mayowela
JF-Expert Member
- Nov 2, 2014
- 2,124
- 1,746
Jina la kitambulisho Ommary Rajabu Saleh Tambwe al maarufu Lilommy jamaa yuko kwenye tasnia kwa muda tangu enzi yuko Voice of Tabora (V.O.T) fm, Kiufupi anakipaji cha kutangaza,production,Graphix design, kuchana (kurap) kiufupi kajaaliwa
Nakumbuka kipindi yuko Tabora alikuwa ni Dj baadae akaanza kutangaza kipindi cha mchana cha Bongo Rhymes then akakibadili jina na kukiita Extra ordinary pia alikuwa na studio kama sikosei ilikuwa inaitwa Lunatic production.
Miaka ya 2008-2009 alipata ubalozi kutoka mtandao wa simu wa Zantel na hapo ndipo mambo yalianza kubadilika, kama masihala akaibuka mjini na milango ikafunguka zaidi pale Times fm, na kwa sasa ni moja kati ya watangazaji wa moto sana anazidi hadi wale walioko kwenye media kubwa ambao wengi wao majina yana wabeba na sio kipaji halisi.
Wengi wanaweza wakawa wamekuona na wakahisi sehemu ulipo sio sahihi, mimi nasema Times ni sehemu sahihi kwa sasa sidhani kama una nafasi ya utangazaji tu pale naamini una nafasi ingine pia ki utawala, Endelea kujenga jina na ipo siku wasio kuelewa watakuelewa ikiwa muda umewatupa mkono.
Ongeza chochote kwa Lilommy, wakuzua aka wamacausative aka ORST the king of Saturday show The PlayList