Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 17,306
- 19,880
Mnamo mwaka 2016 niliamua kukaa na mtoto wa dada yangu ambaye mama yao yupo lakini baba yao alikwisha fariki. Nilimfuata kwa baba yake mdogo huko Sikonge Tabora ambapo inaonekana yule baba hakuwa anamlea vema yule mtoto na alishaanza kuwa kama chokoraa tu wa kuzurura mitaani.
Nilimchukua na kumtafutia sehemu ya kujishikiza akawa anauza duka kwa rafiki yangu huku nikiwa na mipango ya kumrudisha shule aendelee na masomo.
Alichokifanya yule mtoto kiliniacha mdomo wazi. Aliingia kwenye shelf ya pesa na kuzoa kiasi fulani, takribani laki moja na nusu, kisha akapanda gari na kurudi tabora.
Tangu siku hiyo, nikawa na mashaka sana nikitaka kusaidia mtoto wa ndugu kwa kukaa naye.
Let's share kama wema uliwahi kukuponza katika kipindi fulani cha maisha yako.