Lijuakali kawaangusha wabunge vijana

Zawadi Ngoda

JF-Expert Member
Aug 13, 2009
3,768
1,817
Lijuakali kaonyesha udhaifu mkubwa sana katika hotuba yake bungeni na katika andiko lake juu ya kupatikana kwa ubunge Wake Kilombero 2015 humu JF.

Nikianza na mchango Wake bungeni: Katika mchango Wake kaonyesha hana ujasiri wa kukabiliana na mitikisiko ambayo kwenye siasa ni vitu vya kawaida. Katika dakika takriban 10 alizozungumza kama nisingetajiwa umri Wake ningedhani ana umri wa miaka 11 - 16. Ameuhakikishia umma kuwa aligombea ubunge wa Kilombero kwa lengo la kutafuta ajira tu na sio kuwapigania wananchi. Anasema, ah hata boda boda nitaendesha- kwani aliambiwa kuwa kuendesha boda boda ni dhambi au hao wanaofanya kazi hiyo sio binadamu? Kawadharau vijana wote kwa kudhani kuwa kupata ubunge amepanda daraja la kutofanya kazi nyingine kama boda boda, ukulima, biashara nk.

Hii imedhihirisha kuwa alikinzana na wenzake kwenda bungeni kwa ajili ya POSHO TU. Na kinachomtisha zaidi ni kuelewa kuwa CHADEMA haitamsaidia tena kupata ama udiwani ama ubunge kama si kumtosa. Na biashara ya CCM ya kununua wabunge wa upinzani imefungwa, hivyo kilichobaki ni kumuomba Ndugai ampokee kwa kumuonea huruma bila masherti yeyote yale-buree, huku akitoa machozi danganya.

Kuhusu andiko lake humu JF kaeleza mengi, lakini kubwa ni moja tu kuwa kushinda kwake kulitokana na DC, OCD nk kuwa watu wa Lowasa waliopata maelekezo toka kwa Lowasa na kuyatekeleza. Kama hivyo ndivyo basi kaitukana zaidi CCM kuliko alivyodhani kuwa kaivua nguo CHADEMA. Kwa maana kwa mfano kuelekea uchaguzi 2020 ma-DC, OCD wataje tu mpaka umalize wamechaguliwa na Mwenyekiti wa CCM.

Kwa hiyo kama formula ya mahesabu itakwenda kama yeye alivyosema, inamaanisha chaguzi zote CCM inashinda kwa sababu, hao wazito wote huteuliwa na Mwenyekiti wa CCM/Rais. Arudi nyuma na kujitafakari kauli zake, kwani akutukanae hakuchagulii tusi. Mbaya zaidi anawatukana watu ambao leo amewamba wampokee/ CCM.

Huyu kijana hakustahili kuwa mbunge, kwani anawashushia hadhi wabunge wote vijana. Anatakiwa awaombe radhi vijana wote mara moja.
 
Chadema Ile gia angani sasa ndio inawamaliza taratibu.

Tatizo sio gia angani, tatizo ni mfumo uliopo sasa hivi si rafiki kwa vyama vya upinzani. Ila haya yote ni maswala ya muda tu, kwani hata Ethiopia waliwabana wapinzani lakini haikuwasaidia. Sasa hivi wameruhusu tena demokrasia itawale.
 
Tatizo sio gia angani, tatizo ni mfumo uliopo sasa hivi si rafiki kwa vyama vya upinzani. Ila haya yote ni maswala ya muda tu, kwani hata Ethiopia waliwabana wapinzani lakini haikuwasaidia. Sasa hivi wameruhusu tena demokrasia itawale.
Mfumo unamapungufu yake, ila Chadema hawawezi kukwepa lawama kwenye hili.
 
labda upendeleo wa viti MAALUM ndio stahiki iliyobakia kwenye siasa zake

pia atunze mafao yake na aanze kuwekeza kwenye kuku,bodaboda na kulima bustani kama alivyodhihaki wakati anajitabiria!

kuna nazi na koroma

kauli zake zinamtia kwa quarantine ya muda mrefu kisiasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
labda upendeleo wa viti MAALUM ndio stahiki iliyobakia kwenye siasa zake

pia atunze mafao yake na aanze kuwekeza kwenye kuku,bodaboda na kulima bustani kama alivyodhihaki wakati anajitabiria!

kuna nazi na koroma

kauli zake zinamtia kwa quarantine ya muda mrefu kisiasa

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwa jinsi nilivyomsikiliza, uwezo huo hana, sijui CHADEMA waliwezaje kumpitisha kugombea nafasi kubwa kama hiyo. Nafikiri sasa hivi hata senti tano hana atadai kuwa fedha zote kakatwa na Chama.

Siku zijazo CHADEMA ifikirie vizuri katika uteuzi hasa kwa wagombea wa ubunge hata viti maalum.
 
Chadema Ile gia angani sasa ndio inawamaliza taratibu.

..Lijualikali angeenda nccr, cuf, au act.

..lakini kujisalimisha kwa walewale waliomfunga kwa hila na uonevu kunaleta ugumu kumuamini, na ukakasi ktk hoja zake.

. Lijualikali analia akikumbuka alivyoteswa gerezani. Sasa ni chama gani kilichosababisha akafungwa kama siyo ccm, polisi, na mahakama zake?

..Na ni chama gani kilimpigania mpaka akatoka kifungoni? Siyo cdm chini ya mwenyekiti Mbowe? Na rasilimali za chama gani zilitumika kumtoa jela alikokuwa akiteswa?

..Sina tatizo ni wanasiasa kuhama vyama, lakini ingependeza kama wangetoa sababu za kueleweka na zenye mantiki.
 
Na Chadema kila siku wanasaliti tu
Labda chedema ndo kinawaangusha hawa vijana
Hivi kweli wewe unaona mazingiza ya demokrasia yalivyo awamu hii? Ni ajabu kwamba hata vyama vya upinzani bado vipo. Itawachukua Watz miaka mingi sana kuweza kuruhusu chama kingine kitawale.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom