Lindi na Mtwara wameshalipiza kisasi

Lindi na Mtwara wameshalipiza kisasi

Tunataka mtaje mshindi ni nani acheni usanii bado mna kazi kubwa kuitoa ccm
 
tunataka mtaje mshindi ni nani acheni usanii bado mna kazi kubwa kuitoa ccm

kaaa hivyo hivyo na ububusa wako na kwa mtwara mjini,tandahimba,na newala msahau kabisa madhalimu nyie
damu ya yule mama mjamzito mliempiga risasi pale magomeni mkamuua na mtoto alie tumboni itawahunt maisha yenu yote!!
 
Maneno mengi bila ya data hayasaidii

Rudia yale maneno yako ya kipuuzi chopa tatu sijua viti vitatu kwenye lile daftari chovu ambalo kura za marehemu zote walipewa ccm. Hivi mlikuwa hamuoni aibu sehemu yenye wapiga kura elfu 90 wapige kura watu elfu 20 na mgombea wa ccm kuibuka na ushindi wa kura elfu8!? Katafute kazi halali muda wa wewe kuendelea kutetea upuuzi karibu utaisha na utaishi kwa jasho sio kwa ujanja ujanja wa kutembea na mihuri fake ya ikulu huku ukipata kapato haramu. Kuanzia 2016 kama hutatumia hela zako vizuri kufungua mradi endelevu ujue uzee utakuwa mtu wa kulia shida na kuacha laana tu. Wewe endelea kwenda kwenye mabar jioni kwa hela za kifasadi ila uzeeni ndio utapata majibu yake. Halafu zile propanda za kitoto hata wabunge wenu eti walikuwa wanazitumia kama sehemu ya nyinyi kukubalika. Matokeo yake wakaenda kuandika katiba ya kipuuzi kabisa kwani walijua wataendelea kukaa madarakani milele. Kwa matokeo ya jana tunajua bado ccm itakuwa juu lakini katika hali ya uchovu kabisa, yaani hamasa iliyopo mtaani wale watu ambao hawakujiandikisha kupiga kura mpaka wanajilaumu kwanini hawakujiandikisha au kupiga kura. 2015 tegemea bunge lenye 50/50 ya upinzani na ccm hapo mikataba ya siri yote lazima ije hadharani mbona wafadhili wako watakaa. Katafute kazi halali narudia tena.
 
Maneno mengi bila ya data hayasaidii
mkuu tunajua unamahaba sana na ccm. ushauri wangu kama mtanzania mwenzako, hebu tuungane kuuondoa huu ujinga wa kubeba fedha zetu kwenye magunia wakati watanzania wenzetu hawana hata panadol mahosipitali wala maji majumbani.
sio kweli kuwa ccm wote ni wabaya wapo wazuri wengi tu lakini kwa mfumo uliopo hawawezi kupambana na uchafu unaofanywa na baadhi yao.
wewe mwenyewe utakuwa ni shahidi jinsi gani kodi zetu zinazoenda kwenye mahalmashauri lakini zinaishia kutafunwa na wenye meno kwenye vikao vya watendaji na hata wakijulikana wanahamishwa tu badala ya kuchukuliwa hatua za kisheria na kinidhamu.
kwa nia nzuri kabisa nakushauri hebu tuungane mkuu kuliokoa taifa hili kwa ajili ya vizazi vyetu vijavyo.
 
HUku kwetu watu hawataki kusikia kitu kama CCM! Wanathubutu kusema wewe ni ccm na kama binadamu tunakupenda lkn ondoka basi huko ili tukpende zaidi! Mambo ni magumu hasa vijijini ikizingatiwa kuwa vijana wamekuja juu sana!!

Ni Taarifa za kutia moyo! Hongereni sana tupo pamoja!
 
Hali ni tete huko Lindi na Mtwara kwa CCM. Matokeo yanayotufikia hapa Ofisi Ndogo za Chama,Lumumba si vutizi. UKAWA wametupoka sehemu nyingi huko.CUF imetamalaki. CUF imetetea mitaa yake na kupoka mingine toka CCM.Wana-Lindi na Mtwara hatimaye wamelipa kisasi na kuonesha kinyongo chao juu ya sakata la gesi asilia.

Kipigo cha gesi kimejibiwa na kipigo cha kura. Sijui mwakani itakuwaje. Wana-Lindi na Mtwara tusameheni jamani.Tuliteleza.Hatutarudia tena.Safari hii mkiliona jeshi huko basi liko Kambini au limekuja kujenga madaraja na miundombinu mingine.

Kujikwaa si kuanguka.

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
ccm wamezoea unafiki. kusema gesi ni mali ya taifa sio ya wanamtwara peke yao haikua kosa. sasa kama wananchi wamekasirika na kuwabwaga kwenye uchaguzi ni kwa ajili ya dhambi nyingine nyingi za ccm.
 
Tunataka mtaje mshindi ni nani acheni usanii bado mna kazi kubwa kuitoa ccm

Unachosema ni kweli kuna kazi kubwa ya kuitoa ccm madarakani, na inafanyika, nyie laleli tu mkifikiri kuna kazi kubwa sana, kumbe kazi iliyoback ni kidogo. Chapeni usingizi mazee. Nakumbuka nilikuwa nafanya kazi nmb, akanya expert mmoja akasikia ile slogan ya nmb kwamba wameenea tz mzima, yule jamaa akasema that is not an issue, in 5 years, crdb will be in every corner of tz, of which is true at this moment.
 
Msimbati ndiko wamefunga KAZI MOJA KWA MOJA

WAMEPIGA CHINI CCM MAZIMA,,

SHENZY TYPE PANAPO UHAI TUTAKUTANA MWAKANI

ETI WANAKUJA NA GIA YA KUJIFANYA WANAMALIZIA BARA BARA YA NANGURUKURU HAISAIDII HIYO.

LETENI WANAJESHI WAPIGE KURA SASA

LAZIMA TUWAFUNZE ADABU SAFARI HII
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom