BINARY NO
JF-Expert Member
- Dec 29, 2011
- 2,148
- 2,160
Hali inaendelea kua ya wasiwasi ndani ya LIBYA mpya baada ya wanajesshi wanaomuunga mkono kiongozi alieuawa Ghadafi kupigana na wanajeshi wa baraza la mpito la NTC na kuwaua wanajeshi wanne wa NTC na kufanikiwa kuuteka mji wa BANIWALIDI..sambamba na hilo kiongozi wao mkuu Mustafa abdi jalili ameonya kua LIBYA huenda ikatumbukia ktk vita vya wenyewe kwa wenyewe baada ya juzi wanafunzi wa vyuo vikuu kuandamana kwa kupinga kiongozi wao naibu kiongozi wa NTC mpaka kujiuzulu na pia wapo wanao andamana wakitaka LIBYA iendeshwe kwa kufuata mfumo wa SHARIA..pia kuna taarifa kua MAREKANI imetuma kwa siri wanajeshi wake 12000 ili kujaribu kutuliza hali ya mambo na kulinda viwanda vya mafuta.....nini hatima ya LIBYA baada ya GHADAFI?