Let us DIG DEEP on violence Mbagala, Zanzibar etc | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Let us DIG DEEP on violence Mbagala, Zanzibar etc

Discussion in 'Great Thinkers' started by Bongolander, Oct 20, 2012.

 1. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2012
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Wakuu inaweza kuwa ni rahisi sana kunyosheana vidole na kuumizana kutokana na hali inayoendelea sasa hapa Tanzania.

  Naona ni busara tukijadili THEORIES zinazoweza kutueleza ni kwanini hili limetokea, labda tunaweza kujua nini kinatakiwa kufanyika ili kukabiliana na hali hii, ambayo kwa sasa inaonekana kuwa "very fluid" na inawezekana kuwa itaendelea kwa muda mrefu. Najua hapa kuna vichwa venye uelewa na kuweza kujadili issue hii kwa hoja na busara, kuna theories tatu ambazo naona zinaweza kutusaidia kuangalia jambo hili, tusiwalaumu waislamu kwa kuwa katika issue hii ukweli ni kuwa hakuna waislamu naona wanasiasa zaidi na udhaifu katika udhibiti wa mambo yanayoendelea Tanzania.

  1. Unregulated and uncontrolled FREEDOM OF SPEECH AND EXRESSION
  Je ni kutokana na kuwa katiba yetu inatupa "uhuru" kupita kiasi? Yaani sheria zinazolinda uhuru huu zina mianya na kutoa nafasi kwa watu kutumia vibaya uhuru tuliopewa kikatiba [kukusanyika, kuabudu na kutoa maoni], kutukana, kufanya vurugu, vurumai, uharibifu na uuaji? Kwa muktadha huu tuangalie kama kweli hizi ni vurugu za kidini zinatokana na kitendo cha mtoto mkristo kukojolea Koran aliyopewa na mtoto mwislamu na kumwambia akiikojolea atabadilika kuwa Nyoka au Panya? Au suala hili limedakwa na baadhi ya watu ambao kwa muda wamekuwa wakitumia uhuru tunaopewa na katiba kuchochea vurugu, lakini hawakuwa na kisingizo cha kutekeleza yale ambayo wamekuwa wakihubiri kwa zadi ya miaka saba sasa?

  Tukiangalia kwa undani uhuru huu kwa sasa tunaweza kusema hata teknolojia imetifikisha mahali ambao tuna vyombo kama JF, Radio Maria, Radio Imaan, gazeti za Kandanda kitandani, Msemakweli etc etc etc ambayo mto yoyote anaweza kutoa maoni kupitia vyombo hivyo na yeyote anaweza kusoma maoni, bila kuwa na chombo imara cha kudhibiti yaliyomo. Kuna vehicles zenye nguvu sana zenye uwezo wa kusafirisha maoni kwa muda mfupi na kwa haraka sana, serikali yetu bado haijafanya lolote la maana kushughulikia suala hilo.

  Kibaya zaidi "wahuni na majambazi" wamekuwa ni karata nzuri sana kwa baadhi ya vyama na kwa baadhi ya wanasiasa, na kupewa fursa ya kutumia uhuru na vyombo vipya vya kutoa maoni kuchezea amani, umoja, utulivu na muungano wa Tanzania. Kwa hiyo unaona hata wakitoa kauli za kichochezi namna gani serikali inakuwa kimya tu, kana kwamba inawaogopa, hata ra

  2. Nasty POLITICAL COMPETITION (ndani ya CCM, CCM vs Upinzani).
  Kuna mambo mengi sana yamekuwa yakitokea kipindi hiki ndani ya CCM, makundi matatu au manne yanatafuta nafasi ya kushika dola kwa udi na uvumba, lakini ni bahati mbaya sana makundi hayo hayana kitu cha maana kuwaonesha watanzania, kwanini wanastahili kushika dola. Kwa hiyo inaonesha kuwa ni "power at any cost". Tumesikia wanaCCM wakiwekeana sumu, waandamizi wakijiengua, wengine wakijiimarisha, wengine wakilalamika ufisadi na "foul play", wengine wakitoa lugha za ajabu ambazo hawajawahi kuzitoa huko nyuma, na ambazo si desturi yao, yote hayo yanaonesha kuwa kuna mvutano mkali. Lakini kuna wengine wamekuwa kimya sana, kikauli, lakini wana-act. Kuna uwezekano mkubwa kabisa kuwa vurugu za hivi karibuni zilichochewa na mwanasiasa fulani, au kundi fulani la wanasiasa, kwa malengo ya kisiasa kuelekea 2015, au kuweka platform nzuri ya kudhibiti kwa muda wimbi la kukua upinzani.

  If you stand from a vintage point [jifanye wewe sio CUF, CDM wala CCM] you can see that there are very clear signs that the incumbent is launching a dire attempt to remain in power in the wake of surging fortunes of the opposition. Visiwani ni kama opinion inaegemea zaidi kwenye upande wa CUF, kwa hiyo karata ya "uislamu" na vurugu za ‘uamsho' zinaweza kuwa ni kisingizio kizuri cha cha kidivert attention from real issues.

  Sidhani kama ni bahati mbaya kwa matukio kutokea bara na visiwani kwa wakati mmoja, ‘waislamu' wa bara na visiwani kuwa na matatizo tofauti kwa wakati mmoja ni jambo la ajabu kidogo.

  Huku bara ni wazi kabisa kuwa serikali imefanya madudu mengi sana kiasi kwamba maisha ya wananchi yamekuwa magumu sana, watu wamepoteza matumaini na kuchanganyikiwa. Ufisadi sasa ni kama unatambuliwa wazi kuwa ni sera inayokubalika kivitendo, na kupingwa kikauli na kimaandishi. Lakini kuwa beneficiary ni lazima uwe kwenye hatamu. Kitu ambacho wananchi wa kawaida na wanaccm na wapinzani hawakitaki, lakini hakiwezi kutoka kwenye Chama.

  Kutokana na kuonesha incapability na kuto-deliver kwa wananchi, ni kama kuna haja ya kuwa na justification ya kuwepo madarakani at least kwa sasa, na kufunika aibu ya kuwa ‘hatuja-deliver" na kushindwa ku-deal na real issues (union in tatters, inflation, amani na usalama, no jobs, misongamano barabarani, mishahara duni, umeme, maji, elimu, justice). Kuleta kitu ambacho kitawagawa wananchi na kujiweka katikati yao kutasaidia kujustify uwepo wa serikali. At the end of the day utaona wahusika wakuu wananufaika, na wananchi wa kawaida wote wakristo na waislamu wanaathiriwa.

  3. UNYONGE
  Kuna kitu kimoja ambacho tunatakiwa tukubaliane, kwamba kuna unyonge mkubwa sana katika jamii yetu. Inawezekana unyonge huu ndio unaowafanya watu wahusike kwenye ujinga kama huu uliotokea. Labda ndio maana Nyerere alikuwa anasema sema tupambane na adui ujinga.

  Kuna watu wengi hawajui tatizo lao kubwa ni nini. Inawezekana hata leo ukimuuliza mtu mtaani tatizo lako ni nini unaweza kushangaa jibu. Jaribu kutumia akili kidogo kuangalia ni nini kitakufanya uandamane na kutaka mabadiliko, umaskini au udhalilishaji wa kidini. Kuna baadhi ya watu wanadhani kuwa wakristo hapa Tanzania wako better off kuliko watu wa dini nyingine. Lakini ukiangalia uhalisia unaona kuwa watanzania wote bila kujali dini zao wanaogelea kwenye dimbwi moja.

