Elections 2015 Licha ya kukubalika, Jina la Lowassa halitafika hata CC!

11080930_650069158453801_2509018049611795371_n.jpg

mkuu nasikia wewe ndio yule aliyekua anaandika zile articles zilizowai kusisimua za HUTAKI UNAACHA tupe muendelezo basi wa wale waliobaki mkuu
 
Tafadhali nisaidieni kuwajua wajumbe wa kamati ya Maadili ya CCM ... Naona wanatumia nguvu kubwa sana kumtosa Lowassa bila mafanikio!!! Sijui yeye akiaanza kuwatosa wapinzani wake itakuwaje ...
 
Wameshindwa kumfungulia mashtaka bado wanalia kuwa ni mwizi.Wana tume ya maadili walishindwa kumtupa nje ya chama ,lakini wanabweka kama mbwa asiye na meno japo wana meno yenye ncha kali.Lakini wanaimba kwa sauti kubwa eti wanatawala nchi kwa haki na utawala bora na kisheria.Labda zipo chuki binafsi na kuendekeza majungu kama mbinu za kupakana matope.Je mwananchi wa kawaida asiye na rungu ya serikali au mahakama au kigogo kwenye chama chao CCM achukue lipi na aache lipi?Mchezo huu hausaidii taifa au CCM.Tunataka maelezo kwa kina sio vichwa vya habari tu.Mwisho wa siku tunataka kuchagua raisi bora sio bora rahisi.

Mkuu umeongea kwa uchungu sana usijali iko siku watanzania wataujua ukweli nimewai kukaa private akaniambia hii nchi itakua ya asali na maziwa soon
 
..hivi Mkapa naye akiwa Raisi na Mwenyekiti wa CCM si alijiapiza kwamba atawakomesha wanamtandao?

..nini kilimtokea na dakika za mwisho kabisa akabadili msimamo na kumuunga mkono mgombea "anayependwa" na wananchi?

..najua CCM imepata kuwaengua watu wazito kama Cygwiyemwisi John Malecela, lakini sidhani kama Lowassa na wanaomuunga mkono are push overs kama Malecela.

cc Nyamizi, Pasco

Asante Mkuu JokaKuu kwa kutukumbusha kilichotokea back in 2005.Hawa Pro- Membe wanadhani sisi ni wajinga sana na tunaweza kutishwa na simple arguments za eti "Ridhiwan kaapa" who is Ridhwan by tha way? Kama kuna Mwenyekiti wa chama niliwahi kuamini ana msimamo dhabiti ukiondoa Mwl Nyerere,nilidhani alikuwa Mkapa,guess what? I was totally wrong,alisalimu amri kwa wanamtandao dakika za mwisho na akakubali yaishe.Sasa sijui hawa wanaokuja na hadithi za Ridhiwan kaapa kuhama Nchi EL akiwa mgombea wa Rais wanamtisha nani? Kwani Ridhiwan ndio ana hati miliki ya Nchi hii and he can decide who is the next President? EL wanae mpaka hatua za mwisho,waendelee kuhangaika nae huku sisi tunawasubiri na Mgombea wetu wa UKAWA.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu ulivyoipamba post yako utadhani unaemwandikia ndiye mgombea wa UKAWA!?kweli nimeamini sasa EL akipita hakuna UKAWA!
 
Last edited by a moderator:
Wanabodi,

Lengo la hujuma hiyo ni kufuatia Lowassa kukubalika kupindukia, jina lake likifika tuu CC, hakuna wa kumkata, hivyo wahafidhina wa CCM, wanaounga mkono kambi ya mmoja wa wagombea, wameapa kuhakikisha jina la Lowassa, halivuki kisingiti cha kamati ya maadili, hivyo kumchinjia rasmi baharini, ili mgombea wao apete kwa mteremko!.

Pasco
[h=3][/h]
Ili kuondokana na Kisingiti hii na muamvuli huu wa Uvyama. Kuna haja wapenda haki kufungua Kesi ya Kikatiba kwa Hati ya dharura-huu ndio muda na wakati wa Mgombea Binafsi kurudi kwenye historia ya Nchi yetu.

Waheshimiwa wote wenye kutishwa na Vyama vyao pambaneni kutafuta na kuipata haki hii ya Kikatiba.

