Lindi na Mtwara wameshalipiza kisasi

Lindi na Mtwara wameshalipiza kisasi

Pole kiongozi, binafsi naona ndani ya sisiem umebaki peke yako unaoumizwa na utendaji wa chama chako.
1. Ulikataa kwenda arusha mwaka jana na ulisema kwa nini huendi.
2. Ulisema pia baada ya ziara yako ya nyanda za juu kusini na mitaa hiyo ya Mtwara na Lindi.
Pia mengi tu umekuwa muwazi kulingana na hali halisi.
Lakini kauli za Mwenzio Nape huwa unazisikia? Kejeli zako je? Matusi yake kwa wapinzani na kusema shida za watanzania je? Katembea karibu nchi nzima kwa kodi zetu huku akitutukana. Lini uliwahi kumuona akikubali kuwa hali ni mbaya kwa chama chenu? Juzi wakati anafunga kampeni ulisikia kauli yake?
Ushauri wangu kwako ni kuangalia ustaarabu wa nini cha kufanya, kama unaona gari hiyo ya miaka ya 70 inakusumbua nunua nyingine ya kisasa na hiyo paki mahala au tupa huko iwe screpa.

Hali ni tete huko Lindi na Mtwara kwa CCM. Matokeo yanayotufikia hapa Ofisi Ndogo za Chama,Lumumba si vutizi. UKAWA wametupoka sehemu nyingi huko.CUF imetamalaki. CUF imetetea mitaa yake na kupoka mingine toka CCM.Wana-Lindi na Mtwara hatimaye wamelipa kisasi na kuonesha kinyongo chao juu ya sakata la gesi asilia.

Kipigo cha gesi kimejibiwa na kipigo cha kura. Sijui mwakani itakuwaje. Wana-Lindi na Mtwara tusameheni jamani.Tuliteleza.Hatutarudia tena.Safari hii mkiliona jeshi huko basi liko Kambini au limekuja kujenga madaraja na miundombinu mingine.

Kujikwaa si kuanguka.

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Nyumbani kwa Makongoro Mahanga Kata ya Segerea diwani ni wa Chadema na jana mwenyekiti ameshinda wa Chadema na wajumbe wake.

Kata ya Kitunda mitaa yote Chadema, Mtaa anaoishi Meya wa Ilala Jelly Silaa ni Chadema. Kama kawaida wana ngangari CUF wameonesha umwamba wao Buguruni.
 
Tuliwaambia Lumumba kwamba chama cha siasa si majengo bali ni kukubalika kwa sera za chama husika kwa wananchi - wakatubishia, tena wakatubeza na kuendelea na tabia yao ya somba-somba watu kwa malori na mabasi kwenda kwenye mikutano yao huku wakigawa fulana, kofia na wali - pamoja na burudani kede kede toka kwa wasanii maarufu eti hiyo ndiyo njia yao ya kuzinadi sera zao.

Sasa ngoja tuone mwenezi wao atakuja na PAUKWA gani kuhusu pigo hili la uchaguzi.
 
Hongera sana CUF ,CDM ACT NA NCCR Hongera ukawa hongera ccm hongera tanzania nchi yangu itaanza siasa za kweli kama kenya tutakuwa na bunge alilotaka mwalimu nyerere lenye upinzani na wajumbe weledi 2015
 
Kama ubongo wake ndo unatumika kufikiri atakuwa amekuelewa vizuri na tutegemee yeye kubadirika.
Rudia yale maneno yako ya kipuuzi chopa tatu sijua viti vitatu kwenye lile daftari chovu ambalo kura za marehemu zote walipewa ccm. Hivi mlikuwa hamuoni aibu sehemu yenye wapiga kura elfu 90 wapige kura watu elfu 20 na mgombea wa ccm kuibuka na ushindi wa kura elfu8!? Katafute kazi halali muda wa wewe kuendelea kutetea upuuzi karibu utaisha na utaishi kwa jasho sio kwa ujanja ujanja wa kutembea na mihuri fake ya ikulu huku ukipata kapato haramu. Kuanzia 2016 kama hutatumia hela zako vizuri kufungua mradi endelevu ujue uzee utakuwa mtu wa kulia shida na kuacha laana tu. Wewe endelea kwenda kwenye mabar jioni kwa hela za kifasadi ila uzeeni ndio utapata majibu yake. Halafu zile propanda za kitoto hata wabunge wenu eti walikuwa wanazitumia kama sehemu ya nyinyi kukubalika. Matokeo yake wakaenda kuandika katiba ya kipuuzi kabisa kwani walijua wataendelea kukaa madarakani milele. Kwa matokeo ya jana tunajua bado ccm itakuwa juu lakini katika hali ya uchovu kabisa, yaani hamasa iliyopo mtaani wale watu ambao hawakujiandikisha kupiga kura mpaka wanajilaumu kwanini hawakujiandikisha au kupiga kura. 2015 tegemea bunge lenye 50/50 ya upinzani na ccm hapo mikataba ya siri yote lazima ije hadharani mbona wafadhili wako watakaa. Katafute kazi halali narudia tena.
 
Msimbati ndiko wamefunga KAZI MOJA KWA MOJA

WAMEPIGA CHINI CCM MAZIMA,,

SHENZY TYPE PANAPO UHAI TUTAKUTANA MWAKANI

ETI WANAKUJA NA GIA YA KUJIFANYA WANAMALIZIA BARA BARA YA NANGURUKURU HAISAIDII HIYO.

LETENI WANAJESHI WAPIGE KURA SASA

LAZIMA TUWAFUNZE ADABU SAFARI HII

Hongerea Brother yangu.Wajua na hapa mizengwe kibao,nawaza kwa sauti hivi ingekuwa ndani ya viwanja HURU ingekuwaje?
 
......ndiyo maana walianza kuwaengua wapinzani kihunihuni kwenye mapingamizi hewa.

Kweli kabisa. Ila hili nalo liwe ni fundisho kwa UKAWA. Next time, vijimakosa ''vya kizembe'' viepukwe ili CCM wasipate chance ya kupigia bao. Pia next time wasiachwe hawa wakapita bila kupingwa. Ni bora kusimika mgombea hata kama chances za kushinda ni ndogo. You never know.
 
mmepiga hatua 20 nyuma
mmeenda 2 nyuma halafu mnajipongeza hahahaaaaaaaa
ccm bwanaaaaaa
kusini tumewachokkaaaaaaaa

Hahahaa maa unanifurahisha!
Mwambie hyo wenzie wamekiri yy bado hataki!

Yaani mtaani kwangu dar tumechukua kote
Mtaani kwangu nilikokulia iringa hadi mama angu kwa mara ya kwanza kapiga kura na cdm imechukua....
Viva ukawa!
 
Huko kwenu wapi? Hakuna jina?

Mkuu Lizaboni ingawa tunakuelewe wewe mwelekeo wako ni upi lkn kumbuka mambo yameanza kufikia turning point. Kama umesoma hesabu basi unajua maana ya turning point! Kwa kifupi kwetu ni Mbeya kama hii ni muhimu zaidi kwako! Yaani hata wazee wanasema toka CCM ili tukupende zaidi!
 
Haydom, Getarer, Ngwandakw, maghang, harar, wote ni CDM
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom