TANZIA Leopold Kweyamba Lwajabe amekutwa amefariki Mkuranga baada ya kupotea wiki iliyopita

Pole kwa msiba , lakini kuna jambo jina nitatiza
Moja alikuwa mpole hivyo uwezekano wa kufarakana na jirani au majirani ni mdogo

Pili alikuwa mtu mwenye uweledi hivyo alikuwa si mbadhirifu wa Mali ya umma

Sasa unajiuliza nani alikuwa na uhasama naye ?? Jamiii iliyo mzunguka??
Au yeye mwenyewe kwa kutoeleza vizuri alivyo potea Mara ya kwanza nine hasa has a kilitokea na je issue ya kuitwa polisi lipoje ikiwa alikuwa mweledi au kama ni kutokana na kutekwa Kwake hapo awali

Itajulikana familia INA majonzi Kwa sasa labda aliprint aliwaachia familia maagizo au yatakayomkuta.
 
aliyekua mkuu wa Kitengo cha EU, Wizara ya Fedha Leopard Lwajabe .... Hatuna tofauti na nyumbu sasa mbele ya simba na chui
Hapo kuna mambo mengi yamejificha, 1. Kama watu walipiga sana hapo Wizarani kipindi hicho cha JK especially pesa za misaada toka nje kama za Gaddafi 20million usd, huo ni mfano mmoja, hili kuficha evidence kwenye mkono wa sheria ikabidi watuhumiwa watumiye mbinu mbadala wa kumtoa kafara, wengine wapone. Rejea jamaa wa mafuta EWURA aliyetoka kutoa ushaidi bungeni kufika Dar wakakuta amejinyonga au kunyongwa kuficha maovu ya wajanja. 2. Wake za watu maana alikuwa na pesa hivyo angeweza kubeba mwanamke yeyote wa sasa hivi hawa. Lakini number moja yaweza kuwa sawa
 
Unaijua saikolojia ya kujiua? Yaani utoke dar ukajiue Rufiji? Kujiua ni kitendo kisicho cha hiari maamuzi ya kujiua na kitendo cha kujiua huwa havipishani ndani ya dakika 5 huwa ni illusion maruweruwe hadi ufike rufiji ile dhamira ya kujiua huwa ishatoweka sababu njiani ushaingiza image nyingi utakazo kutana nazo.Ukikua utaelewa.
Watu wangapi wanachukua muda kupanga atakavyo jiondoa duniani au unataka kusema hayo maandishi yake uliandika wewe na sio marehemu
 
Watu wangapi wanachukua muda kupanga atakavyo jiondoa duniani au unataka kusema hayo maandishi yake uliandika wewe na sio marehemu

Ungefatilia kisa kizima usingeropoka utekwe mara Mbili then ujinyonge
 
Yani wakati ndugu yake anahojiwa na Mwanahalisionline Tv nilibaki na maswali chungumzima kuhusu kifo cha kutatanisha cha huyu bwana.Jamaa anadai siku ya tukio,marehemu alimtuma dereva wake akairudie simu ambayo alisema ameisahau nyumbani.Haijulikani kama kweli aliisahau simu au ni maelekezo ya kumuondoa dereva hili wauwaji watekeleze hilo jambo.Kwani baada ya dereva kuamrishwa na bosi wake arudi nyumbani kuifuata simu,jamaa ndio siku hiyohiyo alitoweka.

Jengine,wakati ndugu wanataka kuitisha press conference juu ya kutoonekana kwa ndugu yao pale New Africa Hotel,ghafla hapohapo walipigiwa simu na askari kwamba mwili umepatikana.

Tatu,ndugu wanadai wakati wa kuripoti tukio la kutekwa baada ya kurudi mara ya kwanza kwa marehemu wakiwa naye,polisi waliwazungusha sana.Yani walilichukulia poa.

Hitimisho:This to my side is a well planned assassination.Hila ipo siku watalipa damu hizi.
 
Huu utekaji naamini kabisa wakimaliza Raia wa kawaida ipo siku watahamia kwa viongozi, ni hali mbaya sana ambayo inaweza kuingiza nchi Kwnye machafuko makubwa!
 
Tuache unajimu na mambo ya kulaani ttusivyo jua imethibitishwa kwa maandishi yake mwenyewe amejiua na kuacha mgao wa mali zake na ngombe wa kuchinjwa kwenye msiba ni wanne, hays wazee wa saccos leteni santuri nyingine

Kulingana na gazeti la Mwananchi polisi wanasema walikuta karatasi ambalo marehemu aliandika kuhusu kugawa mali zake. Lakini hakukuwa na maandishi yoyote kuwa aliandika kuwa ameamua kuutoa uhai wake au kujiua.

Alipotekwa mara ya kwanza na kurudishwa hakutaka hata kueleza ndugu zake alikuwa wapi na nini kimetokea, badala yake akadai kuwa alichanganyikiwa. Hapo inaonyesha kabisa kuna kitu alikuwa ANAOGOPA kusema kulingana na hayo yaliyomkuta huko.

Kuamua kuandika mgao wa mali zake inaweza kuwa alifanya tahadhari maana nadhani alihisi kuwa muda wowote wanaweza kummaliza na kumuua. Kwa hiyo kuandika mgao wa mali SIYO guarantee kuwa alijinyonga hasa ukuangalia mlolongo mzima wa mambo yaliyotokea
 
Duh ! maumivu lakin naamini haya matukio hipo siku isiyokuwa na jina yatajurikana
 
Kifo hakikosi sababu...
Lazima polisi wafanye uchunguzi wa kina ili wajue kwann injinia alijinyonga!

Ova
 
Back
Top Bottom