  Will there be any change in the content if a person urinates on the Quran or on the bible for that matter? au bado Tanzania kuna ujinga kama wa watu ambao hawana shule hata kidogo wa Afghanistan? Ukiangalia kwa undani unaweza kuona kuwa hii ajenda ni kubwa kuliko kukojolea msahafu. Wajanja wamecapitalize kwenye unyonge wa watanzania. Unyonge mwingine ni kuwa bado tunashindwa kujua nani ni Sheikh hapa Tanzania na nani si Sheikh, bado hakuna vigezo wazi vya nani ni sheikh na nani si sheikh, na nani mwakilishi halali wa waislamu na anayeweza kuwasemea waislamu
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  Mimi nasema kuna unafiki mkubwa hasa kwa wana jf

  kama suala ni haki ya watu kuandamana na 'freedom of expression'

  basi hatukupaswa kuwalaumu waislamu wala kushabikia polisi kutumia nguvu kuubwa

  kudhibiti maandamano......

  wakiwafanyia hivyo CHADEMA tunalalamika.......

  sasa huu si unafiki?

  si tunapaswa tetea sheria na haki bila kutazama sheria hizo zinamhusu nani?

  Kama hawakuvuwa na silaha na walisema maandamano niya amani
  tulipaswa wote kutoshabikia nguvu kuubwa iliyotumika kuzuia maandamano

  hata kama agenda ya walioandamana hatukubaliani nayo...ili mradi ni haki yao kuandamana...
   
 3. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2012
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu The boss, kama umesoma kwa undani maelezo yangu unaweza kuona kuwa suala ni kutumia uhuru wetu bila ukomo, yaani sisi wenyewe tunaondamana, na tunaandama kwa shari kiasi cha kuwawafanya polisi na wanajeshi watufuate. Na suala lingine ni kama kweli tunaandamana kwa sababu ya msingi, au tunaandamana tu kwa kuchochewa na kutumiwa na wanasiasa kwa sababu zao, hasa wale wanasiasa wanaotumia wanyonge.

  Sikubaliani na Polisi kupiga raia au kutumia nguvu kupita kiasi, iwe kwa "waislamu" au Chadema au machinga. Siamini kama kweli walioandama ni waislamu, inawezekana kuwa walikuwepo "waislamu" lakini siwezi kuita maandamano ya vurugu ni ya waislamu, kwa kuwa hakuna waislamu wanaotambulika kuyaunga mkono na kuyapa baraka.
   
 4. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Itakuja kufahamika tu kuwa kulikuwa na mkono wa mtu. Haya mambo hayajatokea tu bali yamefanywa kutokea. Nakumbuka palishakuwa na shehe Gorogosi, kipindi hicho cuf ikiwa juu sana. Hawa jamaa walikuja kujiri baadae kuwa walikuwa wakipita misikitini kwenye kila swala ya ijumaa na kuwahubiria waislam kuwa ccm ni christian movement. Leo wanasema cdm ni cha wakristo, mara movement for chagga... Na masikini kwa bahati mbaya au makusudi wahanga ni waislam. Wanatumika. Waislam wafike sehem waone kuwa wanatumika. Popote pale duniani sijasikia wakristo wakitumika. Waislam wametumika sana naijeria kipindi cha siasa za kina abacha. Leo tunaona makovu yake-kina boko haram. Waliowatumia wako ngazi zingine.

  Waislam wanatumika mombasa-MRC, wanatumika bara, wanatumika visiwani-uamsho. Leo hii baraza la wawakilishi linasusia kikao kisa Fareed kakamatwa. Kwa nini tusiamini kuwa siasa inatumia imani ya kiislam?

  Hilo ni moja. Likitoka la dini litakuja la ukosefu wa ajira. Hili litaungana na chuki dhidi ya viongozi waliopo ambao wanapandikiza watoto wao kwenye nafasi mbalimbali za chama, serikali, taasisi, makampuni, pamoja na popote pale penye ulaji. Hii ni chuki ya wazi inajengwa. Sasa tusiombe haya matatu (udini, ukosefu wa ajira, na undugunaizeshen) yakutane rasmi.

  La msingi la kuomba hapa ni kuwa kwa hii miaka miwili iliyobaki tuvuke salama ili watanzania wafanye maamuzi sahihi hapo 2015 baada ya kusota na kukabiliana na madhila yote haya kwa kipindi cha miaka 10 mfululizo.
   
