Leo Wifi atajibeba...

Leo Wifi atajibeba...

Leo atajibeba... Nimemchoka nimechoka wifi yangu na maneno yake ya kunisakama eti sizai... Najaza choo wakati ndoa yenyewe hata mwaka mmoja bado... Leo kaingia choo cha kiume... Nimemkaribisha chumbani nimemfungulia bafu la chumbani kwangu ameoga, nimempa taulo langu amejifutia,kila kitu nimeshea nae kila kitu changu na night dress yangu nimempa amevaa... Sasa nimemfungia chumbani kwangu... Nimemwambia tumeshea kila kitu sasa na mume wangu anakuja yupo njiani na yeye tushee... Ye si anaona mi nafaidi... Alale na kaka yake apate mimba kama anaona mie nimeshindwa...

Ha ha ha haaa...duu kitamchwea leo lool.

Ila kaka mtu akija amkute bed room kwake kitasomeka kweli?
 
kusema kweli kuna wamama ukiolewa kwao cha moto utakiona ila sidhani kama kuna haja ya kugombana nae kuna wan awake hadi zinapigwa ngumi hadi na baba mkwe zao!
sema na jamii inatakiwa ibadilike jamani kuna wazazi wa upande wa kiume wanawamistreat watoto wa watu jamani!
yaani hamu yote ya maisha inaisha mtu hapumui eti kama huyu dada ameolewa hata mwaka bado atazaaaje sasa?
kama mwaka bado uolewe lini ? ulee mimba lini? uzae lini si fair lakini? ila na mwezetu kaovereact!
Mara nyingi unapoona mama mkwe au ndugu wengine kuleta fujo nyumbani kwako inategemea msimamo wa mwanaume kuna wanaume hawana msimamo yaani wao wanataka mke awe wa family hapo ndio penye shida. Hata neno la Mungu liko wazi kwamba mtawaacha wakwenu nanyi mtakua mwili mmoja. Sasa kuna wanaume huwa hawataki kuwaacha wakwao na kuambatana na wake zao tukumbuke huwezi kwenda kinyume na neon la Mungu. Ndugu wote wanatakiwa wabaki nafac ya wageni na si sehemu ya familia. Kama wifi akubali nafac yake ya mgeni lkn pia hatuwezi kubadili tabia zao daima tuishi nao kwa akili.
 
mgeni gani huyu naona kakosea no ....anataka kunigegeda mimi akagegede kwao !
yaani kwa kweli keshaharibu hata mwaka bado jamani! i wish angeleta hii thread kabla hajapiga hili janga!
amwambie tu wifi mi nilikuwa natania ila yaishe..maisha yenyewe mafupi then uishi na mbifu tena na watu wa nyumbani kwako?? ode ma mi siwezagi
hahahah!!! eto we kusemba nsanyin yeu tena kulara atiri nta sumuni she ndu we mwendekeza kabisa fooo!!!

kama ana hekima basi aongee na wifi yake kiutu uzima amwombe samahan yaishe. ila kama anataka kutoshana nae nguvu aendelee tuu manake si ndio kazi ya wenye nguvu za midomo?

huo muda wa kumfanyia haya wifi yake ulitosha kukaa chini na kusema na Mungu juu ya nini anataka na pengine ndio muda uliokuwa umebaki ama kuda sahihi wa yy kueleka ombi lake lakin ibilisi akamsimamia akaikosa neema hiyo.
 
Mara nyingi unapoona mama mkwe au ndugu wengine kuleta fujo nyumbani kwako inategemea msimamo wa mwanaume kuna wanaume hawana msimamo yaani wao wanataka mke awe wa family hapo ndio penye shida. Hata neno la Mungu liko wazi kwamba mtawaacha wakwenu nanyi mtakua mwili mmoja. Sasa kuna wanaume huwa hawataki kuwaacha wakwao na kuambatana na wake zao tukumbuke huwezi kwenda kinyume na neon la Mungu. Ndugu wote wanatakiwa wabaki nafac ya wageni na si sehemu ya familia. Kama wifi akubali nafac yake ya mgeni lkn pia hatuwezi kubadili tabia zao daima tuishi nao kwa akili.
umenena vyema sana, unapooa ama kauolewa tayari umetengeneza familia yako ambayo lazia itakuwa na mapungufu yake lkn pia itakuwa na maongeo yake. ni vyema kukubali kwamba hii ni familia na yyte ajaye hapa ni mgeni na atahudumiwa kwa nafasi yake kama mgeni.

lkn pa na sisi wanawake tujifunze maisha ya kaka yako yanakuhusu nini wewe wifi?? kwann kwenda kwa kaka yako na kuleta chokochoko zisizo na mpango wala kichwa? tukumbuke kwamba na sisi kama tutaolewa basi tutakuwa ni wageni kama amabvyo wake wa aka zetu ni wageni na kama sio sisi basi hata watoto wetu watakuja kuwa wageni kwenye miji ya watu hivyo tujiheshimu na kuwapenda wengine. tuwe na mipaka na miji ya watu
 
ahahaaaa kwiiii hapo black!
yaani dada yangu una busara wewe ! kweli huo muda angepiga goti kwa kweli! nimependa huu ushauri kwa kweli ! kabla ya kutenda hebu tufikiri
 
tatizo kitchen party badala watu waende na biblia au misahafu kufundisha wamwali jinsi ya kuishi na hizo familia mpya ..watu wanajibebesha vigodoro na mikeka! ndoa haituzwi kwa vigodoro etiii!! vigodoro vipo kil mahali! kwanza wanaotufundisha mbele na vigodoro vyao wameachika long!
 
ni kwelii kabisa umenena vyema sama mdogo wangu.
binafsi huwaga nasema penye magumu sana usitangulize hasira laaa kaa chini mwombe Mungu akue faraja kisha akuonyeshe njia basii.
 
