Wana JF,
Jana nilibahatika kuangalia taarifa ya habari ITV na TBC pia. Moja ya habari ilivyorushwa hewani ilikuwa ikimuonesha Prof. Lipumba, Mwenyekiti wa CUF Taifa, akiwasihi waislamu wenzake (Nasisitiza hili kwa kuwa Prof alitumia neno "Nawasihi Waislam wenzangu kutokufanya maandamano yoyote kesho (leo) baada ya swala ya Ijumaa". Nilitafakari sana na kujiuliza mambo mengi, ni nani huyu Profesa Lipumba? Alizungumza kama Mwenyekiti wa CUF Taifa akiwasihi waislam wenzake wasifanye maandamao leo au alikuwa akizungumza "in his personal capacity as Prof. Lipumba?". Naomba nipate ufafanuzi wa hili kwa kuwa utangulizi wa taarifa hiyo ulimzungumzia Prof. Lipumba kama mwenyekiti wa CUF. Nitashangaa sana leo, kama kweli waislam wataacha kuandamana leo kwa kutii alichosema Prof. Lipumba, kwa kufanya hivyo, kwa maoni yangu, "any reasonable person will come to the conclusion that CUF and Islam in Tanzania are inseparable"
I submit