lini tUtagawana mali za mafisadi jamani??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

lini tUtagawana mali za mafisadi jamani???

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Nov 17, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 17, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,277
  Likes Received: 5,638
  Trophy Points: 280
  mmmmmmhhhh
  aaa jamani mi nimechoka na story za hawa mafisadi...hivi sasa tuangalie jinsi gani tutakamata mali zao sisi kama watanzania tugawane haki yetu...kila thread naona kinachoendelea ni kuongezeka kwa mafisadi tena wengine wanarudia uchafu uleule tunaopigia kelel hapa...embu angalia hivi majuzi kulikuwa na hafla ya MO ...cha ajabu ndani mule walikuja karibia mafisadi wote waliotajwa kwenye EPA,DEEPGREEN,mmmh mi sijui...sasa kama hawa watu tunawakaribisha na huku tukijifanya kuwapeleka mahakamni...huu uhuni mtupu...wakina lukaza na wenzao walikuwa wana smile tu ....jamani ...mmmmmhhh sasa embu tutatfute njia nyingine ya kupata mali zao na sisi tugawane.....mwenye mawazo anakaribishwa

  ANGALIZO
  ISIWE KUUA
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Nov 17, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,277
  Likes Received: 5,638
  Trophy Points: 280
  Kikwete amteua Msekwa kuongoza Mamlaka ya Ngorongoro[​IMG]Na Leon Bahati

  RAIS Jakaya Kikwete amemteua tena makamu mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa kuwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.

  Msekwa ataongoza bodi hiyo yenye wajumbe 11, wakiwemo wabunge watatu ambao ni mahiri kwa kujenga hoja bungeni.
  Wabunge hao ni Lucas Seleli (Nzega-CCM), Job Ndugai (Kongwa-CCM) na Halima Mamuya (Viti maalumu-CCM).

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk Ladislaus Komba alisema katika taarifa yake aliyoitoa jana jijini Dar es Salaam kwamba uteuzi wa Msekwa ulifanywa na Rais Kikwete Oktoba 5, mwaka huu wakati bodi hiyo imeteuliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga.

  Dk Komba aliwataja wakurugenzi wengine kuwa ni Emmanuel Lomayani (mwakilishi wa wafanyakazi Ngorongoro), Metui Ole-Shaudo (mwenyekiti wa Baraza la Wafugaji) na Donatius Kamamba (mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Kale).

  Wengine ni Deogratius Ntukamazina (katibu mkuu mstaafu, Utumishi), Yona Nnko (mkazi wa Arusha), George Kaindoh (mshauri mwelekezi) na mjumbe mwingine ambaye jina lake halijatajwa ambaye atatoka Jeshi la Polisi. Kulingana na uteuzi huo, Katibu wa Bodi ataendelea kuwa mhifadhi mkuu wa Mamlaka ya Ngorongoro ambaye ni Bernard Murunya.

  YALE YALE
   
Loading...