Picha ya Yesu wawili kutoka kwa mchoraji da Vinci

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,447
331795251_676862034209976_1887259541270059323_n.jpg

YESU WAWILI
Picha ya ukubwa wa futi 15 kwa futi 29 kwenye ukuta wa kanisa, The Last Supper ya mchoraji Leonardo da Vinci, inayoonyesha mlo wa mwisho kati ya Yesu na wanafunzi wake kabla ya kukamatwa; muda mfupi baada ya Yesu kumtamkia Yuda kuwa atamsaliti, inaweza kuwa ndiyo kazi ya sanaa inayopendwa zaidi, iliyopata kufanyiwa tafiti nyingi zaidi, na kunakiliwa na wachoraji wengine kuliko kazi nyingine yoyote!

Picha hiyo imeacha simulizi nyingi mno na moja ya simulizi hizo (ambayo pia husimuliwa kwa namna nyingi) ni jinsi sura za watu kwenye picha zilivyopatikana: Inasemekana mchoraji alitumia muda mrefu sana akitafuta watu wa kutazamia wenye sura na tabia zinazoendana na wanafunzi halisi wa Yesu. Hata picha ilipokamilika baada ya miaka mitatu, ilikaa muda mrefu ikiwa haina kichwa cha Yuda mpaka kanisa likapeleka malalamiko kwa mfalme aliyekuwa ametoa kandarasa ya kazi hiyo. Leonardo kwa upande wake alijitetea kuwa hajampata mtu mwenye sura iliyoendana na wajihi wa Yuda.

Malalamiko yalipozidi, mchoraji akaamua kwenda kubahatisha kwenye magereza ya mji wa Milani walikofungwa wanyang’anyi, wezi na matapeli wa kila aina. Humo akapata sura aliyokuwa anaitafuta, sura ngumu, macho makali na isiyo na huruma—Alikuwa ni mtu aliyefungwa kwa jinai nyingi na aliyekuwa anasubiri kunyongwa!
Haraka mfalme akaidhinisha kibali cha kumtoa magareza kwa muda na Leonardo akaanza kazi ya kutazamia sura yake. Walipomaliza uchoraji, mfungwa alimfuata Mchoraji na kumwuliza kama alikuwa anamkumbuka, Leonardo akasema hakumbuki kukutana naye kabla.

Mfungwa akamkumbusha kuwa yeye ndiye aliyemchora kama Yesu huko nyuma. Kisha, akalia sana na kujutia uhalifu uliopelekea kuharibika kwa maisha yake: “Nimeanguka kiasi gani, jana nilikuwa Yesu, na leo nimekuwa Yuda!

Credit: James Gayo
 
Mimi na akili zangu timamu, nimemfuatilia VINCI lakini sijawahi kupata majibu kamili...

Kazi zake nyingi zina kontrovesho aisee
 
Mimi na akili zangu timamu,nimemfuatilia VINCI lakini sijawahi kupata majibu kamili...

Kazi zake nyingi zina kontrovesho aisee
Mkuu nadhani hujaelewa kinachozungumziwa hapo. Subiri GT(Great Thinkers) waje kukupa maelezo
 
Jana nilikuwa kwenye kibanda cha miamala ya mitandao ya pesa,nikaona frame INA picha ya Yesu ambaye ni tofauti na picha nyingine maarufu ambazo huenda zimezoeleka Sana.

Huu ni mtihani Sana kwakweli.
Jambo la muhimu uliweza kuitambua kuwa hiyo sura ni kama sura ya Yesu. Kwa kutambua huko tayari umeshainjilishwa
 
331795251_676862034209976_1887259541270059323_n.jpg

YESU WAWILI
Picha ya ukubwa wa futi 15 kwa futi 29 kwenye ukuta wa kanisa, The Last Supper ya mchoraji Leonardo da Vinci, inayoonyesha mlo wa mwisho kati ya Yesu na wanafunzi wake kabla ya kukamatwa; muda mfupi baada ya Yesu kumtamkia Yuda kuwa atamsaliti, inaweza kuwa ndiyo kazi ya sanaa inayopendwa zaidi, iliyopata kufanyiwa tafiti nyingi zaidi, na kunakiliwa na wachoraji wengine kuliko kazi nyingine yoyote!
Picha hiyo imeacha simulizi nyingi mno na moja ya simulizi hizo (ambayo pia husimuliwa kwa namna nyingi) ni jinsi sura za watu kwenye picha zilivyopatikana: Inasemekana mchoraji alitumia muda mrefu sana akitafuta watu wa kutazamia wenye sura na tabia zinazoendana na wanafunzi halisi wa Yesu. Hata picha ilipokamilika baada ya miaka mitatu, ilikaa muda mrefu ikiwa haina kichwa cha Yuda mpaka kanisa likapeleka malalamiko kwa mfalme aliyekuwa ametoa kandarasa ya kazi hiyo. Leonardo kwa upande wake alijitetea kuwa hajampata mtu mwenye sura iliyoendana na wajihi wa Yuda.
Malalamiko yalipozidi, mchoraji akaamua kwenda kubahatisha kwenye magereza ya mji wa Milani walikofungwa wanyang’anyi, wezi na matapeli wa kila aina. Humo akapata sura aliyokuwa anaitafuta, sura ngumu, macho makali na isiyo na huruma—Alikuwa ni mtu aliyefungwa kwa jinai nyingi na aliyekuwa anasubiri kunyongwa!
Haraka mfalme akaidhinisha kibali cha kumtoa magareza kwa muda na Leonardo akaanza kazi ya kutazamia sura yake. Walipomaliza uchoraji, mfungwa alimfuata Mchoraji na kumwuliza kama alikuwa anamkumbuka, Leonardo akasema hakumbuki kukutana naye kabla.
Mfungwa akamkumbusha kuwa yeye ndiye aliyemchora kama Yesu huko nyuma. Kisha, akalia sana na kujutia uhalifu uliopelekea kuharibika kwa maisha yake: “Nimeanguka kiasi gani, jana nilikuwa Yesu, na leo nimekuwa Yuda!

Credit: James Gayo
images (81).jpeg
 
Back
Top Bottom