Jackomwanda
Member
- Dec 23, 2016
- 99
- 80
Wakimalizana na sisi wataamia kwenu hakuna aliye salama
Acha utoto au uzumbukuku ni mara ngapi watu "hujeruhiwa" kwenye fumanizi na huwa hawaelezi kilichotokea labda picha au video zitoke na wengine wasipopata ushauri huishia kujiuaKulingana na gazeti la Mwananchi polisi wanasema walikuta karatasi ambalo marehemu aliandika kuhusu kugawa mali zake. Lakini hakukuwa na maandishi yoyote kuwa aliandika kuwa ameamua kuutoa uhai wake au kujiua.
Alipotekwa mara ya kwanza na kurudishwa hakutaka hata kueleza ndugu zake alikuwa wapi na nini kimetokea, badala yake akadai kuwa alichanganyikiwa. Hapo inaonyesha kabisa kuna kitu alikuwa ANAOGOPA kusema kulingana na hayo yaliyomkuta huko.
Kuamua kuandika mgao wa mali zake inaweza kuwa alifanya tahadhari maana nadhani alihisi kuwa muda wowote wanaweza kummaliza na kumuua. Kwa hiyo kuandika mgao wa mali SIYO guarantee kuwa alijinyonga hasa ukuangalia mlolongo mzima wa mambo yaliyotokea
Washukuru Mungu tu...kumtafuta mpotezaji ni kujipoteza mwenyewe!Familia Kama INA pesa iwalipe kampuni za udukuzi za nje ( Google) watrace call za mwisho mwisho za marehemu watawapata wahusika wa hack information zao simu zote urekodiwa duniani au wamwachie Mola nae atawalipa wadhalimu juu ya yote.
Jinai haina ukomo,Washukuru Mungu tu...kumtafuta mpotezaji ni kujipoteza mwenyewe!
Kama walivyogundua wapi??Tiacheeni polisi wamalize uchunguzi
Sababu watagundua sababu
Ova
Inabidi tutulie RIP Rafiki yangu Lwajabe. Ipo haja ya kukaa kimya na kuwa mtazamaji hodari bila kufungua mdomo wako. Hicho kitatusaidia, na vizazi vyetu.
Polepole tunaifanya tabia, baadaye itakuwa utamaduni na kuubadilisha itatuchukua maisha yetu yote!
Upo sahihi akina Bulele, Johns Byarushengo, mbunge innocent Bashungwa hamjafanya haki! Alipokuwa hai aliwasaidia leo hii nyie wanyambo mnamsahau? Angekuwa mchagga kabila langu tusingekubali. Ona Mpare Naomi ndugu zake walivyopambana, mpaka ukweli ukajulikanaMimi nitawarahumu wanyambo mlioko dar. Mimi nilienda msibani Jana. Watu walikuwa wakijaribu kuongelea kilichojiri, wanyambo wanakukimbia. Napenda niwaulize maswali....
Huwezi kuhushisha kifo hiki na serikali bali wabaya wake.Inabidi tutulie RIP Rafiki yangu Lwajabe. Ipo haja ya kukaa kimya na kuwa mtazamaji hodari bila kufungua mdomo wako. Hicho kitatusaidia, na vizazi vyetu.
Kama ungejua!Ni kama Awamu ya 5 walivyobadilisha au wanavyotaka kubadilisha tabia na utamaduni wa ufisadi, rushwa, dhuluma na uhujumu uchumi. Unaona wale wote walioguswa wanavyopiga kelele utadhani mwisho wa dunia umefika. Kubadilisha tabia na utamaduni wa kifisadi ili watu waanze tena kuheshimu vipato vyao halali, waache kuiba mali za umma, waache kuuza madawa ya kulevya, waache ujangiri, walipe kodi stahiki nk itatuchukua muda mrefu sana ila ni jukumu letu sote.
Mkuu wasiojulika ni jina tu, si kitengo anachokiongoza bashite?Watu wasiojulikana ndo wanaendesha hii nchi, ni hatari sana. Alafu eti tunajinasibu kuwa ni nchi ya amani huku watu wasiojulikana wakitamba kila kona.