Leonardo da Vinci MTU MWENYE VIPAJI VINGI VINGI KATIKA DUNIA YETU HII | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Leonardo da Vinci MTU MWENYE VIPAJI VINGI VINGI KATIKA DUNIA YETU HII

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Dec 27, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Leonardo da Vinci


  [​IMG] [​IMG]
  Leonardo da Vinci


  Leonardo Da Vinci (15 Aprili 1452 – 2 Mei 1519) alikuwa mtu mwenye vipaji vingivingi kutoka nchini Italia. Kifupi, alikuwa mwanahisabati, mhandisi, mwanasayansi, mgunduzi, mwanaanatomi, mchoraji, mchongaji, msanifu majengo, mwanabotania, mwanamuziki, na mwandishi. Leonardo alikuwa mdadisi wa kila kitu asilia. Alitaka kujua kila kitu kinavyofanya kazi. Alikuwa hodari sana katika masomo, kuunda na kutengeneza vitu vya aina mbalimbali tena vya kupendeza.[1]
  Watu wengi hufikiria kwamba Leonardo alikuwa mmoja kati ya wachoraji bora wa muda wote. Watu wengi hufikiria kwamba alikuwa mtu aliyebarikiwa vipaji katika historia ya maisha.[2] Mwanahistoria wa sanaa Bi. Helen Gardner alisema kwamba hakuna mtu aliyewahi kuwa kama yeye kwa sababu alikuwa na shauku na vitu vingi sana: "...Akili yake na utu wake unaonekana kuwa zaidi ya mtu, ni mtu wa ajabu na tofauti".
  Leonardo alizaliwa mjini Vinci ambapo ni mji mdogo ulio karibu na Florence nchini Italia. Alifunzwa kuwa msanii na mchongaji na mchoraji Verrocchio. Alitumia sehemu kubwa ya maisha yake akimtumikia tajiri mmoja maarufu wa Kiitalia. Katika miaka yake ya mwisho aliishi katika nyumba yake nzuri aliyopewa na Mfalme wa Ufaransa.
  Leonardo aliweza kufanya vitu vya aina nyingi vya kijanja, lakini alikuwa maarufu sana kama mchoraji. Miongoni mwa picha zake mbili maarufu duniani ni pamoja na Mona Lisa na Last Supper. Amefanya michoro mingi sana. Mchoro unaojulikana sana ni Vitruvian Man. Unajulikana sana hata Homer Simpson na Garfield ambazo zilichorwa kwa mraba na mzunguko ili kuonekana kama mchoro. Leonardo siku zote alikuwa akifiria kugundua mambo mapya. Vitu vingi alivyogundua havikuwahi kufanywa. Hata hivyo, tunajua fikra zake, kwa sababu aliweka kwenye vijitabu na kuandika na kuvichora mara kwa mara. Baadhi ya nadharia alizofikiria ni pamoja na helicopta, kifaru, kikokotoo,roboti na vifaa vinavyogeuza nishati ya jua kuwa umeme.

  Maisha


  Utotoni mwake, 1452–1466

  [​IMG] [​IMG]
  Mchoro uliojulikana awali wa Leonardo, Arno Valley, (1473) - Uffizi


  Leonardo alizaliwa mnamo tar. 15 Aprili, 1452, mjini Tuscan mji wa kilima cha Vinci, katika mabonde ya Mto Arno. Babu yake, Ser Antonio, anajuvunia kwa kuweka kumbukumbu ya maelezo. Wazazi wa Leonardo walikuwa hawaja oana. Baba'ke alikuwa mwanasheria,

  Messer Piero Fruosino di Antonio da Vinci.[3][4] Mama'ke, Caterina, alikuwa muhudumu. Yawezekana alikuwa mtumwa kutoka Mashariki ya Kati.[5][6] Jina kamili la Leonardo lilikuwa "Leonardo di ser Piero da Vinci", ambalo lina manaa ya "Leonardo, mtoto wa
  Messer (Mister au Bwana) Piero kutoka Vinci".

  Leonardo alitumia miaka yake mitano ya awali akiishi katika nyumba ya shamba na mama'ke. Halafu akaja kuishi mjini Vinci na baba'ke, mke wa baba'ke aliitwa Albiera, mabibi/mababu zake na wajomba zake, Francesco. Wakati Leonardo kakua, aliandika vitu

  viwili tu kuhusu maisha yake ya utotoni. Alikumbuka kwamba alivyokuwa amelala kwenye kitanda chake cha watoto nje ya nyumba yao ndege mkubwa alikuwa akipaa na kumzungukazunguka juu yake. Mikia yake ikawa inamfutafuta sura yake.[7] Kumbumbu

  nyingine muhimu ya Leonardo ilikuwa vipi aligungua pango milimani wakati anapeleleza. Alikuwa na hofu kubwa sana huenda kukawa na kiumbe cha ajabu kikubwa kimejificha mule ndani ya pango. Lakini pia alikuwa na hamu na shauku ya kujua nini kilichopo ndani mule.