[h=3]Mwalimu Nyerere na mgombea binafsi | Gazeti la Jamhuri[/h]
Tujifunze kutoka historia ya uchaguzi wa mwaka 1961.
Sasa mfano mmoja nautumia mwisho kabisa. Mwaka wa elfu moja tisa mia na siti na moja tulikuwa na uchaguzi mkuu. Akatupinga kijana wetu mmoja anaitwa Herman Sarwatt. Ndiyo, si ulikuwa uchaguzi wa vyama vingi? TANU ilikuwa imechukua viti vingi bila kupingwa. Kiti cha Mbulu tulikuwa tumemweka chifu mmoja anaitwa Chifu Amri Dodo. Mwanàchama wetu mmoja alikuwa anaitwa Herman Sarwatt akasema. Alaa! Hiki chama changu hakina akili hata kidogo. Hawa viongozi wangu hawana akili! Hawa machifu ndiyo zamani wakitaka kutufunga wakati tukigombana na mkoloni. Leo wanamchukua Chifu Dodo aliyetaka kutufunga sisi ndiye awe mbunge wetu katika jimbo la Mbulu?
Sasa sisi tulikuwa tumekwisha kumchukua huyu kuwa ndiye mgombea rasmi wa TANU. Kijana yule akatupinga. Mimi nilitokea hapa Mbeya na nikasafiri kutoka Mbeya kwenda Mbulu kumtaiti yule mgombea wa TANU. Nikashindwa.
Wananchi wa Mbulu hawana uanachama tena, wengi tu wakasema ‘TANU wamekosea’. Wakampa kura Sarwatt. Wakafanya hivyo, mwanachama wa TANU akasimama mwenyewe akatushinda! Ilikuwa haki yake. Hatukuiondoa.

Asante Mkuu JokaKuu kwa kutukumbusha kilichotokea back in 2005.Hawa Pro- Membe wanadhani sisi ni wajinga sana na tunaweza kutishwa na simple arguments za eti "Ridhiwan kaapa" who is Ridhwan by tha way? Kama kuna Mwenyekiti wa chama niliwahi kuamini ana msimamo dhabiti ukiondoa Mwl Nyerere,nilidhani alikuwa Mkapa,guess what? I was totally wrong,alisalimu amri kwa wanamtandao dakika za mwisho na akakubali yaishe.Sasa sijui hawa wanaokuja na hadithi za Ridhiwan kaapa kuhama Nchi EL akiwa mgombea wa Rais wanamtisha nani? Kwani Ridhiwan ndio ana hati miliki ya Nchi hii and he can decide who is the next President? EL wanae mpaka hatua za mwisho,waendelee kuhangaika nae huku sisi tunawasubiri na Mgombea wetu wa UKAWA.
Kumbe ni walewale! Lowasa naye kajiunga na ukawa?
 
Lowassa ni mwizi hafai kuwa kiongozi. Lowassa ni fisadi hafai kuwa kiongozi, huko kupendwa na wengi siyo bali ananunua kupedwa

Uthibitisho khs kauli yako tafadhar usiamin kila unachoambiwa, akili ya kuambiwa changanya na ya kwako ndg,kununua watu hayo maneno yanasemwa na mahafidhina wasiolitakia mema taifa letu
 
Watanzania wa leo wemeelika wameerevuka, lakini wakimpa lowassa Ikulu ntaamini Taifa hili ni kichwa cha mwendawazimu
 
Nyamizi,

..lakini usiwategemee sana hawa wa-Tz.

..hawaeleweki wanataka nini haswa.

..UKAWA wana kazi kubwa kwelikweli bila kujali CCM watamsimamisha nani.

cc Gagnija
Kwenye uchaguzi wa mitaa uliopita wameonyesha wanachokitaka. Kile kilichoelezwa na serikali kwamba ni dosari na hivyo kuahirisha uchaguzi hazikuwa dosari. Ni baada ya kubaini kipigo walichokuwa wanakwenda kukipokea hivyo wakapanga namna ya kuepuka aibu. Oktoba ni kiama kwa watawala wa sasa.
 
wanabodi,

hii ni tetesi ya habari mbaya kwa wapenzi wa kipenzi cha watu, waziri mkuu mstaafu, edward lowassa kuwa pamoja na mhe. Lowassa kuwa ndie mtu anayekubalika sana kuliko mtu mwingine yoyote ndani ya ccm, wale wasiolitakia mema taifa hili, wamepania kupanga njama za kumhujumu kwa kuhakikisha kuwa jina lake halitaingia hata ndani ya kikao cha cc kujadiliwa!, wamepanga kumchinjia baharini kwenye kamati ya maadili, itakayoyajadili majina wagombea kabla ya kuyaingiza kwenye kamati kuu, kujadiliwa!.

Lengo la hujuma hiyo ni kufuatia lowassa kukubalika kupindukia, jina lake likifika tuu cc, hakuna wa kumkata, hivyo wahafidhina wa ccm, wanaounga mkono kambi ya mmoja wa wagombea, wameapa kuhakikisha jina la lowassa, halivuki kisingiti cha kamati ya maadili, hivyo kumchinjia rasmi baharini, ili mgombea wao apete kwa mteremko!.

Naomba nisitaje chanzo cha habari hizi, kwa kutumia kanuni ya "the confidentiality of the source"
ila kwa vile hizi ni tetesi tuu, zitakapothibitika ndipo nitaweka source!.

Kama kawaida yetu jf, habari kama hizi ambazo hazijathibitishwa, zimeletwa humu hivi hivi zilivyopokelewa, ili wewe kama mwana jf, be the first to know!, na information is power!, hivyo kutoa fursa kwa wenye uwezo wa kuizuia hii mipango dhalimu inayopangwa, kutaka kuwakosesha watanzaia mgombea kipenzi chao, chaguo la wengi, na mwenye uwezo usio tia shaka kuyamaliza matatizo yote ya taifa letu tanzania.

Hii ni thread ya info tip, tuu, hivyo naomba nisiulizwe swali lolote kuhusu hii news tip for your info tuu.

Nb. Chama cha mapinduzi ni taasisi huru yenye uwezo wa kufanya shughuli zake kwa uhuru vile ambavyo wataona wenyewe inafaa, ikiwemo vigezo na jinsi ya kuwachagua wagombea wake, ila kwa sisi ambao ni wakereketwa wa mustakali mwema wa nchi hii, kamwe hatutakubali, kuona watu wenye uwezo na wanaokubalika na wengi, wakienguliwa kwa mizengwe tuu, kitu ambacho ccm imekuwa ikikifanya mara nyingu huko nyuma na labda ni kweli ndicho walichopanga kukifanya mwaka huu!, yaani ccm imekuwa ikiwaengua wagombea wazuri kwa mizengwe na ikabaki salama!, lakini this time, nimewasikia baadhi ya wana ccm kindakindaki, kuwa wamejiapiza, this time ccm ikimuengua chaguo lao kwa mizengwe, patachimbika!.

Pasco
ngoja sheria ya makamba iipite....
 
Wanabodi,

Hii ni tetesi ya habari mbaya kwa wapenzi wa kipenzi cha watu, Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa kuwa pamoja na Mhe. Lowassa kuwa ndie mtu anayekubalika sana kuliko mtu mwingine yoyote ndani ya CCM, wale wasiolitakia mema taifa hili, wamepania kupanga njama za kumhujumu kwa kuhakikisha kuwa jina lake halitaingia hata ndani ya kikao cha CC kujadiliwa!, wamepanga kumchinjia baharini kwenye kamati ya maadili, itakayoyajadili majina wagombea kabla ya kuyaingiza kwenye Kamati Kuu, kujadiliwa!.

Lengo la hujuma hiyo ni kufuatia Lowassa kukubalika kupindukia, jina lake likifika tuu CC, hakuna wa kumkata, hivyo wahafidhina wa CCM, wanaounga mkono kambi ya mmoja wa wagombea, wameapa kuhakikisha jina la Lowassa, halivuki kisingiti cha kamati ya maadili, hivyo kumchinjia rasmi baharini, ili mgombea wao apete kwa mteremko!.

Naomba nisitaje chanzo cha habari hizi, kwa kutumia kanuni ya "the confidentiality of the source"
ila kwa vile hizi ni tetesi tuu, zitakapothibitika ndipo nitaweka source!.

