Prof. Lipumba amesahau kwamba yeye ni kiongozi wa CUF siyo waislam. CUF wanalishughulikia kwa msingi gani? Eti kazungumza na Kova - rpc - kama nani? Kwani Ponda ni kiongozi wa CUF? Lipumba kavaa ngozi yz kondoo!!!
Kama walivyosema wachangiaji wengine Prof amedhihirisha udhaifu wake na hafai hata kupewa kura, labda ya Ponda. Hakika hata mke wake atamnyima kura.
Phobia ni ugonjwa wa kisaikolojia
unaomfanya mwenye kuwa nao
awe na woga na chuki za
kupindukia zisizo na msingi dhidi
ya kitu, mtu au hali fulani. Katika
kamusi, neno hili limefasiliwa kama irrational fear and, or, irrational
abhorrence. Na miongoni mwa
fasili za neno irrational ni illogical,
unreasonable, foolish, crazy,
ridiculous, absurd, silly na
unfounded. Siwezi kutafsiri kila moja ya fasili hizi, lakini itoshe
kusema, kwa ufupi na kwa jumla,
kuwa phobia ni aina moja ya
uwendawazimu. Na wendawazimu tuko wengi.
Tumo miongoni mwetu, kwa
mfano, tunaogopa buibui, kiumbe
dhalili kama vilivyo, bila ya
ushahidi ikiwa vidudu hivi vina
madhara kwetu. Wengine tunaogopa kupanda ngazi ama
kuangalia chini baada ya kupanda
juu, kwa kisisi cha kuanguka.
Tupo tunaoogopa kupita maeneo
ya wazi, kama uwanja wa mpira,
tukidhani dubwana fulani linaweza kutokea hapo na
kutubeba. Mara nyingi dhana hizi
zina chimbuko lake katika sadiki-
ukipenda, stereotypes. Lakini phobia si kuogopa peke
yake. Kwa kuwa ni woga usio na
msingi, basi huja na chuki. Kwa
hivyo, kwa kumuogopa jongoo
kwa ujinga wetu wa
kutomkumjua, kwa mfano, tunaishia kumchukia. Utamsikia
mtu akisema: dudu hili
silipendi, kumbe pia analiogopa.
Hali hiyo hiyo hutokea kwa kwa
kuwachukia watu wengine
kutokana na giza hilo hilo la kutokuwajua. Nakusudia kuwa nyingi ya chuki
zetu kwa watu na, au, imani zao
zinatokana na ujinga wetu.
Tunaowajua kikwelikweli huwa
aidha hatuwachukii kabisa na, au,
hata tukiwachukia, hatuwaogopi. Vivyo hivyo kwa imani zao. Lengo la makala hii si
kuitambulisha phobia kwenu, bali
kuitambulisha kwamba ipo na,
kwa muktadha huu, ipo zaidi
katika jamii za Magharibi (Ulaya
na Marekani) kwa jina la islamophobia. Ugonjwa huu
haujaanza leo katika dunia hiyo,
lakini ni bahati mbaya sana
kwamba licha ya kutambulika
kwake, bado haujaponywa kwa
kuwa ni ugonjwa unaopendwa na kukubalika na tawala za huko. Miaka nenda miaka rudi sasa,
woga unaoambatana na chuki
dhidi ya Uislam na, au, kitu
chochote kinachohusishwa nao,
umekuwa ukienezwa kwa kila
aina ya rangi na sura na tawala mbali mbali za Magharibi (bila ya
shaka kwa maslahi ya kisiasa na
kiuchumi ya familia za tawala
hizo), huku nyuma ya
islamophobia yenyewe kukiwa na
ujinga wa kutokuujuwa kabisa huo Uislam wenyewe. Na sasa
ugonjwa huu unaugharimu
ulimwengu wote kwa jumla. Mimi si muhubiri wa dini, na
sikusudii kuigeuza makala hii
kuwa kipande cha mjadala mpana
wa kidini, lakini ni muumini na
mfuasi wa itikadi inayotambua
mdahalo na mdahala (dialogue and coexistence) baina ya watu
wa dini tafauti na juu ya umoja
wa imani zao kuliko tafauti zao.
Nimelelewa na kukulia katika
mazingira hayo hapa hapa
Zanzibar. Nazungumza dhidi ya islamophobia
si kwa sababu ya Uislam wangu,
la. Hata ningelikuwa muumini wa
dini nyengine, bado itikadi yangu
ya mdahalo na mdahala
ingeliniambia kuwa islamophobia ni ugonjwa usio faida kwa dini
yoyote ile, bali unaoitishia
kuimomonyoa hata misingi ya hizo
dini zenyewe. Nazungumza dhidi ya islamophobia
kwa kuwa ni saratani inayoila
itikadi hiyo. Vita dhidi ya ugaidi
vinavyoongozwa na Marekani
vikiungwa mkono na nchi kadhaa
za Ulaya, kwa mfano, licha ya kuwa pia na tafsiri kadhaa za
kiuchumi na kisiasa, ni matokeo
mamojawapo ya ugonjwa huu. Vita hivi havijaisaidia dini yoyote
na wala havitafanya hivyo milele.
Vinaweza, yumkini, kutanua na
kudhoofisha himaya za kisiasa na
kiuchumi za tawala fulani, lakini
kamwe haviwezi kutanua ama kudhoofisha himaya za kidini.
Panapohusika imani za
walimwengu kidini, vita hivi
vinajenga kuta zaidi baina ya
waumini wa imani tafauti kuliko
kujenga madaraja baina yao. Kauli ya karibuni ya Andres
Tobias Rubio, afisa wa ngazi ya
juu wa Jumuiya ya Ulaya (EU)
anayeshughulikia masuala ya
Afrika, Karibian na Pasifiki (rejea
magazeti ya Mwananchi na The Citizen ya tarehe 01 Oktoba,
2006), kwamba Jumuiya yake
iliendelea mbele kukubaliana na
matokeo ya uchaguzi wa
Zanzibar wa mwaka 2005 hata
baada ya kuwapo ushahidi unaonesha kinyume chake, kwa
kuwa tu haikutaka kukiunga
mkono Chama cha Wananchi (CUF)
inachokihusisha na Uislam, ni
mfano mmoja kati ya mingi ya
kuwepo na kukubalika kwa ugonjwa huo wa islamophobia
katika dunia ya Magharibi. Kwa mujibu wa Rubio ni kwamba
hata kama jumuiya yake iliyaona
matatizo chungu nzima
yalioukabili uchaguzi huo ambayo
yaliuweka mbali na vigezo vya
kuwa huru na wa haki, bado, kwa kuhofia kwake kwamba CUF
ni chama kinachofuata siasa za
Kiislam, ilifumbia macho matatizo
hayo na ikayapa kisogo matakwa
ya demokrasia, ili Zanzibar
iendelee kuwa ya amani kwa watalii wa Ulaya kuweza
kuitembelea. Ni islamophobia. Baadhi ya wakati,
hata wenye ugonjwa huu,
hutumia sababu kengefu
kukijengea ukuta wa ulinzi kile
wakiaminicho. Katika hili, EU
inaweza kuwa imetumia ile iitwayo deductive reasoning,
yaani kusema kwa kuwa
Wazanzibari wengi ni Waislam, na
kwa kuwa Wazanzibari wengi
wanaiunga mkono CUF, basi CUF
ni chama cha Kiislam. Ikiwa hutumii kipawa chako vyema,
unaweza nawe ukaambukizwa
ugonjwa huo huo. Lakini, ukiangalia hili katika
uhalisia wake, utajuwa kuwa CUF
inaungwa mkono zaidi Zanzibar
kuliko sehemu nyengine za
Tanzania, si kwa sababu za kidini,
lakini kutokana na historia yake ya mapambano na namna
ambavyo inauelezea Muungano
wa Tanzania. CUF haitaki kuvunja
Muungano lakini inazungumzia
kuipa hadhi zaidi Zanzibar kuliko
ilivyo sasa. Na hicho ni kitu kinachopendelewa na zaidi ya
nusu ya Wazanzibari. Sasa kwa
kuwa Zanzibar ina Waislam wengi,
bila ya shaka CUF itakuwa na
wanachama wake miongoni mwa
Waislam hao. Si kwa kuwa wao ni Waislam, bali ni kwa kuwa wao ni
Wazanzibari. Vyenginevyo, ilikuwa iwatoe wapi
na ifanyeje? Waanguke kutoka
mbinguni? Au iwatake wabadilishe
dini yao kwa kuwa tu sasa
wanaingia katika mfumo wa siasa
za vyama vingi, ambao waliozileta (Ulaya na Marekani) wanaiogopa
na waniuchukia dini yao. Kwa
kufanya hivyo, CUF nayo pia
ingelikuwa na islamophobia! Vyama vingi havikuja
kuwapokonya watu dini zao. Wala
Zanzibar haijapata kuwa na
tatizo la imani kali za kidini katika
historia yake. Licha ya kuwapo
kwa mchanganyiko wa kitamaduni, hakujawahi kuwapo
na ukereketwa wa kidini katika
Visiwa hivi. Waumini wa dini zote
wamekuwa wakiishi vyema huku
kila mmoja akitambua na
akiheshimu uwepo wa mwenzake. Zipo familia Zanzibar ambazo
wanafamilia wake wanatoka dini
tafauti na hilo halijapata kuwa
tatizo kwao. Lakini wenye islamophobia
hawawezi kuliona na kulitambua
hilo. Kwao wao, madhali CUF
inaungwa mkono zaidi Zanzibar
kwenye Waislam wengi, hitimisho
ni kwamba CUF ni chama cha Kiislam na hivyo kuingia kwake
madarakani kunamaanisha
kuanzisha utawala wa Kiislam
ambao, kwa mujibu wa akina
Rubio wa EU, hupelekea
machafuko na hali ya kukosekana kwa usalama katika
taifa husika. Jukumu la kuthibitisha kwamba
CUF si chama cha kidini ni la
wanachama na uongozi wa CUF
wenyewe, lakini msimamo wa
Jumuiya hii unatakiwa kuipa
changamoto CUF kwa kuionesha sura halisi ya watu
inaowatambua kama washiriki
wazuri wa ujenzi wa demokrasia. Kwamba hawa si wenza wazuri
wala makini katika utetezi wa
haki za walimwengu wenzao,
maana vichwani mwao muna
tatizo la islamophobia. Kwamba
wanauogopa na kuuchukia sana Uislam kiasi ambacho akili zao
zinagoma kufikiri na hivyo
kwenda kinyume na hata misingi
ya demokrasia wanayodai
kuitetea kwa gharama zote. Ikiwa baada ya damu yote
kumwagwa, heshima yote ya
Wazanzibari kuvunjwa na baada
ya mateso yote waliyopata
Wazanzibari huku wao
wakishuhudia, bado walikwenda mbele kuhalalisha matokeo
yanayotokana na uchaguzi huo,
basi hawa si watu wa kuwaamini.
Si watu wa kuwaamini, maana
wako tayari kukuuza kwa bei
rahisi ati kwa kuwa tu wewe ni Muislam. Islamophobia ndio hasa
unaosababisha kuzaliwa kwa
magaidi wanaojinasibisha na
imani za dini ulimwenguni. Kwa nini
wakajinasibisha na dini, ni kwa
kuwa walipokandamizwa (au katika mfano huu, waliposalitiwa
na kuachwa wateseke) dini yao
ndiyo iliyokuwa kigezo.
Waliangaliwa kwa mujibu wa dini
zao na wakakandamizwa kwa
mujibu wa dini hiyo, nao, katika kutafuta utetezi, hutumia dini
hiyo hiyo. Hiyo, japokuwa si halali,
ndiyo mantiki nyepesi kabisa ya
ufurukutwa wa kidini. Zanzibar ya sasa haiko tulivu
(ikiwa hali ya sasa inaweza
kuitwa hivyo) kwa kuwa CUF
ilishindwa kuingia madarakani, bali
ni kwa kuwa bado CUF imebakia
kuwa kama CUF___ chama cha siasa kinachotumia siasa kufanya
siasa. Hilo limeipa CUF uhalali na,
hivyo, mamlaka, miongoni mwa
Wazanzibari walio wengi. Siku CUF, kwa maana ya uongozi
wake, itakapopoteza udhibiti wa
siasa za nchi, huo usalama na
utulivu anaozungumia Rubio pia
utapotea. Kuwadhibiti na
kuwaongoza watu waliovunjwa moyo na usaliti wa mara kwa
mara (kama huu wa EU), ni kazi
kubwa sana. Ni kazi ngumu
inayofanywa sasa na uongozi wa
CUF na inaonekana hadi sasa
hakuna mbadala wake. Lakini usaliti ukiendelea, mbadala
utakuwa hauepukiki.