  Leonardo alianza kuchora tangu yungali bado kijana. Giorgio Vasari aliandika kuhusu maisha ya Leonardo kwa ufupi baada ya kifo chake. Ameelezea hadithi za kuvutia kibao kuhusu ujanja aliokuwa nao Leonardo. Anasema kwamba Leonardo alichora bamba la

  taarifa la mbao-mzunguko likiwa na picha ya mijoka inayotema moto. Messer Piero alichukua michoro ya mwanawe hadi Florence na kuiza kwa wauzaji wa bidhaa za kisanaa.[8]
  [​IMG] [​IMG]
  The Baptism of Christ (1472–1475)—Uffizi, by Verrocchio and Leonardo


  Kifo

  Mwaka 1516 Leonardo alikwenda Amboise, Ufaransa, baada ya kupata mualiko kutoka kwa mfalme Francis wa kwanza na kati ya mizigo aliyosafiri nayo ulikuwemo mchoro maarufu wa Monalisa. Leonardo aliishi Amboise toka mwaka huo wa 1516 mpaka mwaka

  1519, alifariki Mei 2 1519 mjini Amboise na kuzikwa St. Hubert akiwa na umri wa miaka 67, lakini taarifa za afya yake hazikuwa nzuri kwasababu Leonardo alipata ugonjwa wa kiharusi toka mwaka 1517 lakini taarifa za ugonjwa wake zikatolewa wiki chache kabla ya kifo chake.

  [​IMG] Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
  Je, unajua kitu kuhusu Leonardo da Vinci kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
  Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
  Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  Rudishwa kutoka "Leonardo da Vinci - Wikipedia, kamusi elezo huru"

   
 2. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #2
  Dec 27, 2010
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Niliwahi kusoma mahali fulani kuwa alikuwa Shoga.
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Dec 27, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,599
  Likes Received: 18,607
  Trophy Points: 280
  picha yake ya Mona Lisa ndio the most expensive painting ever was mpaka sasa. mchoro wake mwingine wa Last Super ndio most popular painting ambayo ina hang ndani nyumba za karibu kila Mkatoliki nami nikiwemo.
  Very proud of it.
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Dec 27, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  una uhakika wa hilo unalolisema?
   
 5. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #5
  Dec 27, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mbona umerukia kwenye private domain tena jamani? Alivyokuwa kichwa hauoni na alivyochangia kwenye modern marvels?
   
 6. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #6
  Dec 27, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Aliyewahi kuripotiwa kuwa ni shoga ni Michelleangelo Bruanot ambaye ndiye aliyefanya ramani ya kanisa la Roma na vatican Square, Pia alidesign and construct Papal Church (Sistine Chapel) pamoja na kuweka michoro maarufu kwenye ceiling pamoja na asilimia 80 ya sculpture za pale vatican....

  Da vinci ni multi purpose artist kama anavyotabanaisha MziziMkavu.

  Huyu na wenzake yaani Michelleangelo na Raphael wanatajwa sana kuwa ni waasisi wa mapinduzi ya sanaa ya uchoraji. walikuwa wanafanya tafiti za kutisha, walituwekea misingi ya anatomy kwa kufanyia tafiti maiti na kufukua makaburi kupata skeletones za kufanyia tafiti.

  Ninawaheshimu sana hawa walumendago na wengineo. najua mnamkumbuka Pablo Picaso ambaye alikuwa maarufu kwa sanaa ya transformation from reality to cubism (wengi husema Abstract)... kuna wengi wengi na orodha haiishi. tafuta kitabu cha ART WITHOUT BLUSHIT cha John Farhman... amefanya summary nzuri ya history of art from flat yaani rock paintings, Egyptian arts to modern renaissance.....

  MZIZIMKAVU thanx kwa bandiko lako. umegusa mtima wangu...
   
 7. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #7
  Dec 27, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Tafuta mchoro wake mwingine wa Adoration of Magi uone msanii huyu alivyokuwa kichwa... Kuna sketch yake ya the womb ambayo wanasayansi wa awali walitumia kusoma mfumo wa mtoto tumboni na tumbo la uzazi, the guy was brilliant.
  Sanaa zake nyingi hakuzifanyia finnishing na alizomalizia chache zilipata umaarufu mkubwa,
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  Dec 27, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Leonardo da Vinci was a super-being of his time..a man of a spectrum of knowledge kwa wakati ule. hii thread inanikumbusha Leonardo Express kutoka Fumicino kwneda Roma Termini, not a very state of art express lakini ndio hivo to the Italian Standards.
   
 9. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #9
  Dec 27, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  nadhani ni vyema pia akachambuliwa kama tunavyowachambua wasanii wetu wa leo kuona kama maisha yake binafsi yalikuwa kivutio au ilikuwaje...

  Kumbuka Michelleangelo alikuwa anawaudhi sana watawala wa vatican (Papa na squad yake) hivyo sehemu kubwa ya kazi alizofanya ilikuwa ni kama adhabu kulipia makosa yake. hakupenda sana kulifanyia kazi kanisa ambalo hakuwa na aimani nalo kwa sana.
  Tujadili na personal demain yake pia ilikujua affection ya inventions zake
   
 10. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #10
  Dec 27, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  huyu jamaa, alikuwa balaa, picha zake ni nzuri, na zina mafumbo babu kubwa
   
 11. L

  Leornado JF-Expert Member

  #11
  Dec 27, 2010
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  I gat my name from him.......:whoo:
   
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #12
  Dec 27, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,599
  Likes Received: 18,607
  Trophy Points: 280
  kama umebahatika kupata jina la Leornado toka kwa Da Vinci, then, lazima kuna baadhi ya vipaji vyake utakuwa navyo, jee umebahatika kuwa na nini?.
   
 13. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #13
  Dec 27, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,599
  Likes Received: 18,607
  Trophy Points: 280
  Wanabodi, kila linapotajwa jina la Leonardo Da Vinci, mimi humkumbuka school mate wangu primary school, ikiitwa Peter Bakilana (RIP) ambaye ndiye aliyenifungua macho kuhusu Monalisa, way back in 1978!. Peter naye alikuwa mchoraji na kichwa mbaya.
  Mungu amweke mahala pema peponi Peter Bakilana.
   
 14. L

  Leornado JF-Expert Member

  #14
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Msanii sema arts yangu haijakua kama ya kwake but soon it will be out.
   
Loading...