Limeshawahi kukutokea hili?

Limeshawahi kukutokea hili?

Nyalotsi

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2011
Posts
6,989
Reaction score
5,066
Nakumbuka nilikuwa na miaka mitano kituko hiki kilivyotokea. Siku hiyo alikuja mgeni toka Mbeya na debe la mchele. Wali ulipikwa siku hiyo tofauti na tulivyozoea kwani ilikuwa ni wakati wa sherehe tu.! Chezea wali wa sikukuu wewe!! Basi kaka yangu aliyenitangulia alikula siku hiyo mpaka akavimbiwa. Usiku bwana!! Si akatoa haja kubwa kitandani! Nilipozidiwa na harufu nikahamia wanakolala kina sister. Mpaka leo tukirudi home huwa namtania wali ukipikwa.! Je umewahi kutana na vituko vya aina hii ukiwa mdogo?
 
yaani aliangusha zigo kitandani...huo wali ulipikwa kwa kuchanganywa na vilegeza bolt za makalio au?
 
Mim nakumbuka walipika wali nyama hapo kijiji kipindi hicho...basi mim nilikuwa kwa shangaz yngu baba na mama wakamwambia mdogo wangu nikija anipe chakula,sasa kumbe yy akaamua kula nyama yote na wali akabakisha mchuzi na ukoko...mimi narudi akaniambia hicho ndio nilichobakishiwa nilisikia uchungu kukosa nyama,waliporudi wazaz nikawaambia wameninyima nyama na wali na kunibakishia makombo.,si ndo DINGI akaniambia ukweli duh!dogo wangu alipata kichapo cha kikwelikweli mpaka leo ananikumbushia alivyonifanyia umafia tena ameshaoa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom