Gashongoile
JF-Expert Member
- Jun 13, 2013
- 487
- 145
Katika sheria ya haki "Substantive Justicce" kuna Phrase inayosema. " SUBSTANTIVE JUSTICE SHOULD BE ADMINISTERD WITH UNDUE REGARD TO TECHNICALITIES" Maana yake ni kuwa hata kama kuna kinga amazo zimewekwa na sheria ndogo ndogo kama hizo za kinga ya bunge haziwezi kuzuia msingi wa Katiba kuhusu haki. Na ndiyo maana kuna sheria inayoitwa " lifting the vail" yaani kuondoa kinga ili kupata haki. Hivyo mtu yeyote anayebwabwaja kuwa Waziri Mkuu hawezi kushitakiwa kwa kauli aliyoitoa Bungeni ni kwa kuwa hana uelewa wa Sheria au amekariri tu.Mzee Pinda ni Waziri Mkuu tena Mwenye Taaluma ya sheria hivyo kwa nafasi yake kauli aliyoitoa Bungeni ni Maagizo ya Serikali na haiwezi kukingwa na sheria za Immunity. My Take:Waliotunga sheria hiyo ya immunity ya Bunge awakuiweka ili viongozi. Watoe kauli hatari kama hizo na wasichukuliwe hatua, hivi kesho waziri wa mambo ya ndani akitoa kauli BUNGENI kuwa police waue watu hatashitakiwa kwa kuwa tu alisema akiwa Bungeni? Tafakari!