Licha ya changamoto za biashara duniani, biashara kati ya China na Afrika yaimarika na kuchochea maendeleo ya Afrika

Licha ya changamoto za biashara duniani, biashara kati ya China na Afrika yaimarika na kuchochea maendeleo ya Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,242
Reaction score
1,212
VCG111573521382.jpg


Kuyumba kwa biashara duniani kutokana na vita ya ushuru iliyozushwa na Rais Donald Trump wa Marekani, uhusiano wa kibiashara kati ya China na Afrika umekuwa unaendelea vizuri, na thamani ya biashara kati ya pande hizo mbili imeendelea kukua kwa miaka 16 mfululizo, na mwaka jana thamani hiyo ilifikia rekodi ya dola bilioni 295.6, likiwa ni ongezeko la asilimia 4.8 kwa mwaka, huku ushirikiano kwenye maeneo muhimu kama vile uwekezaji, viwanda na teknolojia ukiendelea kuongezeka.



Maonesho ya 4 ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika yamefanyika hivi karibuni mjini Changsha, mkoani Hunan China. Kabla ya kufanyika kwake, naibu waziri wa biashara wa China Bw. Tang Wenhong aliongea na wanahabari mjini Beijing akisema maonesho hayo na mengine yanayofanana na hayo yamekuwa mchango mkubwa kwenye kuhimiza biashara kati ya China na nchi za Afrika, na hasa China kuagiza bidhaa za kilimo kutoka barani Afrika..



Maonesho ya nne ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika yaliyoandaliwa na wizara ya biashara ya China na serikali ya mkoa wa Hunan, ni moja ya majukwaa muhimu ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya China na Afrika kwa mwaka huu. Maonesho yamepanua dirisha la bidhaa za Afrika kwenye soko kubwa la China, linalotoa fursa kubwa kwa bidhaa za Afrika. Mifano inayoonesha ukubwa wa maonesho hayo ni pamoja na asilimia 90 ya pecans za Afrika Kusini inauzwa nchini China. Afrika Kusini ikiwa ni nchi ya tatu duniani kwa uzalishaji wa pecans, mauzo ya zao hilo kwa China yaliongezeka kutoka dola bilioni 116.8 na kufikia dola bilioni 178.8.



Profesa Song Wei wa taasisi ya Uhusiano wa Kimataifa na Diplomasia katika Chuo Kikuu cha Mafunzo ya Kigeni cha Beijing, amesema mbali na uagizaji wa bidhaa za kilimo, katika miaka ya karibuni China imekuwa moja wa wawekezaji wakubwa barani Afrika, hatua ambayo pia imekuwa na mchango katika kuhimiza uzalishaji wa bidhaa barani Afrika, na bidhaa hizo kuuzwa katika nchi mbalimbali za Afrika.



Kinachofurahisha zaidi ni uwekezaji wa China barani Afrika umegusa maeneo ambayo yamekuwa na mchango mkubwa kwenye kuweka muunganiko wa sekta mbalimbali za uzalishaji katika nchi ulipo uwekezaji huo. Kwa mfano nchini Misri, Eneo la Ushirikiano wa Kiuchumi na Kibiashara la Suez lina uwekezaji kwenye makundi mbalimbali kama vile nguo, vioo, vifaa vya ujenzi na vifaa vya nyumbani, baadhi ya viwanda vinavyozalisha bidhaa hizo vinategemeana.



Nchini Tanzania kwa mfano, zaidi ya wafanyabiashara wadogo wadogo wa China wapatao 430 wamejiunga na maeneo ya biashara na usafirishaji ambayo yametoa nafasi za ajira zaidi ya 20,000 za ndani. Nchini Zambia, eneo la ushirikiano kati ya China na Zambia limejenga mnyororo kamili wa sekta ya shaba ili kuongeza thamani ya mauzo ya madini nje ya nchi.



Wakati dunia ikiendelea kushuhudia vitendo vya kuvuruga soko la biashara duniani vinavyofanywa na Marekani, China na Afrika zimekuwa zinaendelea kuimarisha ushirikiano na kuwa na matokeo ya kuridhisha. Kwa sasa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) linaendelea kuwa jukwaa linalobeba mwelekeo wa ushirikiano kati ya China na Afrika. Katika siku za hivi karibuni kupitia kundi la nchi za BRICS, China imekuwa ikichukua hatua nyingine kupanua ushirikiano na nchi za Afrika.



Kwa uhakika, China itaendelea kuunga mkono maendeleo ya Afrika kwa dhati, na kuchukulia biashara kama njia muhimu ya kupunguza vizuizi vya maendeleo na kujenga uwezo wa bara la Afrika kwa ukuaji wa kujitegemea.
 
Back
Top Bottom