 5. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #5
  Oct 20, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,026
  Likes Received: 7,419
  Trophy Points: 280
  Very Interesting.....naomba muda kidogo nimalizie ka-report kangu kabla sijamkabidhi mtendaji wa kijiji ili na bwana shamba, then narudi kuchangia.
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Oct 20, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Bongolander,

  Mkuu wangu huu ndio Uzalendo kwenda deep kujua matatizo yetu yanatokana na nini? shukran sana, hakika kama vile umekuwa kichwani mwangu.
   
 7. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #7
  Oct 20, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Yaa...yawezekana kabisa hasa kwa hayo mawili ya mwisho.
   
 8. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #8
  Oct 20, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Violence tunayoiona ni mtandao wa kitawala/kisiasa katika kutugawa. Full stop!
   
 9. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #9
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Hili haliwezi kuisha leo kwa vitisho vya kutumia nguvu ya dola .Vurugu hizi ni matunda ya umasikini uliokithiri ukiambatana na ukosefu wa ajira kwa Vijana mengi huko mitaani .Ukitaka kugundua chanzo cha hili vurugu fuatilia kwa umakini washiriki rika lao na vitendo wanavyofanya kipindi cha maandamano .Kundi hili la hawa wanaofanya vurugu ni watu waliokata tamaa ya maisha hivyo anapotokea mtu kuwashawishi kufanya jambo la kiuhalifu kwao ni neema .

  Nimeshuhudia maandamano nchi nyingi za kiafrika ya namna hii na kwa mara nyingi taarifa zinapotoshwa kuhusu chanzo ni nini .Chanzo hupotoshwa kwa makusudi kwa maslahi ya waliyopo madarakani .Mfano vurugu za Kenya mwaka kwa 2007 report ya kituo cha television Aljazira ilibainisha wazi chanzo ni umasikini uliokithiri kwa jamii kubwa ya wakenya(maeneo ya kibera na kwingineko ) ,hivyo walipotokea wanasiasa kuwashawishi waingie mitaani ,haikuwa taabu.

  Kwa mini naandika chanzo ni umasikini.
  Pindi vurugu hili zinapoanza ndipo utagundua kundi hili lililopo mstari wa mbele wanakusudia nini. Mara zote vurugu hili kundi kubwa la washiriki hutumia mwanya huo kutoka na kuiba mali , kufanya uharibifu wa Mali za watu.Haya nimeyashudia Zimbabwe,Malawi ,Kenya na Uganda .Mfano Uganda wahindi na wafanya biashara wengine walipogundua kuwa baazi ya waandamanaji wautumia mwanya huo kupora mali zao wakabuni njia ya kudhibiti .Hili hii imepelekea kundi kubwa la hawa waporaji kutoshiriki kikamilifu kwenye maandamano (vijana hao watokea sehemu maarufu iitwayo NDEVA)

  Udini katika hizi vurugu anatuhumiwa kama njia kwani kwa sasa ndio sehemu inayoonekana kuwa na sauti Kutokana na udhaifu wa dola .Serikali imelala sana na kufumbia macho ukuaji wa kasi miongoni mwa jamii ya Tanzania ni vigumu sana kumtawala mtu mwenye njaa .Julie hizi dini /madhehebu yanayoibuka kila kukicha inatokana na nini!
   
 10. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #10
  Oct 21, 2012
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu is CCM mtandao still intact, do they have one voice going to 2015? au tunachooona ni mapambano kati ya "waislamu" wa mtandao na "wakristo" wa mtandao?
   
 11. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #11
  Oct 21, 2012
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135

  Mkuu ukiangalia udani wa suala lote unaweza kuona kuwa kuna maswali mengine mengi yanajitokeza. Ni kweli serikali yetu haina uwezo wa kuwashughulikia wachochezi? Kimsingi nguvu inayo, lakini inaonekana kuwa hao wanaofanya vurugu wanawekewa vifua na watu ndani ya vyama na kutumiwa kama pawns kwenye chess game.

  Ukisikiliza Radio Imaan huwezi kuamini kama kuna serikali au kama kuna idara inayofanya kazi ya kusimamia matangazo. Lakini swali ni kwanini inaachwa tu? maana yake ni kuwa kuna sababu inayofanya wanaachwa.....

  Tanzania kimsingi hakuna udini, isipokuwa watu wanapandikiza chuki za udini ili kuzitumia kwa maelngo yao kisiasa. Jaribu kunagalia linapokuja suala ma hija na mahujaji, unaweza kuona wanaojitokeza ni matapeli kusema kuwa tunahakikisha watu wanaenda kuhiji, lakini angalia matendo yao, unaweza kujiuliza ni kwanini wanapigania sana suala hili wakati CV zao utata mtupu.
   
 12. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #12
  Oct 29, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  mwandishi anafanya silly attempt kuutoa uislam katika makosa,ila sijui atasemaje sehemu nyingine duniani?maandamano ni haki, ila pia hiyo haki inaweza kuwa nusu haki nusu haramu kama malengo yake yanawayima wengine haki kwa makusudi.Wakristu wana haki ya kulindwa na sheria,na hakuna mwenye haki ya kufanyi amizaha uhuru na mali za wengine just because kasikia anawashwa na mwili wake au fikra zimeamua kufanya hivyo.Sasa hizi theories nyingi za nini?Wengine wanafikia kusema wale jamaa ni vibaka na si waislam kwa vile wengine waliiba pombe na mali.Sasa sijui kuwa muislam ndio kunazuia mtu kuwa mwovu?Kuvamia wengine tayari ni uovu achilia mbali kuiba vitu na kwenye mabaa kuiba pombe.

  Kwa ujumla hawa waislam walishachoma makanisa na ponda hotuba zake zipo wazi sana,sasa maandamano ya kutaka aachiwe na sheria isichukue njia yake ni kutowajibika.Hapa ndipo watu wana question na si msingi mkuu wa maandamano.Ila lengo lake.

  Ipo siku paedophiles wataandamana wakidai sisi tumewazuia kubaka watoto wetu.Je haki ya kuandamana itabaki palepale?
   
 13. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #13
  Oct 29, 2012
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu Nicholas, issue hapa ni kuwa uislamu na waislamu vinatumiwa. Hapa Tanzania waislamu wamekuwepo miaka nenda miaka rudi, sidhani kama naweza kusema waislamu wa Tanzania ni violent.

  Tatizo ni kuwa wanasiasa ambao kwa sasa wanaendelea kupoteza popularity wanatumia uislamu ili kufkia ajenda zao za kisiasa.

  Kama ukiangalia vizuri bandiko langu, nimetaja suala na kutumia vibaya uhuru tulionao na unaolindwa kikataba. Kiasi kwamba mtu anaweza kwenda kutoa kauli za uchochezi matusi na hata uongo kwa kisingizio cha maslahi ya waislamu. Lakini ukiangalia undani wa watu hao unaweza kuona kuwa si waislamu, ndio maana mimi nawaitwa 'waislamu'.

  Angalia kama kweli huyo Sheikh Ponda ni mwislamu kama tafsiri ya mwislamu ilivyo. Ukichimba kwa undani utaona kuwa hana credential ya kusimamia haki za mwislamu, zaidi anatumiwa tu.

  1. Je ni mwislamu ambaye anafuata mafundisho na mtume Mohamed SAW na kutaka kuyaeneza?
  2. Je anaishi kama mwislamu safi ambaye anatakiwa kuwa mfano kwa waislamu wengine?
  3. Anajua uislamu unahubiri nini na yeye anahubiri nini?
  4. Tukiacha mambo ya dini, yeye ana elimu gani ya kuweza kuchanganua mambo kwa kutumia elimu na busara kwa kuangalia mazingira anayoishi na wakati anaosihi.

  Kwa kuangalia juu juu unaweza kuona kuwa anachofahamu ni kuwa ana haki ya kukusanyika na kutoa mihadhara ya ajabu. Inawezekana kabisa kuwa yeye ni mwislamu wa kutokula nguruwe na kuvaa kanzu tu. Kama angekuwa mwislamu wa kweli asingekuwa mstari wa mbele kuchochea vurugu na uharibifu, hayo si mambo yanayoweza kufanywa na Sheikh.

  The point here is muslims are just pawn and Christians are scapegoats of the whole fracas, the root of the problem is within CCM, where there are politicians who will do whatever they can to maintain the status quo, even at the expense of our harmony. The war should be waged against them, not against others.
   
 14. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #14
  Oct 29, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  Waislam wanapenda sana kuja maelezo mbadala ili kukwepesha ukweli kwanini mambo hayaendi ktk dunia yao.Hii haitasaidia sana kwa waislam kwa ujumla.Kwani kuna waislam wengi tuu na makafiri pia ambao huwa kauli kama hizi zinawapotosha sana.

  Kwa nini wasilam na uislam uwe rahisi tumika duniani kote?Well, kama kweli wanatumika then ni dini ya kitumwa.Kama hawatumiki then kuna shida na jinsi wanavyoitumia dini yao.

  Kwanini unasema hao si waislam wakati miaka yote wamekuwa ktk usilam na wamehubiri ktk mikitini inayotumika waislam wa madhehebu yaliyosajiliwa kihalali na kwa jinsi kila mtu anaujua uislam anayeukufuru uislam hawezi ingia miskitini mara zote hizi akapona kama si mara ya kwanza tuu.Mwinyi mwenyewe alihubiri condom tuu alichokipata tunakijua.

  Ulichoandika kinapumbaza wengi sana waliwepo waislam wenyewe wasioijua dini yao vyema.Ila unachofanya ni sehemu ya soft jihad,madhubuti kwa ajili ya kuwapotosha makafiri, au hata kutumia tekkiya.Uongo mtakatifu.Sijui kam aunafahamu au umefanya makusudi ila ukweli ni kwamba uislam ulikuwa tatizo kwa mara nyingine tena.Mara ya kwanza walisingizia muungano huku wanachoma makanisa.Hakuna muislam hata mmoja aliyesema waist a minute hii haina cha kufanya namuungani wala ini hii ni sehemu ya uchokozi kwa wengine ambao mnawaona hawastahili ishi na ni waoga.Kila miskiti unauza tape na CD za progranda ambazo hata kusikiliza unapata kichfuchefu.Ila sidhai kam ulishawahi wauliza kama kweli zinastahili uzwa maeneo ya msikitiki kama si kuuzwa kabisa.


  Sijui kwa kiasi gani umedanganyika au kuamua danganya watu ila wapo waislam wengi tuu wamechoshwa na hizi aibu na wameamua sema wazi kuwa wale waislam walitia aibu sana.Wapo wanaojua udhaifu wa taasisi zao ktk kila sector hawa alifikia pa kuwaona waislam walifany amatendo kama vile wamekatwa vichwa.Lakini problem ipo ktk jinsi waislam wanavyofundishwa kuvia pproach vitabu vyao.Hapo ndipo shida inapokuja kwani wana apporach vibaya wanaishia kutoa wakiwa wamekuwa wabaya sana.

  Unless unasimamia hili hakuna unachosaidia hapa zaidi ya kuchelewesha chuki kuchukua nguvu zaidi hadi unawadanganya nao watajiridhisha kuwa shida ni "dini na si siasa wala nini".Kwani dunia nzima haya matendo yanaonekana.Na wenzetu hapa wanawahi sana kufikia level ya wenzao.wenzao wanajitahidi sana kuweza jirekebesha angalau waweze ishi kwa amani na wenzao,lakini waislam wanazidi tafsiri kuwa wenzani ni waoga huku wakizidi fany amahusiano yawe magumu zaidi na zaidi tena.Unachoongea hapa kitawatuliza Wakristu ila siku zinavyokwenda chuki itajijenga zaidi huku waislam wakijiamisha kuwa wamepewa haki miliki ya kufanya vurugu kama walevi kila mara wanapohisi kuwa wana hamu ya kufanya vurugu.Au pale wanapohisi kuna kanisa zuri linalowapa kijiba rohoni basi wanalipangia tuu siku na kasababu ka kijinga.Ila siku zitakuja,itapigwa vita ya kweli.

  Ndugu yangu usipende paka rangi nzuri na ladha unayodhani kuwa inakuwa nzuri,kwani huko kupaka kunaweza kufanya utangaziwe vita hapa hapa,na wanaoamini dini yao kwa uhasilia wake.
  Upe uislam haki yake ili uweze jiuliza maswali ya haki kama kweli upo innocent au lah.Unakufaa au lah.Ila si kuupaka rangi kwa nje ukausafisha kwa njea halafu ukala kwa ndani pasiposafishwa.Badla ya kudanganya waili wakuwasaide meza kitu mabcho ktk mindi yako hakiingi akilini,kwanini usifce hayo maswali mwenyewe.N akuwaacha wengine wakiugulia maumivu ya walichokumbana nancho kwa jina uislam.Pengine ungekuja na chochote ktk nguzo tano za uislam ambazo zinawafanya hao watu wasiiwe waislam.
   
 15. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #15
  Nov 3, 2012
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu uislamu wanaweza kuelezea waislamu wenyewe, na ukristo pia wanaweza kuuelezea ukristo wao wenyewe. Lakini siku zote kwenye ukweli uongo hujitenga, bila kujali nani anasema nini. Facts never lie. Tunaona facts na tunaona tunakoelekea. Kuna maswali mengi ya kujiuliza, why muslims why now why Dar es salaam not Kilwa or Pemba unaweza kuona kuwa amjibu yote yanaenda kwa wanasiasa, sio waislamu in their totality.

  Kinachosemwa na kinachoonekana ni vitu viwili tofauti. Kwa mfano huyp Ponda anajiita Sheikh, lakini he behaves like a political activists not a cleric, ndio maana kwa maoni yangu binafsi ni mhuni tu sio sheikh. Kama uislamu upo innocent au la, huo ni mjadala mkubwa sana. Kama unajua kuna video ya innocence of muslims ilitolewa hivi karibuni imeonesha wasiwasi kama wako, lakini ukweli kuhusu jambo hilo uko wazi sana.

  Lakini ni vizuri tukiangalia sheria zetu kwa makini na namna tunavyozitekeleza, ili kuona kama tunawapa mwanya watu kama Ponda kuleta vurugu.

  By they way this is not the first time we have this madness, nakumbuka kina Kundecha na Msikiti wa Kwa Mtoro, Makamba ali-deal nao vizuri..
   
 16. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #16
  Nov 3, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  Ngugu yangu hembu soma haya. "wenye mabusha wanajua mabusha ni nini au wenye watoto mataahira wanajua kwanini wanao ni mataahira".

  Nadhani utaona ni wapi logic yako ipo flawed. Wengi wa wenye mabusha ktk pwani ya Tanzania walifikia mahali wakawa wanaona fahari sana hawakujua ni ugonjwa, wenye watoto mataahira nchi za asia na africa wengi kama si wote wanaamini kuna mkono wa mtu,hata wasomi kuna mara nyingine wanajikuta wakiamini kila tukio la mashaka likiwajia.

  Waislam wame buy idea duni sana kuwa wao tuu ndio wanaujua uislam vyema.Hawajui comprehesion ya maandiko yoyote kila mtu ana uwezo wake.PIa wanasahau kuwa kuna watu walianzia kwenye uislam na baadaye kuachana nao, wanasahahu kuwa makafiri wamechangia sana mambo mengi sana ktk tafiti za historia ya uislam na mambo ya kiutawala.
  Unaweza kuwa na ukweli kuwa kinachosemwa n akinachoonekana ni vitu viwili tofauti ila ,kwa kinyume.Yaani unachosema wewe hapa na kinachotokea hapa ni vitu tofauti.Watu wameusoma uislam sana na wana documents nzuri sana na viashiria vinavyowasaidia kujua what is next.

  Hiyo movie ya innocence of muslims ni mind provocative ili watu wajiulize maswali muhimu ya kuweza mto muislam ktk uovu na kuupeleka uislam.Wanaojua hilo ndio wanakomaa na watu ili kubakisha.Kwani wanajua watu wakianza jiuliza hivyo uislam utakuwa na hali ngumu sana.