Imagine nakuta mke wangu amemfungia dada yangu tumbo moja chumbani ninapolala, uamuzi wa kwanza ni kumwajibisha mke wangu halafu ndio nisikilize ugomvi wao. Huu uamuzi mbaya sana
 
umenena vyema sana, unapooa ama kauolewa tayari umetengeneza familia yako ambayo lazia itakuwa na mapungufu yake lkn pia itakuwa na maongeo yake. ni vyema kukubali kwamba hii ni familia na yyte ajaye hapa ni mgeni na atahudumiwa kwa nafasi yake kama mgeni.

lkn pa na sisi wanawake tujifunze maisha ya kaka yako yanakuhusu nini wewe wifi?? kwann kwenda kwa kaka yako na kuleta chokochoko zisizo na mpango wala kichwa? tukumbuke kwamba na sisi kama tutaolewa basi tutakuwa ni wageni kama amabvyo wake wa aka zetu ni wageni na kama sio sisi basi hata watoto wetu watakuja kuwa wageni kwenye miji ya watu hivyo tujiheshimu na kuwapenda wengine. tuwe na mipaka na miji ya watu
Ni kweli maisha ya kaka yangu hayanihusu. Lkn kwa bahati mbaya sisi waolewaji sometimes tuna overdo , unaweza kuikuta familia iko shwari kabisa lkn kwa sababu ulishajiaminisha kwamba upande wa pili hawana jema basi waweza anzisha vituko vya karne. So bado nipo kwa mwanaume anapaswa kusimama nafac yake , awacontrol ndugu na mkewe. Lazima kila mmoja aijue nafac yake na pia tusiwape nafac watu wengine kuja kutuambia kwamba oooh wifi yako kasema eti huzai, tusikubai kufanyia kazi taarifa hizi kwani mara nyingi hata wanapolaumu huwa hawatuambii live bali kuna vimessenger huwa vyenyewe vipo ili kutupa habari. Kama taarifa haihusu kukudhuru basi iache ipite mpaka utakapopewa live . Na mara uambiwapo live basi omba hekima ya Mungu namna ya kumjibu mhusika kwa hekimaa. Tukumbuke haya tunayopitia sisi sio wa 1 , tujifunze kwa waliopita je wao walifanyaje juu ya haya.
 
ni kwelii kabisa umenena vyema sama mdogo wangu.
binafsi huwaga nasema penye magumu sana usitangulize hasira laaa kaa chini mwombe Mungu akue faraja kisha akuonyeshe njia basii.
ila kwa watu bwana hakuhitaji ubabe etii! ukitaka kufanikiwa kuwa mpole
 
Imagine nakuta mke wangu amemfungia dada yangu tumbo moja chumbani ninapolala, uamuzi wa kwanza ni kumwajibisha mke wangu halafu ndio nisikilize ugomvi wao. Huu uamuzi mbaya sana
huwa mnafurukuta basii!!!!!!
 
tatizo kitchen party badala watu waende na biblia au misahafu kufundisha wamwali jinsi ya kuishi na hizo familia mpya ..watu wanajibebesha vigodoro na mikeka! ndoa haituzwi kwa vigodoro etiii!! vigodoro vipo kil mahali! kwanza wanaotufundisha mbele na vigodoro vyao wameachika long!
Aaah jamii ilishapotoka long time ago. Binti anatakiwa aanze kufundishwa kuishi na watu tofauti tofauti toka akiwa kigoli, si unajua ngombe hanenepi siku ya mnada. Tunajifunza maisha bora toka tukiwa nyumbani . Kama mama hawapendi mashangazi na bibi basi asitegemee binti atabadilika siku ya kitchen party. Kwenye dini nako business kwa kwenda mbele tumeacha kabisa kuwafundisha vijana maisha ya kiafrica tumekazania utajiri na Baraka za mwilini. Ingefaa kua na mafundisho ya vijana toka wakiwa na 17 yrs ili tuweze kujenga familia bora kwa sababu huko majumbani wazazi wako busy kutafuta fedha.
 
ni kweli dear ...mambo mengi tunajifunza toka kwa jamii inayotuzunguka! ila siku hizi dunia imepanuka kuna jinsi nyingi za kujifunza ..kuna mitandao kama hivi nk..ina maana kama wazazi wako ni walevi na wewe uwe mlevi kisa home kwenu walevi? yaani na kukua kwako hujafahamu kwamba hilo ni jambo baya! mi naona ukiwa mbaya ni wewe mwenyewe umependa bana!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom