Leseni ya udereva ikiisha muda, ina maana na utaalamu wa kuendesha umeisha?

bab-D

JF-Expert Member
May 2, 2015
1,207
301
Naomba nielimishwe, leseni ya udereva ikiisha muda ulioandikwa inamaanisha na ujuzi unaisha? Kwa nini kama ndiyo hata vyeti vya taaluma basi tuwe tunabadilisha kila baada ya muda fulani.

Pia kama Kitambulisho cha NIDA kimefutiwa ukomo basi na leseni ifutiwe.

Au ni biashara?
 
Naomba nielimiamshwe, leseni ya udereva ikiisha muda ulioandikwa inamaanisha na ujuzi unaisha? Kwa nini kama ndiyo hata vyeti vya taaluma basi tuwe tunabadilisha kila baada ya muda fulani.

Hapana mkuu una update kwa kulipia
 
Kumbuka jambo moja, ni serikali hiyo hiyo ilitoa leseni ya kitabu enzi zile na kusema wewe ni wa daraja E, baadae wakasema huwezi kuwa daraja E mpaka uoneshe cheti cha VETA au NIT, wakisahau kuna watu wanazo hizo E kabla VETA haijaanza.

Unafutiwa uhuru wa kuendesha chombo cha moto ndani ya mipaka yao.

Kuna raia hata baiskeli hawajui kuendesha ila wanayo madaraja yote kwenye leseni.
 
Kifurushi cha simu kikiisha na cm inakuwa imeharibika?

Lengo la lessen ni kuongeza mapato ya serikali.....au ulitaka kiwe km cheti cha kuzaliwa ukipewa umepewa?
 
Naomba nielimiamshwe, leseni ya udereva ikiisha muda ulioandikwa inamaanisha na ujuzi unaisha? Kwa nini kama ndiyo hata vyeti vya taaluma basi tuwe tunabadilisha kila baada ya muda fulani.

Pia kama Kitambulisho cha NIDA kimefutiwa ukomo basi na leseni ifutiwe.

Au ni biashara?
Kuna baadhi ya taaluma pia zina leseni na kuna muda ukifika lazima zilipiwe haijalishi umeitumia au lah, haimaanishi ujuzi wa io fani umeisha.. Anyway ndo ivo mkuu😂😂😂
 
Hiyo tisa kumi kukamata gari kuukuu kusema ni mbovu na chanzo cha ajali, sikubaliani nao! Magari mapya yenye uwezo wa kwenda kasi uchangia 90% ya ajali nchini. Hivyo sipenda kunyanyasa magari ya mchanga, mkaa, yaendayo shamba kubeba mazao ghafi!
 
Swali la uelewa kwa wale wenye ufahamu na hili;

Je iwapo dereva amekumbwa na matatizo na hajaripia upya leseni yake kwa hiyo miaka mitatu inakuwaje?

Je? Leseni inafungiwa au anaenda ku-renew tu. Au anaanza upya process za kupata leseni
 
Hapana mkuu una update kwa kulipia
Tafsiri yake ni kuwa udereva kama utaalamu unanunuliwa! Otherwise ibadilishwe jina; isiitwe leseni ya udereva badala yake iitwe leseni ya barabarani!

That means, ili uwe na chombo barabarani lazima uwe umelipia na sio kwamba huna skills.
 
Kuna baadhi ya taaluma pia zina leseni na kuna muda ukifika lazima zilipiwe haijalishi umeitumia au lah, haimaanishi ujuzi wa io fani umeisha.. Anyway ndo ivo mkuu😂😂😂
Mbinu za kupiga hela tu hamna kitu na hasa hizi professional boards ili utambuliwe lazima ulipie.
 
Kifurushi cha simu kikiisha na cm inakuwa imeharibika?