  Pengine utaniona kuwa mimi nipo harsh sana ila ukweli ni kwamba uislam unamfanya muislam kuwa very vulnerable, na mkorofi sana huku akiamini kuwa afanyacho ni dhabihu kwa mola wake.

  wewe unamwona Ponda ni political activist zaidi ya sheikh,inaonekana kuwa bado uislam huujui vizuri.Fahari ya muislam ni kwamba dini yake ni mfumo kamili wa maisha(dola,utamaduni,dini, etc),uislam una mwoongoza muislam kuanzia aingiapo chooni,kutoka,kufanya mapenzi, siasa,vita, imani,afya etc.Siasa ni sehemu ya uislam na wengi wanasema ni dini ya haki.Neno haki lina uzito sana ila tafsiri ya "haki" au "kweli" kwa muislam ni tofauti sana na wasio waislam.Hapa ndipo shida inapoanzia.Wakati waislam wandaia haki zao kwa kiasi kikubwa wanakandamiza haki za wengine.Wakati wakisema kwa kuwa kitu fulani ni kweli basi ujue wana maanisha cha mwingine ni uongo.Conflict ya idea inatokea tena.Na ikitokea ndipo waislam wanaposema Allah kasema haki pekee na kweli pekee ni ile iliyoandikwa ktk Quran.Hayo ni baadhi tuu ya mambo ambayo huwezi singizia US,Israel, Russia, Saudi Kingdom,CCM au Wabidha kule Thailand, au Burma.
  Sheria zipi zinazokubalika na waislam safi?Sheria zao ni sharia na kila mmoja anatamani hizo.Hizo unazoongea ni dalili tuu kam ailivyo homa .Homa hutokea kwa kila ugonjwa.Na hizi confusing patterns ndizo zimesaidia sana ukuaji wa uislam duniani.Hata waislam wenyewe,wengi hawajui sana matukio yanatoakana na nini?Ndio maana masheikh hubadilisha sababu tuu, kama makanisa yalivyoungua walisema ni muungano na ukandamizaji,wazee wa ndani wanajua ni kwanini,ila waumini nusunusu na makafiri wataaminishwa hivyo ili waendelee na shughuli zao.Ila siku uislam unajisjika vizuri hapatakuwa tena na siri ndugu yangu.

  Mtazungushwa sana kwa hizi sababu general ila huwezi pata sheria zozote duniani zinazokubalika kwa waislam.kila sehemu waislam wana sababu kuwa wengine wanawakandamiza.Ila hata serikali za nchi za kiislam husimama kwa udictator,saddam ahakupata shida,ghaddafi naye,Al bashir, Assad,Salmin etc
   
 17. M

  Mkandara Verified User

  #17
  Nov 4, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Unampigia mbuzi gitaa!...
   
 18. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #18
  Nov 5, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  teh teh...hapo ndipo ulipota matumaini?

  Kuwa muislam ni kufuata nguzo 5 za uislam zote ila kuna mazingira ya kuacha ya mwisho ya hija.Sasa ni wapi umemzidi au kumtoa Ponda?Weka na ya sita Jihad(wauwe makafir popote walipo hadi dini ya allah itawale).Ponda kafanya wewe hujafanya?

  Kipi kinakufanya uupunguze uislam wake?Kwa wasioujua uislam hawakosi suprises kila kukicha na nyie ni mojawapo ya wasioujua uislam au wanaficha ukweli.

  Sioni wapi waislam wanataka aminisha watu kuwa uislam hauwezi eleweka na wasio waislam?Au ni wapi uislam upo that wonderful kiasi ch akuupamba hivyo?Kwangu mimi ni dini ya hovyo sana ,kwa mtu mwenye akili kuufuata na haina ushawishi wowote kwangu.Hizo blah blah sijui unachukiwa, zinawatosha sana nyinyi kiushawishi.Watu wanauchukia kwa sababu unachukiza, sasa kama hamuwezi meza si mjiulize kama ni worth it nyie kuung`ang`ania.Haku kosa kuuchukia uislam,ila kuna kosa kuwachukia waislam(Watu) huko kutakuwa kuvunja haki za binadamu.Simchukii mwizi ila nauchukiwa wizi.
   
Loading...