalitolewa ktk mkutano huo wa CCM.

Unajua Chairman Unapoitwa Vuvuzela inauma sana Mkuu, Viongozi wa Upinzani hawakuswa kuhudhururia Ufujwaji huu wa Pesa ambao Baadaye wataanza kusema CCM imetumia pesa chafu kushinda Uchaguzi na wakati wao wameanza kuzitumbua Dom
 
.... huwezi ukatengeneza gari jipya kwa kutumia vifaa vya GARI chakavu utaliitaje hilo jipya na imara... sasa hivi vyama Wamepaste almost 90% ya mambo mengi kutoka CCM, and to make thing even worse wameingiza ukabila na udini... what the hell do u expect.... CCM is not as strong as ppl seems to think... its just use ur own weakness to destroy U... the problem u keep point on their weakness "which is the same weakness as of urs" and thats left voters with no choice and exception and the keep voting for CCM... THEY SIMPLY DO NOT SEE ANY THING NEW..ANYTHING TO CONVINCE THEMTO VOTE 4 U ....jisafisheni kwanza then ndio mje kwetu otherwise it simply the old same story....anyway i am no FAN of this political stuff , i am afraid of being a "Serial Killer"....

HAYO ni MAWAZO WANGU.....

Maneno mazito sana haya.
 
Unajua Chairman Unapoitwa Vuvuzela inauma sana Mkuu, Viongozi wa Upinzani hawakuswa kuhudhururia Ufujwaji huu wa Pesa ambao Baadaye wataanza kusema CCM imetumia pesa chafu kushinda Uchaguzi na wakati wao wameanza kuzitumbua Dom
Kaka Hapa JF kuna mdau aliweka mada ya kuwa Dr. SLAA ni Vuvuzela...kabla ya hio ya CCM. does it mean that Dr. SLAA asiingie tena JF kwa kuwa ameitwa Vuvuzela na genge fulani tu?....km Kiongozi nafikiri kuna matusi mengi tu unaweza yapata muhim ni kuwa mvumilivu. Wengi wa watoaji maneno mabovu ni wajinga. Kumbuka Mrema alivyokuwa CCM na maneno gani alikuwa anawapa Wapinzani?...JK mwenyewe ameshaitwa majina mengi ya hovyo..kwa nafasi alonayo angeweza kuwaweka selo. lkn kachukuwa uamuzi gani?...Hivi Wale Ze Komedy ushawaona? unaridhia wanachofanya?...ifikie Kipindi sis kama watanzania au wasomi tuwaone wote wanawatukana wenzao ni Wajinga/au Majuha...lkn Ukishakuwa Kiongozi itabidi uvumilie tu, otherwise Kaa na Mbali na Uongozi.

By the way hata kama Viongozi wa Upinzani wasingekwenda Dodoma, bado Vyombo vyote vya habari vilikuwa LIVE DOM...na wale wa Nje ya nchi wameona LIVE..so ulitaka Hawa Viongozi wakae kisiwa gani wasione au wasijue yanayotokea Dodoma?...bro pls think Wide.
 
nafikiri viongozi wote wa upinzani wangepigiwa kura na wachagua mmoja wa kugombea na kikwete kila mtu kivyake CCM forever tuwaige wenzetu wa kenya wajameni
 
Back
Top Bottom