Kama kawaida yetu jf, habari kama hizi ambazo hazijathibitishwa, zimeletwa humu hivi hivi zilivyopokelewa, ili wewe kama mwana jf, be the first to know!, na information is power!, hivyo kutoa fursa kwa wenye uwezo wa kuizuia hii mipango dhalimu inayopangwa, kutaka kuwakosesha Watanzaia mgombea kipenzi chao, chaguo la wengi, na mwenye uwezo usio tia shaka kuyamaliza matatizo yote ya taifa letu Tanzania.

Hii ni thread ya info tip, tuu, hivyo naomba nisiulizwe swali lolote kuhusu hii news tip for your info tuu.

NB. Chama cha Mapinduzi ni taasisi huru yenye uwezo wa kufanya shughuli zake kwa uhuru vile ambavyo wataona wenyewe inafaa, ikiwemo vigezo na jinsi ya kuwachagua wagombea wake, ila kwa sisi ambao ni wakereketwa wa mustakali mwema wa nchi hii, kamwe hatutakubali, kuona watu wenye uwezo na wanaokubalika na wengi, wakienguliwa kwa mizengwe tuu, kitu ambacho CCM imekuwa ikikifanya mara nyingu huko nyuma na labda ni kweli ndicho walichopanga kukifanya mwaka huu!, yaani CCM imekuwa ikiwaengua wagombea wazuri kwa mizengwe na ikabaki salama!, lakini this time, nimewasikia baadhi ya wana CCM kindakindaki, kuwa wamejiapiza, this time CCM ikimuengua chaguo lao kwa mizengwe, patachimbika!.

Pasco
Mimi navyoona ni Lowassa anayetumia nguvu kubwa sana dhidi ya wenzake. Humu JF watu wote ni against Membe, against January against Pinda yaani zinatungwa hadithi hadi Wachungaji kuzua hoja dhidi ya mtu yeyote anayesimama dhidi ya Lowassa maana wameisha lewa na nguvu ya kiza.

Nitakuwa mpumbavu nilioje, nikiamini kwamba Lowassa anaonewa ikiwa magazeti yote nchini ni Lowassa, wanamuziki Lowassa, wachekeshaji Lowassa, makanisani na misikitini Lowassa..yaani huyu Lowassa anapendwa kama Katiba ya Wananchi (tume ya Warioba). Halafu hao hao wanakuja sema Lowassa anatengwa. Ama kweli Miafrika Ndivyo Tulivyo!
 
Atakayetaka kuona ccm inawekwa jumba la makumbusho
milele amuengue EL.2015 ni wazi EL hakwepeki iwe kupitia upinzani
au ccm yenyewe,sababu ni kwamba kwa jinsi alivyopita kwenye mikikimikiki
ataiweza tanzania tuitakayo.
Kwa mawaziri wakuu tuliowahi kuwa nao ukimuondoa sokoine hakuna anayemfikia EL kiutendaji japo alitumika muda mfupi sana.
Hivyo ataiweza TZ.
 
Daah,nimekuelewa mkuu huyu Lowasa asipopitishwa patachimbika ccm,ngoja tuone itakuwaje ila jina lake likipitishwa hana haja ya kufanya kampeni
 
Kwenye uchaguzi wa mitaa uliopita wameonyesha wanachokitaka. Kile kilichoelezwa na serikali kwamba ni dosari na hivyo kuahirisha uchaguzi hazikuwa dosari. Ni baada ya kubaini kipigo walichokuwa wanakwenda kukipokea hivyo wakapanga namna ya kuepuka aibu. Oktoba ni kiama kwa watawala wa sasa.

..na sisi tunawaombea iwe hivyo.

..itokee kama Nigeria ambapo chama tawala wamepata kipigo mpaka mgombea wao akasalimu amri kabla hata tume ya uchaguzi haijamaliza kuhesabu kura zote.
 
Mkandara,

..hii michezo Lowassa alianza kuifanya tangu mwaka 95.

..alipumzika hapa katikati ili kumpa nafasi JK kwa "makubaliano" maalum.

..sasa this time inaonekana Lowassa doesn't wanna take any chances.

..hivi kipenga hakijapulizwa mambo yako hivi. wakiruhusiwa ku-campaign itakuwaje?

cc Pasco, Gagnija, Nyamizi
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom