mansoorsaid
JF-Expert Member
- May 31, 2014
- 1,498
- 284
Mnadai Magufuli kasema Polisi akiuwa jambazi hashitakiwi, sawa hilo amepotoka; je, hili la Lowassa la ubaguzi wa dini.
LHRC kauli iliyotolewa na Lowassa kanisani mbona hamjalikemea?
Kuhusu Libya ni kweli walitaka mabadiliko leo wanajuta huo uwongo?
Acheni nyinyi vineno nyinyi ndio wachonganishi
LHRC kauli iliyotolewa na Lowassa kanisani mbona hamjalikemea?
Kuhusu Libya ni kweli walitaka mabadiliko leo wanajuta huo uwongo?
Acheni nyinyi vineno nyinyi ndio wachonganishi
LHRC yamtaka Dkt. Magufuli kufuta kauli zake
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimekemea kauli zenye kuwajengea hofu wananchi kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kidemokrasia unaoendelea kwa kutoa mifano isiyoshabihiana na hali iliyopo nchini ikiwemo kufananisha na nchi zenye machafuko.
Katika taarifa yake iliyotolewa kwa vyombo vya habari imemtaka mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Mh. John Magufuli kufuta kauli zake ikiwemo ya kufanisha mchakato wa uchaguzi na vuguvugu la mabadiliko ya Libya pamoja na serikali yake kuwapiga risasi wahalifu wa kutumia silaha.
Kituo hicho kimesema kauli hizo zinatoa vitisho kwa wapiga kura kinyume na demokrasia kwa kuwa huwezi kufananisha mabadiliko ya kimapinduzi ya Libya na umwagaji damu uliotokea huko na mabadiliko ya amani kwa kupitia mchakato wa uchaguzi za kidemokrasia.
SOURCE: EATV NA EAST AFRICA RADIO