Lengo la lessen ni kuongeza mapato ya serikali.....au ulitaka kiwe km cheti cha kuzaliwa ukipewa umepewa?
Hapo sawa! Waende straight kwenye sababu ya msingi sio kuzunguka bila sababu. Iitwe kodi au tozo ya udereva itaeleweka vizuri zaidi badala ya kuleta confusion.
 
Tafsiri yake ni kuwa udereva kama utaalamu unanunuliwa! Otherwise ibadilishwe jina; isiitwe leseni ya udereva badala yake iitwe leseni ya barabarani!

That means, ili uwe na chombo barabarani lazima uwe umelipia na sio kwamba huna skills.
Hapana mkuu ujuzi hauishii ila ni njia tu za upigaji japo sijafuatilia nchi nyingine wanafanyaje all in all tupo kwenye nchi ya ajabu sanaa
 
Kuna sababu 3 kubwa za msingi za kumalizika kwa muda wa leseni kila baada ya miaka 10 at least:

1. Kubadilika kwa sura ya mtu baada ya muda.

2. Kubadilika kwa hali ya afya e.g. matatizo ya macho

3. Ku update system e.g. kifo na kukosa uwezo wa kuweza kuendesha kutokana na umri kuwa mkubwa.

Ku renew leseni haitakiwi kuwa ni chanzo cha mapato kwa taasisi husika.
 
Kama sababu ndo hizo kwanini isiwe bure ku-renew?
 
Swali la uelewa kwa wale wenye ufahamu na hili;

Je iwapo dereva amekumbwa na matatizo na hajaripia upya leseni yake kwa hiyo miaka mitatu inakuwaje?

Je? Leseni inafungiwa au anaenda ku-renew tu. Au anaanza upya process za kupata leseni
Iwapo hujailipia leseni kwa muda wa miaka mitatu mfulululizo(respectively) leseni yako inafungiwa na ukitaka tena leseni itabidi uanze process upyaa za kutafuta leseni kama mwanzo

Mamlaka imeweka sheria hio lbda kwa kuona kua utakua ushasahau mambo mengi kuhusu udereva au ndio sheria tu imewekwa hivo

Asante sana
 
Mada nzuri, driving license ina ukomo na sababu kubwa ni kila inapokua imeisha muda wake, dereva anatakiwa a renew na hii inaendana na dereva kuwa na afya njema ya kuendelea kuendesha(medical report &eye test)ndio muhimu zaidi, masuala ya uzee na vifo haviathiri sana maana systems za home affairs zina uwezo to pick this, mfano dereva anapokuwa amefariki, ripoti ya doctor kuthibitisha hili na death certificate kutolewa na home affairs ambao watakua wameshaingiza kwenye systems ya nchi, means systems zote kuanzia police, bank,etc ile I'd number ikiingizwa moja kwa moja itaonyesha mhusika ni deceased.
 
Naomba nielimiamshwe, leseni ya udereva ikiisha muda ulioandikwa inamaanisha na ujuzi unaisha? Kwa nini kama ndiyo hata vyeti vya taaluma basi tuwe tunabadilisha kila baada ya muda fulani.

Pia kama Kitambulisho cha NIDA kimefutiwa ukomo basi na leseni ifutiwe.

Au ni biashara?
Serikali iligundua hilo kwa kuanzia kitambulisho cha NIDA kuwa inacheza upatu kwenye eneo la lifespan.

Leseni ya udereva ni utaratibu wa ajabu sana.

Renewal ya lesen ya udereva ni utaratibu unaopaswa kufamyiwa maboresho. Rushwa haikwepeki
 
Iwapo hujailipia leseni kwa muda wa miaka mitatu mfulululizo(respectively) leseni yako inafungiwa na ukitaka tena leseni itabidi uanze process upyaa za kutafuta leseni kama mwanzo

Mamlaka imeweka sheria hio lbda kwa kuona kua utakua ushasahau mambo mengi kuhusu udereva au ndio sheria tu imewekwa hivo

Asante sana
Mkuu je kama ni miaka miwili ma nusu inakuwaje
 
Back
Top Bottom