Life begins at 40 Vs Midlife crisis

Kuhusu kujenga huwa naona watu wanajibana sana, kwanini ukimbilie kujenga?? Mimi binafsi huwa sioni sababu ya kujenga mapema, labda nitajenga nikiwa hapo kwenye 40 - 45. Ukishayapangilia vyema maisha yako around 27 - 30 ukajua either nahitaji kuwa na familia au la, nahitaji kujenga nikiwa na 40 yrs au la, Career yangu ni hii au la etc then maisha yako ukiwa 40 yrs natumaini yatakua matamu sana
 
Yeah, walioishi kipindi kazi zikitafuta wat(80s na early 90s) hawawezi kuelewa.
Na ubaya huwa wanalaumu na kuwatukana wale walioshindwa kwa kutumia reference ya enzi zao bila kujua kuwa, ni kukosa kwao maono ndiko kumesababisha haya yote

Ila ubarikiwe sana mkuu, japo siwezi slow down kwa ninachokipigania lakini mada yako imenipa picha nyingine about life ambayo huwa tunapewa kwa nadra sana na watu wa umri wako mtaani. πŸ™πŸ½πŸ™πŸ½πŸ™πŸ½
 
πŸ˜‚ wanasema kwanini ujenge na una uwezo wa kulipia kodi bila kusumbuka?

Ila je, ukijakata moto ghafla, utaachaje mke na watoto?
 
Well said mkuu kuna nilivyong'amua hapa nitavipa kipaumbele
 
Sijasema at 46 umezeeka, ila wanasema umri huo upo katikati ya lifespan yako, nguvu na akili zipo kwenye peak yake.

Tatizo ni kujipanga hasa ukiwa kijana, kuna vitu vya msingi mtu anatakiwa kuviangalia ili mambo yasije kuwa mengi katika umri fulani.
Nimekuelewa Boss
Ni kweli kujipanga ni muhimu huku ukiomba yaende unavyotarajia ila yakibadilika pia ndio hivyo tena
Maisha hayatabiriki kwa kweli ila malengo muhimu sana na akiba muhimu pia
 
Niko naelekea kumaliza phase 2 kuingia ya phase ya 3 lakini kwa navyoona hi phase ya 3 inanibidi nipambane sana nafuture nashukuru Mungu kwenye hii phase ya 2 issue ya kusoma soma naimaliza hapa atleast I have ka degree kah mchongo pia inshallah kabla mwaka ujaisha ntapata kakijana kangu kah Nkundwe Jr
 
Imagine upo 40s, umebarikiwa watoto watatu, wote wanaenda shule na wana mahitaji yao ya msingi huwezi kuwanyima. At the same time kuna majukumu ya familia yako na yake, then unaishi kwa kupanga, unafanya mchakato wa kujenga. Katika situation ya namna hiyo, crisis unaikwepaje?
 
Furahia kila siku Mungu anapokupa zawadi ya uhai.

Future na kesho yako iko mikononi mwa Mungu.

Kuna watu wana kila kitu leo jumapili familia zinakwenda kuwatembelea magerezani.

Ukiishi kama mpagani ndio utababaishwa na swala la umri.

Kwanza Bongo kwa kipato halali bila kufika miaka 50 plus hutoboi ng'oo utapata pesa ya kula tu na kuhifadhi matofali yasiibiwe.
 
πŸ˜‚ wanasema kwanini ujenge na una uwezo wa kulipia kodi bila kusumbuka?

Ila je, ukijakata moto ghafla, utaachaje mke na watoto?
πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ Kuna mahali nimeweka pesa za mtoto wangu + mafao yangu ni yake, kuhusu mke nilisha decide sina plan ya kuwa na mke. Nikikata moto ghafla i hope sitaacha migogoro duniani
 
I think hii inawahusu walio na ndoto za kuoa na kua na watoto watatu, Mimi binafsi sina plan ya kuwa na mke, mtoto mmoja tu ananitosha
 
πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ Kuna mahali nimeweka pesa za mtoto wangu + mafao yangu ni yake, kuhusu mke nilisha decide sina plan ya kuwa na mke. Nikikata moto ghafla i hope sitaacha migogoro duniani
acha uroho mkuu... Inatakiwa kidume ukifa watu wagombanie mali... Sio msiba mtu unakufa wanahudhuria watu 20 [emoji23] af wanagawana nguo[emoji23] Aaah sio uanaume banaaa...
 
Ukajiombee mkuu wangu, ukiwaachia kazi ya kukuombea, watakuimbea yakuharibikie, udhalilike🀣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…